Kariakoo, 7 Agosti, 2026
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kariakoo imeendelea kusogeza huduma karibu na walipa kodi kwa kukutana na wafanyabiashara wa maduka ya simu katika Kijiwe cha Zungu, Kariakoo, kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kutoa ufumbuzi wa masuala ya kodi na biashara.
Aidha, wafanyabiashara walipata fursa ya kueleza kwa uwazi changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku,ikiwa ni pamoja na ujio wa wageni(wachina) ambao wanauza bidhaa kwa bei rahisi Zaidi huku wakipata ufafanuzi, maelekezo na majibu ya papo kwa hapo kutoka kwa viongozi wa TRA kuhusu namna bora ya kuzitatua.
Hata ivyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafabiashara Bw. Severine Mushi amesema kuwa “Kukutana na TRA kunaondoa hofu na kunatupa nafasi ya kusikilizwa, kuongeza uelewa wa masuala ya kodi na kutujengea imani katika utekelezaji wa majukumu ya kikodi kwa ufanisi zaidi.”
Akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa TRA Mkoa wa Kariakoo Bw.Edson Issanya alisema mamlaka itaendelea kuwafikia walipa kodi katika maeneo yao ya biashara ili kutoa elimu, kusikiliza maoni yao, kutatua changamoto wanazokumbana nazo na kuendelea kuboresha huduma kwa lengo la kujenga mazingira wezeshi ya biashara.
















Post A Comment: