Na. Saidina Msangi, WF, Dar es Salaam.
Jukwaa hilo la siku mbili lililofunguliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, liliipatia Tanzania fursa ya kusaini hati tatu za makubaliano ikiwemo hati ya makubaliano ya kujenga kituo kipya cha huduma za usafishaji wa figo, mradi wa kuchakata gesi asilia kuwa gesi kimiminika na makubaliano kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Africa50 ya kuendeleza miundombinu ya usafirishaji wa umeme.
Aidha, Mikutano hiyo iliyokutanisha washiriki wapatao 1,200, imeipatia Tanzania fursa ya kutangaza vivutio vya utalii, uwekezaji na miradi ya kimkakati kwa lengo la kuvutia mitaji na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya miundombinu na hivyo kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Kitaifa wa Miaka Mitano (FYDP IV) na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
.jpg)
Post A Comment: