Articles by "SIASA"
Showing posts with label SIASA. Show all posts

 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) nchini Tanzania, Ndugu Xu Sujiang, huku akisisitiza dhamira ya CCM ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na wa kimkakati kati ya vyama hivyo viwili.









Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 20,2026 katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma, ambapo Ndugu Xu ametumia nafasi hiyo kuaga rasmi kabla ya kuhitimisha majukumu yake nchini Tanzania

 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri (MCC), leo Agosti 15, 2026, amekuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Hadhara wa Jimbo la Ubungo, ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.


Kabla ya kushiriki mkutano huo, Ndugu Mwanri alipokewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Sekretarieti ya CCM Mkoa, chini ya Katibu wa CCM Mkoa, Ndugu Mkandawire.

Aidha, alipokea taarifa fupi kuhusu utendaji wa Chama katika Mkoa huo na kuwashukuru viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa usimamizi mzuri wa Chama na Serikali.

Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Mwanri amesisitiza umuhimu wa Wabunge, Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara ili kuwapa wananchi mrejesho kuhusu utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na CCM wakati wa Uchaguzi.

Aidha, amewasihi wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.

Kwa upande wake, Prof. Kitila Mkumbo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya wananchi wa Jimbo la Ubungo, akieleza hatua zilizochukuliwa katika kuboresha miundombinu, hususan sekta ya barabara.

Prof. Kitila amesema ataendelea kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi na Serikali katika kuhakikisha wananchi wa Ubungo wanaendelea kupata huduma na maendeleo yanayostahili.

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE.

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amefungua rasmi Tawi la CCM Kibuteni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, leo tarehe 12 Agosti 2026.

Tawi hili lina historia kubwa tangu nyakati za ASP na TANU, na ni jambo la kujivunia kuona sasa lina sura mpya inayokwenda sambamba na mahitaji na hadhi ya Chama.

Dkt. Migiro amewahimiza viongozi na wanachama kuhakikisha Tawi hilo linakuwa kituo cha uhai wa Chama, mshikamano, mafunzo, vikao na utekelezaji wa shughuli za Chama.

Pia, Katibu Mkuu amewashukuru wana-CCM wa Kibuteni kwa mapokezi mazuri, upendo na zawadi.


 


Katibu wa NEC, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kitaifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Rabia Abdalla Hamid, leo Agosti 4, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Ndugu Garvey Pierre, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na uhusiano wa kimataifa.

 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akiongoza Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, wakati wa kuwapokea na kuwatambulisha wajumbe walioteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), hivi karibuni. Katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, leo Jumamosi, tarehe 1 Agosti 2026, pia Balozi Dkt. Migiro alishuhudia makabidhiano ya ofisi na majukumu kati ya viongozi wapya na wanaoondoka 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu Aggrey Mwanri akipokewa na kusalimiana kwa tabasamu na bashasha na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Ndugu John Mongella, leo Jumamosi, tarehe 1 Agosti 2026, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, walioteuliwa hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) akishuhudia makabidhiano ya ofisi na majukumu, kati ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Komredi Aggrey Mwanri (kushoto pichani) na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Komredi John Mongella (kulia pichani), yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, leo Jumamosi, tarehe 1 Agosti 2026.





 


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Akiongoza Kikao Maalum cha Halmashauri  Kuu ya CCM Taifa  kilichofanyika Zanzibar Jumatano tarehe 29 Julai, 2026.







Na Mwandishi Wetu, Tanga

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Muheza mkoani Tanga kimesema hakihusiki na vitendo vinavyodaiwa kufanywa na aliyekuwa Katibu wa chama hicho wilayani humo, Joseph Mwakidasi, huku kikiwataka wanachama kuendelea kudumisha mshikamano na kuepuka makundi yanayoweza kukigawa chama.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu wa CHADEMA Jimbo la Muheza, Michael Mhina, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio yaliyojitokeza ndani ya chama katika siku za hivi karibuni.

Mhina alisema Julai 8 mwaka huu viongozi wa chama waliona kupitia vyombo vya habari taarifa za Mwakidasi akimtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, kutumia vibaya fedha zinazochangwa na wanachama kupitia kampeni ya "Tone Tone".

Alisema kutokana na uzito wa tuhuma hizo, Kamati Tendaji ya Wilaya ilikutana kwa dharura Julai 9 na kumuita Mwakidasi ili afafanue chanzo cha madai yake, lakini hakufika wala wanachama wa CHADEMA. Alisema waliingia ofisini baada ya kuchukua funguo kutoka kwa m hayo, Julai 21 tuliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili vifanye uchunguzi kuhusu kilichotokea. Sisi kama CHADEMA Muheza hatuhusiki kwenye kikao hicho wala kutoa maelezo.

Mhina alidai kuwa Julai 20, Mwakidasi aliwasili katika ofisi za CHADEMA Wilaya ya Muheza akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi kutoka wilaya nyingine pamoja na watu ambao, kwa mujibu wa chama hicho, si viongozi wala wanachama wa CHADEMA. Alisema waliingia ofisini baada ya kuchukua funguo kutoka kwa mweka hazina wa chama.

Kwa mujibu wa Mhina, watu hao walifanya kikao ndani ya ofisi hizo na baadaye kurekodi na kusambaza taarifa mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, jambo alilodai lilisababisha taharuki miongoni mwa wanachama na wananchi wa Muheza.

"Baada ya matukio hayo, Julai 21 tuliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili vifanye uchunguzi kuhusu kilichotokea. Sisi kama CHADEMA Muheza hatuhusiki na yaliyofanywa na watu hao," alisema Mhina.

Alisema viongozi wa chama wilayani humo wanaendelea kumuunga mkono Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, pamoja na Mwenyekiti wa chama, Tundu Lissu.

Pia aliomba vyombo vya dola kuchunguza madai ya kuwahamasisha wananchi kuhudhuria mkutano kwa ahadi ya kulipwa fedha, akisisitiza kuwa CHADEMA haina utaratibu wa kuwalipa wanachama kushirikiio yote yaliyotokea katika ofisi za chama, akidai hatua zilizochukuliwa na Mwakidasi na wenzake zilichangia taharuki miongoni mwa wanachama na wananchi wa shughuli za chama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Muheza, Ally Mahanyu, alisema chama kinapinga vitendo vinavyodaiwa kufanywa na Mwakidasi kwa madai kuwa vilikiuka taratibu za chama.

Mahanyu alisema viongozi walimuita Mwakidasi mara kadhaa kwenye vikao vya Kamati Tendaji ili kutoa maelezo, lakini hakuitikia wito huo.

Aidha, alivitaka vyombo vya dola kuchunguza matukio yote yaliyotokea katika ofisi za chama, akidai hatua zilizochukuliwa na Mwakidasi na wenzake zilichangia taharuki miongoni mwa wanachama na wananchi wa Muheza.

Aliwataka wanachama wa CHADEMA kuendelea kuwa watulivu, kuwaamini viongozi wao na kushiriki shughuli za ujenzi wa chama kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Wilaya ya Muheza, Isa Mwaikani, alisema baraza hilo pia lilimuita Mwakidasi kutoa maelezo kuhusu tuhuma alizozielekeza kwa Heche, lakini hakuitikia wito huo.

Mwaikani alisema viongozi wa chama walishangazwa na tuhuma hizo kwa kuwa, kwa mujibu wa muundo wa uongozi wa chama, Makamu Mwenyekiti hahusiki na usimamizi wa fedha.

"Hatuelewi amepata wapi ujasiri wa kumtuhumu kiongozi wa juu wa chama bila kuwasilisha ushahidi kwenye vikao halali vya chama," alisema.

Aliongeza kuwa wanachama wengi wa CHADEMA Muheza wameendelea kubaki ndani ya chama na hali ya kisiasa wilayani humo ni tulivu.



Akijibu tuhuma hizo, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Muheza, Joseph Mwakidasi, alisema madai yanayotolewa dhidi yake hayana ukweli na kwamba anaendelea kutetea nafasi yake ndani ya chama.

Alisema hana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa na anasubiri maamuzi ya vikao vya chama kuhusu nafasi yake.

Kuhusu tuhuma alizomwelekeza John Heche, Mwakidasi alisema suala hilo linatokana na mijadala iliyofanyika katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichofanyika Dodoma, akidai baadhi ya taarifa zilizokuwa siri zilivuja kutoka ndani ya chama.

 

Viongozi wa Serikali wameshauriwa kuongeza Elimu ya utoaji na urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10, ambayo katika bajeti ya mwaka 2026/2027 itakuwa asilimia 15.

Hayo yameelezwa leo Julai 12,2026 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg Rabia Abdalla Hamid katika muendelezo wa ziara yake ya Kusikiliza na kutatua changamoto za Makundi mbalimbali ya kijamii mkoani Rukwa.

“Nitoe rai kwa Viongozi wa serikali kuhakikisha Elimu ya utoaji na urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10,ambayo katika bajeti ya mwaka 2026/2027 itakuwa asilimia 15 inatolewa kwa kasi  ili wananchi wawe na uelewa mpana katika masuala ya fedha na walengwa waendelee kunufaika ”,amesema Ndugu Rabia.