Na Amani Mongi : MsumbaBlog

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewaagiza  viongozi wote katika ngazi za Wilaya,Halmashauri na wakuu wa idara mkoani Arusha kwenda kukagua maeneo yote yaliyopitiwa na zoezi la sensa ya watu na makazi ili kujiridhisha mwenendo mzima wa zoezi hilo kabla ya tarehe ya mwisho. 

Rc Mongella amebaini hayo baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya sensa ya watu na makazi katika Wilaya ya Longido  na kubaini amebaini uwepo wa baadhi ya maeneo yaliyokadiriwa kuwa na kaya yalikuwa chini au zaidi na kuwataka viongozi wa wilaya na halmashauri zote kuyabaini hayo maeneo na kuchukua hatua haraka ili kuhakikisha kaya hizo zinahesabiwa

"Lengo letu kuu sio tu kumaliza zoezi la sensa kwa muda uliopangwa bali kuhakikisha kila kaya inahesabiwa hivyyo niwaagize viongozi wa makarani kuhakikisha wale wanaomaliza kuhesabu katika maeneo yao mapema wapangiwe maeneo mengine ambayo yanauhitaji zaidi ili kaya zote ziweze kufikiwa" Rc Mongela

Kwa upande wake Karani kutoka Wilayani Longido Frida Chome amesema zoezi la sensa kwa upande wake limeenda vizuri. na amefanikiwa kuhesabu kaya 70 na akahamishiwa kwenye eneo jinqine

Frida ameendelea kueleza kuwa changamoto kubwa aliyokutana nayo ni baadhi ya watu kutowakuta kuenye kaya kwa sababu ya majukumu yao ya kikazi hivyo kupelekea kufanya zoezi la sensa kufanyika hadi  wakati wa usiku.

Hata Hivyo Samueli Steven ambaye ni miongoni mwa wananchi waliohesabiwa na amesema zoezi la sensa ya watu na makazi ni nzuri kwani litasaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo na huku akimshukuru Rais Samia  Suluhu Hassan kwa kuwezesha zoezi hilo kwa wakati.

RC Mongella anaendelea na zoezi la kufuatia mwenendo mzima wa sensa ya watu na makazi katka halmashauri zote za Mkoa wa Arusha na kutatua changamoto mbalimbali zinazokuwa zimejitokeza katika maeneo hayo.







Share To:

Post A Comment: