Articles by "sensa2022"
Showing posts with label sensa2022. Show all posts

Na Amani Mongi : MsumbaBlog

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewaagiza  viongozi wote katika ngazi za Wilaya,Halmashauri na wakuu wa idara mkoani Arusha kwenda kukagua maeneo yote yaliyopitiwa na zoezi la sensa ya watu na makazi ili kujiridhisha mwenendo mzima wa zoezi hilo kabla ya tarehe ya mwisho. 

Rc Mongella amebaini hayo baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya sensa ya watu na makazi katika Wilaya ya Longido  na kubaini amebaini uwepo wa baadhi ya maeneo yaliyokadiriwa kuwa na kaya yalikuwa chini au zaidi na kuwataka viongozi wa wilaya na halmashauri zote kuyabaini hayo maeneo na kuchukua hatua haraka ili kuhakikisha kaya hizo zinahesabiwa

"Lengo letu kuu sio tu kumaliza zoezi la sensa kwa muda uliopangwa bali kuhakikisha kila kaya inahesabiwa hivyyo niwaagize viongozi wa makarani kuhakikisha wale wanaomaliza kuhesabu katika maeneo yao mapema wapangiwe maeneo mengine ambayo yanauhitaji zaidi ili kaya zote ziweze kufikiwa" Rc Mongela

Kwa upande wake Karani kutoka Wilayani Longido Frida Chome amesema zoezi la sensa kwa upande wake limeenda vizuri. na amefanikiwa kuhesabu kaya 70 na akahamishiwa kwenye eneo jinqine

Frida ameendelea kueleza kuwa changamoto kubwa aliyokutana nayo ni baadhi ya watu kutowakuta kuenye kaya kwa sababu ya majukumu yao ya kikazi hivyo kupelekea kufanya zoezi la sensa kufanyika hadi  wakati wa usiku.

Hata Hivyo Samueli Steven ambaye ni miongoni mwa wananchi waliohesabiwa na amesema zoezi la sensa ya watu na makazi ni nzuri kwani litasaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo na huku akimshukuru Rais Samia  Suluhu Hassan kwa kuwezesha zoezi hilo kwa wakati.

RC Mongella anaendelea na zoezi la kufuatia mwenendo mzima wa sensa ya watu na makazi katka halmashauri zote za Mkoa wa Arusha na kutatua changamoto mbalimbali zinazokuwa zimejitokeza katika maeneo hayo.







 


Pamoja na shughuli ya kuhesabu watu ikiendelea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, changamoto ya umeme inasababisha baadhi ya maeneo sensa ya watu na makazi kuendelea kwa kasi ndogo.

Mratibu wa sensa wa Wilaya ya Simanjiro Linus Mboya akizungumza na Mwandishi wetu wa Habari leo Jumatano Agosti 24 amewatoa hofu wana Simanjiro kuwa wote watafikiwa kwani watahesabiwa kwa muda wa siku saba.

"Wana Simanjiro wasihofu watahesabiwa wote kwani baadhi ya vishkwambi havina power bank na maeneo mengine hakuna umeme wa kuchaji ndiyo sababu kunakuwa na kasi ndogo ila watafikiwa wote," amesema Mboya.

Hata hivyo, amesema tangu shughuli hiyo ianze imefanyika inavyopaswa hakuna kishkwambi kilichopotea wala makarani wa sensa kuwa walevi hivyo wanatimiza wajibu wao ipasavyo.

Mkazi wa kijiji cha Shambarai Obeid Sarakikya amesema jana Agosti 23 alishinda nyumbani kwake akiwasubiri makarani wa sensa ili ahesabiwe ila hawakufika.

Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Shujaa Baruti amesema jana hakuhesabiwa ila anasubiria kwani wameelezwa itafanyika kwa muda wa siku saba.

 


KARANI wa Sensa Kata ya Majimoto,  Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi, Kenan Kasekwa, amevamiwa usiku wa kuamkia leo na kuporwa kishikwambi cha kutunzia kumbukumbu za sensa.

Akithibitisha tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Catherine Mashala, amesema karani huyo ambaye ni mwalimu, alivamiwa na mtu aliyevunja kitasa na kuingia chumbani, kisha kubeba kifaa hicho, fedha kiasi cha Sh 760,000, redio na vitu vingine.

“Inavyoonekana alipuliza dawa ya kuwalaza usingizi yeye na familia yake, yule mwizi aliingia chumbani akabeba ka lasketi, kishikwambi, fedha alizozikuta, simu na redio, “alisema Mashala.


 


KARANI wa Sensa ya Watu na Makazi Jiji la Arusha, Sarapia Kiwango ameporwa kishikwambi chake wakati akijiandaa kwenda kuhesabu makundi maalum jana usiku huku mume wake akijeruhiwa.

Akizungumza na mwandishi wa HabariLEO, Mratibu wa sensa ya watu na makazi katika Jiji la Arusha, Maneno Maziku amesema Kiwango aliporwa kishikwambi usiku wakati akienda kuhesabu makundi maalum huku mume wake akijeruhiwa kichwani.

Amesema baada ya tukio hilo Karani huyo alipewa kishikwambi kingine na anaendelea na kazi.

“Ni kweli aliporwa kishikwambi na mume wake kujeruhiwa kichwani lakini ameshapewa kishikwambi kingine anaendelea na kazi lakini pia majeruhi hali yake inaendelea vizuri,” amesema Maziku.

Diwani wa Kata ya Unga Limited, Mahamod Said na Mtendaji wa Kata hiyo, Sophia Laizer wamesema karani huyo alivamiwa na watu waliokuwa na boda boda na kumpora kishikwambi hicho.

“Jana usiku hawa makarani wa sensa waliitwa kwa mtendaji, wakati wanakwenda huko ndiyo akakutana na vibaka waliokuwa kwenye bodaboda wakamjeruhi mumewe na kumpora kishikwambi kisha kutoweka kusikojilikana,” amefafanua Said.


H.T HabariLeo


.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameupongeza Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) alipokuwa akielezwa na Mtaalamu wa Sheria wa taasisi hiyo, Harvey Kombe kuhusu huduma mbalimbali wanazozitoa kwa wananchi alipotembelea banda hilo katika kilele cha Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane Kanda ya Kati jijini Dodoma Agosti 8, 2022

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano MKURABITA, Glory Mbilimonyo akitoa maelezo zaidi kwa RC Senyamule kuhusu baadhi ya wananchi walivyonufaika kwa kupata mikopo kupitia hatimiliki za ardhi.

 


Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
KAMISAA wa Sensa 2022, Anne Makinda ametoa ufafanuzi kwamba ,siku ya sensa agost 23 mwaka huu haitakuwa siku ya mapumziko badala yake kila mmoja ataendelea na shughuli za kimaendeleo .

Aidha amesema , tarehe 23 itakuwa siku maalum ya kuhesabiwa lakini itaendelea taratibu za kuhesabu madodoso Hadi tarehe 28 agost mwaka huu.

Pamoja na hayo ,aliliasa kundi la vijana wakati wakitumia mitandao kuchat pia watumie wasaa huo kuhamasishana kuhusu suala la umuhimu wa Zoezi la sensa ili kutambua vijana waliopo na taarifa zao kuhusiana na suala la ajira.

Akizungumza katika Kongamano la viongozi wa dini pamoja na kuzindua tangazo la umuhimu wa ushiriki wa sensa alisema ,kila mmoja ana wajibu wa kujisensa mwenyewe kwa kutambua wajibu ni wa kila mmoja.

"Mkoa wa Pwani na wilaya ya Kibaha
Nimejifunza Jambo kubwa kujisensa mwenyewe,kilichobaki agost 23 mwaka huu tuweze kujisensa wenyewe ili kupata takwimu sahihi kwani tukifanikiwa Tanzania itakuwa mpya".

"Siku hii sio ya mapumziko Kuna mtu nilimsikia akisema Ni siku ya mapumziko hapana ,kila mmoja ataendelea na shughuli zake Ila atakuwa ameacha taarifa zake katika makazi ambayo alikuwa amelala siku ya Zoezi la sensa"alisisitiza Anne.

Anne alisema, wamejiandaa vizuri mno kwa kutumia teknolojia ya kisasa (kishkwambi ) kurahisisha uhifadhi wa taarifa tofauti na sensa za miaka iliyopita.

Hata hivyo aliomba watu waweke vitambulisho vyao karibu ili wanapopita makarani waweze kujua idadi ya wenye vitambulisho huku mamlaka husika iweze Kuwa na takwimu halisi ya walivyo navyo na wasio navyo.

Vilevile alitoa Rai kwa jamiii kuacha kuwaficha walemavu na badala yake wahesabiwe ili kupata taarifa sahihi ya idadi na aina ya ulemavu walionao.

Kuhusu Wamachinga wameingizwa katika sensa ,Ni kundi muhimu ,ambapo Serikali inataka kujua idadi halisi,wenye vitambulisho kwani mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan ni WAMACHINGA kupatiwa vitambulisho vya ujasiliamali.

"Tushiriki kikamilifu , na Baadhi ya maswali yatakayoulizwa na makarani wa Sensa ni elimu ya wanakaya, shughuli zao za kiuchumi, hali ya uzazi, taarifa za vifo na vifo vitokanavyo na uzazi,ajira, makundi maalum"alisema Anne.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alieleza, mkoa umejipanga Kuwa sehemu ya mafanikio Kwenye Zoezi la sensa .

Alielezea kwamba ,zaidi ya viongozi wa dini 1,500 kutoka madhehebu na nyumba za ibada mbalimbali wameshiriki kwenye kongamano hilo la viongozi wa dini.

Kunenge alisema, mkoa na wilaya umejiwekea mikakati kuanzia vitongoji ,kata,wilaya na mkoa kutoa elimu ya umuhimu wa sensa kupitia njia mbalimbali ikiwemo mikutano na wananchi,bodaboda,wakufunzi,makarani,matamasha ,kwenye michezo na makongamano.

"Watendaji 143 nao wameudhuria mafunzo ili kupata uelewa wa kusimamia Zoezi la sensa". Pamoja na vikao viwili vya kamati ya sensa mkoa vimefanyika "alieleza Kunenge.

Kwa upande wake,Mwenyekiti mwenza wa kamati ya Usalama mkoa ambae pia ni Sheikh mkuu mkoa wa Pwani Hamis Mtupa sensa Ni takwa la kidini.

"Mafanikio pia ya kidunia ni kwasababu ya kujisensa mwenyewe kwahiyo sensa ni agizo na takwa la kidini ili kujua kesho yako."

Mtupa alieleza kuwa, viongozi wa dini wamelibeba Zoezi hili watahakikisha linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Nae Askofu Emmanuel Mhina alisema kuwa kamati hiyo ilianza kipindi kirefu kufanya maandalizi ya kongamano hilo na hadi sasa wanaona kuna mwelekeo mzuri.

"Tunaona kuna mafanikio makubwa hadi hapa tulipofikia mwitikio ni mkubwa hivyo tunaamini kuwa siku ya sensa wananchi watajitikeza kuhesabiwa"alisema Mhina.

Mchungaji wa Kanisa Anglikana Kibaha Mkoani Pwani Exavia Mpambichile aliwataka Waumini na wakazi wa Mkoa huo kuzingatia maagizo ya Serikali na kujitokeza wakati wa Sensa Ili kupatikana takwimu sahihi itakayofanikisha Serikali kupanga bajeti stahiki.

 


Majina ya Watanzania walioitwa Kwenye Usaili Wa Makarani, Wasimamizi Wa Maudhui Na Wasimamizi Wa Tehama Wa Kazi Za Sensa Ya Watu Na Makazi 2022 yameanza kutoka katika mikoa mbalimbali.

Hapo chini, tumeweka majina ya mikoa mbalimbali.

 

==>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA

 


Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amewataka Wananchi mkoani humo kutoa ushirikiano kwenye zoezi la Sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu.
Amesema wataandaa Nyama ya kutosha kwa ajili ya jamii ya wahadzabe wanaofanya shughuli za uwindaji ili zoezi la uhesabuji watu linapofanyika wawepo katika nyumba zao.
"Niwahakikishie Wahadzabe,zoezi la Sensa ya watu na tumewaandalia nayama ya kutosha" alisema Makongoro
Amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi katika maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi mkoani humo zilizofanyika mjini Babati.
Mbunge wa Jimbo la Babati mjini (Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Paulina Gekul, amesema Sensa ni Muhimu kwa maendeleo ya Taifa hivyo ni muhimu watu wote kushiriki kikamilifu.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza zoezi la Sensa ya watu na Makazi kufanyika Agosti 23,2022 ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Sensa kwa Maendeleo, Jiandae kuhesabiwa".
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), ipo kwenye maandalizi ya kufanya Sensa hiyo. Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012, hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.