
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu-kazi, ajira na mahusiano, mhe. Deus sangu (kulia) akiteta jambo na waziri wa kazi nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mari, mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue’ kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, uliofanyika Oktoba 6, 2026, jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Husserin Ali Mwinyi (Wapili kushorto), akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Kazi wa nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mariri, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, akishuhudia wakati w aufunguzi wa mkutano wa pili wa majadiliano ya Doha (Doha Dialogue)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akisisitiza jambo mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, Uliofanyika Oktoba 6, 2026, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza Kulia) akiwa na viongozi wenzake, katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialoguie’ Jijini Dar Es Salaaam, Oktoba 6, 2026
Dar es Salaam, Oktoba 6, 2026
Mkutano wa Pili wa mazungumzo ya Doha (Doha Dialogue) kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, umekamilika leo Oktoba 6, 2026 jijini dar es salaam na kuja na fursa mpya za ajira kwenye nchi za Ghuba.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mwishoni mwa mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema kama taifa tumepata fursa ya nchi za GCC+ kuja nchini ili kujadili na kutafakari uhamaji wa nguvu kazi kutoka Barani Afrika kwenda katika nchi za Ghuba (GCC+)
“ Lakini pia tumeahidiwa ajira zaidi, kando na mkutano huu tuliendelea na mikutano mingine kuhusisha nchi mbalimbali za Ghuba kuona namna gani wanaweza kuongeza fursa za ajira hivyo katika mikutano hiyo tumepata fursa nyingi zitakazopelekea kusaini mikataba mingi ya ajira.” amesema Mhe. Sangu.
Mbali na ajira zisizo za ujuzi (Un skilled), sasa zimekuja fursa za ajira za kitaalamu (Skilled labour) wanahitaji vijana wengi madaktari, manesi, wafamasia, mafundi na mainjinia, kwahivyo wameona fursa ya nguvu kazi kutoka afrika lakini kipekee kutoka Tanzania.
“Vijana wa Kitanzania waliopelekwa kwenye nchi hizo kufanya kazi wameonyesha uhodari katika kuchapa kazi na uaminifu,” amesisitiza.
Aidha, Mhe. Sangu amesema, katika mkutano huo nchi za Ghuba zimeuhakikishia mkutano huo uliowaleta pamoja wajumbe kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika na AU uzingatiaji wa mikataba waliyoingia (Bilateral Agreements) ambayo mingi inazingatia haki na maslahi ya wafanyakazi hasa katika suala la hifadhi ya jamii.
“ Tumekubaliana kimsingi sasa, suala la hifandhi ya jamii ni kipaumbele katika mikataba yote tutakayoingia na nchi hizo, tumejadili kuhusu bima ya afya kwa wanaokwenda kufanya kazi na malipo ya mishahara,”Amesema Mhe. Sangu.
MWISHO




Post A Comment: