
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu-kazi, ajira na mahusiano, mhe. Deus sangu (kulia) akiteta jambo na waziri wa kazi nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mari, mwishoni mwa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialogue’ kuhusu Uhamaji wa Wafanyakazi, uliofanyika Oktoba 6, 2026, jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Husserin Ali Mwinyi (Wapili kushorto), akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Kazi wa nchini Qatar, Mhe. Dkt. Ali Bin Samikh Ali Mariri, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, akishuhudia wakati w aufunguzi wa mkutano wa pili wa majadiliano ya Doha (Doha Dialogue)
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (Wakwanza Kulia) akiwa na viongozi wenzake, katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa ‘Doha Dialoguie’ Jijini Dar Es Salaaam, Oktoba 6, 2026
✅ Abainisha Makubaliano ya Mkutano huo katika kuimarisha Uhamaji wa Nguvu Kazi
Na: OWM (KAM), Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue II 2026 umefungua fursa zaidi za ajira kwa Watanzania na wananchi wa nchi nyingine za Afrika, kupitia kuimarishwa ushirikiano wa uhamaji wa nguvu kazi kati ya Afrika na nchi za Ghuba (GCC+).
Mhe. Sangu amesema hayo akizungumza na Waandishi wa Habari mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika leo Oktoba 6, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Amesema, kama taifa tumepata fursa ya nchi za GCC+ kuja nchini ili kujadili na kutafakari uhamaji wa nguvu kazi kutoka Barani Afrika kwenda katika nchi za Ghuba (GCC+).
“ Kupitia mkutano huu tumejadili na nchi mbalimbali za Ghuba kuona namna gani wanaweza kuongeza fursa za ajira ikiwemo za kitaalamu (Skilled labour) zinazohusisha madaktari, manesi, wafamasia, mafundi na mainjinia,”
Aidha, Mhe. Sangu amesema vijana wa Kitanzania waliopelekwa kwenye nchi hizo kufanya kazi wameonyesha uhodari katika kuchapa kazi na uaminifu.
Kadhalika, amesema katika mkutano huo nchi za Ghuba zimeihakikishia mkutano huo uliowaleta pamoja wajumbe kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika uzingatiaji wa mikataba waliyoingia (Bilateral Agreements) ambayo inazingatia haki na maslahi ya wafanyakazi hasa katika suala la hifadhi ya jamii.
“ Tumekubaliana kimsingi sasa, suala la hifandhi ya jamii ni kipaumbele katika mikataba yote tutakayoingia na nchi hizo, tumejadili kuhusu bima ya afya kwa wanaokwenda kufanya kazi na malipo ya mishahara,” amesema
MWISHO



Post A Comment: