Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amefungua rasmi Tawi la CCM Kibuteni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, leo tarehe 12 Agosti 2026.

Tawi hili lina historia kubwa tangu nyakati za ASP na TANU, na ni jambo la kujivunia kuona sasa lina sura mpya inayokwenda sambamba na mahitaji na hadhi ya Chama.

Dkt. Migiro amewahimiza viongozi na wanachama kuhakikisha Tawi hilo linakuwa kituo cha uhai wa Chama, mshikamano, mafunzo, vikao na utekelezaji wa shughuli za Chama.

Pia, Katibu Mkuu amewashukuru wana-CCM wa Kibuteni kwa mapokezi mazuri, upendo na zawadi.

Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: