Articles by "HABARI"
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu-kazi, ajira na mahusiano, mhe. Deus sangu (kulia) akiteta jambo na waziri wa kazi nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mari, mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue’ kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, uliofanyika Oktoba 6, 2026, jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Husserin Ali Mwinyi (Wapili kushorto), akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Kazi wa nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mariri, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, akishuhudia wakati w aufunguzi wa mkutano wa pili wa majadiliano ya Doha (Doha Dialogue)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akisisitiza jambo  mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, Uliofanyika Oktoba 6, 2026, Jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza Kulia) akiwa na viongozi wenzake, katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialoguie’ Jijini Dar Es Salaaam, Oktoba 6, 2026

Dar es Salaam, Oktoba 6, 2026

Mkutano wa Pili wa mazungumzo ya Doha (Doha Dialogue) kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, umekamilika leo Oktoba 6, 2026 jijini dar es salaam na kuja na fursa mpya za ajira kwenye nchi za Ghuba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mwishoni mwa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema kama taifa tumepata fursa ya nchi za GCC+ kuja nchini ili kujadili na kutafakari uhamaji wa nguvu kazi kutoka Barani Afrika kwenda katika nchi za Ghuba (GCC+) 

“ Lakini pia tumeahidiwa ajira zaidi, kando na mkutano huu tuliendelea na mikutano mingine kuhusisha nchi mbalimbali za Ghuba kuona namna gani wanaweza kuongeza fursa za ajira hivyo katika mikutano hiyo tumepata fursa nyingi zitakazopelekea kusaini mikataba mingi ya ajira.” amesema Mhe. Sangu.

Mbali na ajira zisizo za ujuzi (Un skilled), sasa zimekuja fursa za ajira za kitaalamu (Skilled labour) wanahitaji vijana wengi madaktari, manesi, wafamasia, mafundi na mainjinia, kwahivyo wameona fursa ya nguvu kazi kutoka afrika lakini kipekee kutoka Tanzania. 

“Vijana wa Kitanzania waliopelekwa kwenye nchi hizo kufanya kazi wameonyesha uhodari katika kuchapa kazi na uaminifu,” amesisitiza.

Aidha, Mhe. Sangu amesema, katika mkutano huo nchi za Ghuba zimeuhakikishia mkutano huo uliowaleta pamoja wajumbe kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika na AU uzingatiaji wa mikataba waliyoingia (Bilateral Agreements)  ambayo mingi inazingatia haki na maslahi ya wafanyakazi hasa katika suala la hifadhi ya jamii.

“ Tumekubaliana kimsingi sasa, suala la hifandhi ya jamii ni kipaumbele katika mikataba yote tutakayoingia na nchi hizo, tumejadili kuhusu bima ya afya kwa wanaokwenda kufanya kazi na malipo ya mishahara,”Amesema Mhe. Sangu.

MWISHO

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa utoaji wa huduma za matibabu kwa wanachama wa NHIF, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma hizo za kibingwa nchini.

Makubaliano hayo yamesainiwa katika hafla iliyofanyika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene C. Isaka, kwa niaba ya Mfuko huo, pamoja na Mtendaji Mkuu wa Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Zeenat Sulaiman, aliyesaini kwa niaba ya Taasisi ya Aga Khan.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dkt. Isaka amesema ushirikiano huo ni sehemu ya jitihada za NHIF za kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanachama wake, hususan huduma za kibingwa zinazohitaji utaalamu na teknolojia maalumu.

Dkt.Isaka,amesema  NHIF inaendelea kupanua wigo na kuboresha ubora wa huduma zinazotolewa kwa wanachama wake, sambamba na kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma hizo kupitia mtandao wa watoa huduma wa Mfuko.

“NHIF inaendelea kuboresha wigo na ubora wa huduma zinazopatikana kwa wanachama wake na kuongeza wigo wa vituo vinavyotoa huduma hizo. Kusainiwa kwa makubaliano haya ni hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa za matibabu ya saratani kupitia mtandao wa watoa huduma wa Mfuko,” amesema  Dkt. Isaka.

Ameongeza kuwa makubaliano hayo yanaendeleza historia ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili na yamekuja wakati ambao Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, unaolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa usawa na kwa wakati.

NHIF imeeleza kuwa itaendelea kuimarisha ushirikiano na watoa huduma mbalimbali wa afya nchini kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wanachama wake, kuboresha ubora wa huduma na kuhakikisha matibabu yanatolewa kwa ufanisi kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki,Dkt. Zeenat Sulaiman amesema Hospitali ya Aga Khan inathamini ushirikiano huo na NHIF, akieleza kuwa makubaliano hayo yanaimarisha dhamira ya taasisi hizo mbili ya kushirikiana katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

“Ushirikiano huu unaonesha umuhimu wa taasisi za umma na binafsi kushirikiana katika kuimarisha huduma za afya. Tutaendelea kutumia utaalamu, teknolojia na uzoefu wetu katika kutoa huduma za kibingwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu,” amesema Dkt. Sulaiman.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, wanachama wa NHIF watanufaika na huduma za matibabu hususan Saratan katika Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam,Mwamza na kliniki 14 za hospitali hiyo.

Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza wigo wa vituo vinavyotoa huduma za matibabu yakiwemo ya saratani kwa wanachama wa NHIF, huku ikiwapa fursa ya kupata huduma za kibingwa kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu na kutumia teknolojia zinazohitajika katika matibabu ya ugonjwa huo.

lamu wenye uzoefu na kutumia teknolojia zinazohitajika katika matibabu ya ugonjwa huo.