Articles by "JAMII"
Showing posts with label JAMII. Show all posts


Na Ashrack Miraji 

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Meneja wa Benki ya NMB tawi la Wilaya ya Same, Saad Masawila, ameongoza timu ya wafanyakazi wa benki hiyo kutembelea Gereza la Wilaya ya Same, ambapo walitoa msaada wa mahitaji muhimu kwa wafungwa na uongozi wa gereza hilo.


Ziara hiyo iliyofanyika mapema wiki hii ilikuwa ni sehemu ya juhudi za NMB kuonyesha mshikamano na kuunga mkono jamii, hasa makundi yenye uhitaji maalum. Mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na sabuni, dawa za meno, taulo, pamoja na vifaa vya usafi.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya makabidhiano, Masawila alisema kuwa benki ya NMB inatambua umuhimu wa huduma kwa jamii, siyo tu kwa wateja wao wa kila siku, bali pia kwa makundi yanayosahaulika kama wafungwa. Alisisitiza kuwa ni wajibu wa taasisi zote kuonyesha ubinadamu na kusaidia sehemu ambazo msaada unahitajika zaidi.


Wiki ya Huduma kwa Wateja huadhimishwa kila mwaka duniani kote na taasisi mbalimbali, ikiwa ni nafasi ya makampuni kuthibitisha dhamira yao kwa wateja na jamii kwa ujumla. NMB ikiwa ni miongoni mwa benki kubwa nchini, imekuwa mstari wa mbele kushiriki kwa vitendo katika kuleta maendeleo ya kijamii.

NA DENIS CHAMBI, TANGA

MAMLAKA ya vitambulisho vya Taifa ‘NIDA’ mkoa wa Tanga imezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho  kwa wananchi wapatao  165, 000  ambavyo vitakuwa vipatikana kupitia ofisi za kata na vitongoji ili kurahisisha upatikanaji kwa walengwa wote.

Akizindua zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Tanga  Waziri Kindamba amemwagiza meneja wa NIDA wa mkoa huo kuhakikisha ifikapo january 31 , 2024 wananchi wote ambao waliomba  wawe tayari wameshapata huku akiwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za wilaya pale ambapo itatokea mtu yoyote kudai pesa ili weze kupewa kitambulisho chake .
 
“Kwa mkoa wetu wa Tanga Mamlaka yetu ya NIDA imeweza kusajili wanannchi 1, 191, 488 sawa na asilimia 88,   namba za vitambulisho zilizo zalishwa ni  9, 50 ,392  sawa na asilimia  80 ya wakazi wote wenye umri wa miaka kuanzia 18 na vitambulisho vilivyopokelewa na kusambazwa ni 7,  96, 155 sawa na asilimia 83 ya wananchi wote waliokidhi vigezo  ni matumaini yangu kuwa wananchi wote kupitia wilaya zote mtajitokeza kupata vitambulisho vyenu,  jambo ambalo ni la kusisitiza  ni kwamba vitambulisho hivi vitagawiwa bure kama itatokea mtu yeyote atakudai fedha taarifa hizo zifike mara moja kwenye ofisi za wakuu wa wilaya na hatua kali zichukuliwe mara moja”  alisisitiza Kindamba.
Meneja wa Mamlaka ya vya vitambulisho vya Taifa NIDA  mkoa wa wa Tanga Kitashu Lembira alisema  kuwa  zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho ambalo limezinduliwa na mkuu wa mkoa  leo litafanyika  katika ngazi za wilaya ili kuwarahisishia na kuwawezesha wananchi wote waliokidhi kupata  akipongeza juhudi za serikali kwani  malalamiko ya wananchi kuhusu kukosekana kwa vitambulisho hivyo muda mrefu impshapatiwa ufumbuzi.
“Tumezindua mkoani lakini  kuazia  jumatatu ijayo vitambulisho vyote kuanzia ngazi za wilaya kata vijiji na vitongozi vitakuwa vimeshasambazwa na kutakuwa na majina yamebandikwa kwenye  mbao za matangazo ,  kikubwa ni kuipongeza na kuishukutu serikali hususan kwa awamu hii ya sita kwa mkoa wa Tanga  tunajivunia kwa sababu ni kipindi ambacho changamoto cha kukosekana kwa vitambulisho  inakwenda kuisha na kila mwenye namba ya kitambulisho cha taifa atapata kitambulisho chake” alisema Lembira
Kama alivyotuagiza mkuu wa mkoa kuwagawia vitambulisho ananchi wote wenye namba za NIDA ifikapo January 31, 2024  wananchi wote watapata na tutashusha mpaka ngazi vya vijiji na vitongoji  kikubwa tywaombe tu wananchi wawe watulivu kwa sababu tumeweka utaratibu mzuri kwa yule mwananchi ambaye atakqenda na atakosa ktambulisho chake atayoa taarifa kwa mtendaji wa kata ambaye naye atalazimika kufikisha katika ngazi ya wilaya ili kitambulisho kiweze kupatikana” aliongeza 
Wakizungumza baadhi ya wananchi waliopata vitambulisho vyao wakiwemo Waziri Omari na Mwanamisi Mbwana  wameishukuru na kuipongeza  serikali kwani kwa kuwapatia vitambulisho hivyo kumewasaidia kupata huduma mbalimbali ikiwemo za kifedha. 
“Naishukuru sana Serikali kwa kutupatia vitambulisho hivyi tulikuwa tunavisubiri kwa muda mrefu tumekuwa tukikosa baadhi ya huduma ,  kitambulisho cha Taifa  kinahusika maeneo mengi tumekuwa tukikosa huduma”
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba (kulia) akipokea vitambulisho kutoka kwa meneja wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA ‘ Mkoa wa Tanga Kitashu Lembira mara baada ya kuzalihswa na mamlaka hiyo tayari kwaajili ya kugaiwa kwa wananchi.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akikabidhi kitambulishi cha Taifa kwa mwananchi wa jiji la Tanga Waziri Omari mara baada ya kuzindua zoezi hilo leo January 17,2024 katika ofisi yake 

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akikabidhi kitambulishi cha Taifa kwa mwananchi wa jiji la Tanga Mwanahawa Mbwana mara baada ya kuzindua zoezi hilo leo January 17,2024 katika ofisi yake. 

NA DENIS CHAMBI, TANGA

MAMLAKA ya vitambulisho vya Taifa 'NIDA' mkoa wa Tanga imezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho  kwa wananchi wapatao  165, 000  ambavyo vitakuwa vipatikana kupitia ofisi za kata na vitongoji ili kurahisisha upatikanaji kwa walengwa wote.

Akizindua zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Tanga  Waziri Kindamba amemwagiza meneja wa NIDA wa mkoa huo kuhakikisha ifikapo january 31 , 2024 wananchi wote ambao waliomba  wawe tayari wameshapata huku akiwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za wilaya pale ambapo itatokea mtu yoyote kudai pesa ili weze kupewa kitambulisho chake .
 
"Kwa mkoa wetu wa Tanga Mamlaka yetu ya NIDA imeweza kusajili wanannchi 1, 191, 488 sawa na asilimia 88,   namba za vitambulisho zilizo zalishwa ni  9, 50 ,392  sawa na asilimia  80 ya wakazi wote wenye umri wa miaka kuanzia 18 na vitambulisho vilivyopokelewa na kusambazwa ni 7,  96, 155 sawa na asilimia 83 ya wananchi wote waliokidhi vigezo  ni matumaini yangu kuwa wananchi wote kupitia wilaya zote mtajitokeza kupata vitambulisho vyenu,  jambo ambalo ni la kusisitiza  ni kwamba vitambulisho hivi vitagawiwa bure kama itatokea mtu yeyote atakudai fedha taarifa hizo zifike mara moja kwenye ofisi za wakuu wa wilaya na hatua kali zichukuliwe mara moja"  alisisitiza Kindamba.

Meneja wa Mamlaka ya vya vitambulisho vya Taifa NIDA  mkoa wa wa Tanga Kitashu Lembira alisema  kuwa  zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho ambalo limezinduliwa na mkuu wa mkoa  leo litafanyika  katika ngazi za wilaya ili kuwarahisishia na kuwawezesha wananchi wote waliokidhi kupata  akipongeza juhudi za serikali kwani  malalamiko ya wananchi kuhusu kukosekana kwa vitambulisho hivyo muda mrefu impshapatiwa ufumbuzi.

"Tumezindua mkoani lakini  kuazia  jumatatu ijayo vitambulisho vyote kuanzia ngazi za wilaya kata vijiji na vitongozi vitakuwa vimeshasambazwa na kutakuwa na majina yamebandikwa kwenye  mbao za matangazo ,  kikubwa ni kuipongeza na kuishukutu serikali hususan kwa awamu hii ya sita kwa mkoa wa Tanga  tunajivunia kwa sababu ni kipindi ambacho changamoto cha kukosekana kwa vitambulisho  inakwenda kuisha na kila mwenye namba ya kitambulisho cha taifa atapata kitambulisho chake" alisema Lembira

Kama alivyotuagiza mkuu wa mkoa kuwagawia vitambulisho ananchi wote wenye namba za NIDA ifikapo January 31, 2024  wananchi wote watapata na tutashusha mpaka ngazi vya vijiji na vitongoji  kikubwa tywaombe tu wananchi wawe watulivu kwa sababu tumeweka utaratibu mzuri kwa yule mwananchi ambaye atakqenda na atakosa ktambulisho chake atayoa taarifa kwa mtendaji wa kata ambaye naye atalazimika kufikisha katika ngazi ya wilaya ili kitambulisho kiweze kupatikana" aliongeza 

Wakizungumza baadhi ya wananchi waliopata vitambulisho vyao wakiwemo Waziri Omari na Mwanamisi Mbwana  wameishukuru na kuipongeza  serikali kwani kwa kuwapatia vitambulisho hivyo kumewasaidia kupata huduma mbalimbali ikiwemo za kifedha. 

"Naishukuru sana Serikali kwa kutupatia vitambulisho hivyi tulikuwa tunavisubiri kwa muda mrefu tumekuwa tukikosa baadhi ya huduma ,  kitambulisho cha Taifa  kinahusika maeneo mengi tumekuwa tukikosa huduma"

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba (kulia) akipokea vitambulisho kutoka kwa meneja wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA ' Mkoa wa Tanga Kitashu Lembira mara baada ya kuzalihswa na mamlaka hiyo tayari kwaajili ya kugaiwa kwa wananchi.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akikabidhi kitambulishi cha Taifa kwa mwananchi wa jiji la Tanga Waziri Omari mara baada ya kuzindua zoezi hilo leo January 17,2024 katika ofisi yake 
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akikabidhi kitambulishi cha Taifa kwa mwananchi wa jiji la Tanga Mwanahawa Mbwana mara baada ya kuzindua zoezi hilo leo January 17,2024 katika ofisi yake. 





NA DENIS CHAMBI,  TANGA.

TAASISI ya Umoja wa  amani Kwanza  imempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha,   kusimamia na kuboresha misingi ya  amani kwa Taifa  ambayo imekuwa ni kielelezo kwa mataifa mbalimbali hususani ndani ya Africa.

Pongezi hizo wamezitoa leo December 16 mkoani Tanga katika  hafla iliyoambatana na kumpongeza rais wa taasisi hiyo Dkt  Wilson Munguza  kwa kutunukiwa cheo cha udaktari  na rais  wa amani kwanza Afrika Mashariki iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga katika hafla hiyo ,  Mkurugenzi wa Halmashauri jiji la Tanga  Said Majaliwa ameipongeza taasisi hiyo kwa jitihada inazozifanya kwa kuvisaidia vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kutekeleza na kusimamia majukumu yake ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa amani kwa Taifa  ambayo huchochoea maendeleo  kupitia nyanja mbalimbali.

Majaliwa amesema taasisi hiyo isiyokuwa ya kiserikali  itaendelea kupata ushirikiano wa hali na mali  kutoka serikalini katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia na kuilinda amani kwa Taifa ambayo imekuwa ikiwavutia wawekezaji katika maeneo mbalimbali  hapa Nchini.

Awali akizungumza  rais wa  Umoja wa amani kwanza Dkt Wilson Munguza amesema wataendelea kuwa msaada kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha amani inakuwepo  na katika kuhakikisha wanawafikia watanzania wote wana malengo ya kufika hadi ngazi ya kata ili kutoa elimu na kusisitiza uzalendo kwa Taifa.

Aidha Dkt. Munguza ameiomba Serikali kuwashika mkono katika kutimiza lengo lao la kujenga chuo cha amani katika wilaya ya Handeni mkoani  Tanga kinachotarajiwa kuchukua wanafunzi kutoka ndani na nje ya Afrika mashariki.

" Ombi la taasisi kwa serikali ya  mkoa  wa Tanga  tunaomba kuelekea  lengo letu la kujenga chuo cha Amani  katika wilaya ya Handeni tunaomba  kupelekewa Buldoza  litakalosaidia kusafisha eneo  ambalo tunatarajia kujenga chuo hicho ambacho kitachukua wanafunzi wa kutoka ndani ya Nchi za Afrika Mashariki" alisema Dkt Munguza .

Akitoa salamu za jeshi la polisi kwa niaba ya kamanda wa mkoa wa Tanga ,  mkuu wa kitengo cha  Polisi jamii kamshina  msaidizi wa Polis  ACP  Yohana Mjengi ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi wanazoendelea kuzifanya wakishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.

Aidha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuwa mabalozi wa amani katika kuwavumbua wahalifu sambamba na kuwataka madereva na wanatumia vyombo vya usafiri kuzingatia usalama barabarani ili kuepukana na matukio ya ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu na mali zao.

"Tumetika ofisini kwenda  mpaka kwenye vijiji vitongoji na hata mitaa kwaajili ya kuongeza ulinzi shirikishi niwapongeze sana umoja wa amani kwanza  kwa kutambua umuhimu wa amani  sisi Polisi na wao majukumu yetu yanafanana  tumekuwa tukishirikiana  nao mara kwa mara  katik kutoa elimu ya kuimarisha amani  maendeleo yeyote pasipo kuwa na amani  hayawezi kuja" alisema ACP Mjengi.

"Jeshi la Polisi linawataka wananchi wote kuimarisha ulinzi na usalama hasa katika kipindi  hiki kuelekea  mwisho wa mwaka  kuhakikisha tunakuwa mabalozi wa amani na kwa upande wa madwreva kuzingatia sheria za usalama barabarani ,  wananchi wachukue tahadhari za kiusalama  hasa tunapokuwa kwenye mikusanyiko" alisisitiza.

Taasisi hiyo ya Amani Kwanza  ambayo ilianzishwa mwaka 2018 ikiwa na wanachama 14  inaendelea kukua ambapo  sasa imeweza kufikisha zaidi ya wanachama 5, 000 ikiwa ipo katika mikoa yote ya Tanzania.


rais wa Umoja wa amani kwanza Tanzania Dkt Wilson Munguza  akizungumza katika hafla hiyo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Said Majaliwa akimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba katika hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika leo December 16,2023 katika Hotel ya Panoli jijini Tanga ikiwa imeandaliwa na Umoja wa Amin kwanza.
Mkuu wa kitengo cha Polis jamii mkoa wa Tanga ACP Yohana Mjengi akizungumza katika hafla hiyo ikiwa amemwakilisha kamanda wa Jeshi la Polis mkoa wa Tanga.




Na Denis Chambi, Tanga

HALMASHAURI ya jiji la Tanga imepongezwa na tume ya maadili ya viongozi wa Umma  kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo kwenye taarifa ya mkaguzi na mdhibiyi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG' ikitakiwa kuongeza usimamizi wa matumizi ya fedha pamoja na koboresha utendaji ili kuendelea kufanya vizuri.

Pongezi hizo zimetolewa leo November 2, 2023 na afisa maadili kutoka tume ya maadili nchini  Zanabu Kissoky akimwakilisha mkurugenzi wa tume ya maadili ya viongozi wa Umma  kwenye kikao cha  robo ya kwanza  cha baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji la Tanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kusema licha ya pongezi hizo ni lazima halmashauri iangalie na kujitathmini kupitia hoja zilizotolewa mwaka uliopita na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG'

"Nilikuwa najaribu kuangalia ripoti za ukaguzi kwa miaka mitano jiji la Tanga mnapata hati safi na  inayoridhisha niwapongeze kwa hilo lakini tunafahamu hoja  ndogo ndogo hazikosekani katika uwajibikaji tunaambiwa tujitathmini katika utendaji wetu ukiangalia kwa mwaka wa fedha uliopita hatukuweza kukusanya mapato kama ilivyokusudiwa yawezekana labda sababu ni ufuatiliaji umekuwa hafifu kwahiyo katika uwajibikaji sasa inatutaka tujitathmini" alisema Kissoky.

"Tuanze kuhuisha kanzi data zetu za halmashauri kuanzia ngazi ya kata tukishirikiana na viongozi kuhakikisha tuna kanzi data zote za biashara zilizopo kwahiyo katika kujitathmini tuboreshe na kubuni mbinu mbalimbali ambazo zitaweza kuboresha utendaji kazi wetu sote kwa pamoja kwa nafasi zetu" aliongeza

 Aidha amewataka watumishi wote  wa Umma kwa kushirikiana na viongozi kuendelea kutimiza majukumu yao kwa wakizingati sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza na kujiepusha na migogoro mahala pa kazi ambayo inakwenda kinyume na maadili.

"Watumishi wa Umma mnatakiwa kufwata na kuzingatia misingi ya maadili  yanayotakiwa kila mtu kwa nafasi yake uwajibikaji uanzie ndani yake tujiepushe na migongano ya kimaslahi mahala pa kazi lakini vitendo vyote vya uvunjifu wa maadili na sio tu mahala pa kazi bali hata tunapokuwa nje ya majukumu yetu maadili tunapaswa kuyazingati@amnapokuwa nje  ninyi ni serikali mnamwakilisha Rais  hivyo matendo yako shalti yawe yenye heshima na staha" alisema.

Akifunga baraza hilo mstahiki meya wa jiji la Tanga  Abdulrahaman Shillow amesema baraza  limemtaka mkurugenzi kutekeleza mamuzi mbalimbali yaliyotolewa na  baraza lililopita la madiwani yakiwemo yakumtaka kubomoa nyumba iliyopo katika mtaa wa Ikulu ambayo haipo kwenye  raman ya miapango miji.

"Tumeondoka na maadhimio ya kumwachia mkurugenzi wiki mbili ili atekeleze maamuzi ya baraza la madiwani ya kubomoa nyumba ya ikulu na maamuzi mbalimbali yaliyotolewa kwenye mabaraza ya kata  ikiwa ni pamoja na kujenga shule za gorofa,  lakini pia  tumeondoka na maadhimio ya kwenda kuweka taa kayika barabara za Ngamiani Kaskazini pamoja na kuwachia kazi ya kutafuta fedha kwaajili ya  stendi ya daladala ya Ngamiani kati" alisema Shillow.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya jiji la Tanga Abdulrahman  Shillow akiongoza mkutano wa robo ya kwanza wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo leo November 2,2023.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya jiji la Tanga wakiwa kwenye mkutano wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jiji hilo.



Baadhi ya wataalam na wakuu wa idara wa halmashauri ya jiji la Tanga wakifwatilia mkutano wa madiwani  wa  robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika leo.

 

 

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeshiriki na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa washiriki wa kongamano la Wanawake na Manunuzi ya Umma, linaloendelea jijini Tanga. 

Meneja waNSSF Rehema Chuma alikuwa miongoni mwa waliotoa mada katika kongamano hilo lililoanza tarehe 23 Agosti, 2023, amesema kupitia kongamano hilo NSSF imetoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ambayo imebeba kundi kubwa kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, bodaboda na wajasiriamali wengine wote ili waweze kujiunga na kuchangia katika Mfuko kwa maisha yao ya sasa na baadaye.

Lengo la kongamano hilo ni kueleza fursa za biashara zinazoambatana na mradi wa bomba la mafuta Afrika Mashariki (EACOP) hivyo mradi huo ni fursa kwa NSSF kupata wanachama wapya ambao watapata ajira za moja kwa moja na wale watakaonufaika na ajira za muda pamoja na wanufaika wengine kama vile mama lishe na bodaboda ambao wataweza kujiunga na kuchangia katika Mfuko.

Meneja huyo aliwahamasisha wanawake kuchangamkia fursa za mradi wa bomba la mafuta na pia amewataka kujiunga na kuchangia katika Mfuko ili waweze kujiwekea akiba yao ya sasa na baadaye.

Katika kongamano hilo, NSSF licha ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii pia itaeleza fursa mbalimbali zinazopatikana zikiwemo za nyumba na viwanja ambazo zinauzwa kwa bei nafuu
 
 
Mmoja wa washiriki wa kongamano la wanawake (Daraja Comference )lililofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera akipata elimu ya uifadhi wa jamii kutoka kwa meneja wa NSSF Rehema Chuma mara baada alipotembelea katika banda la mfuko huo.
Meneja wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Rehema Chuma(kushoto)  akiwa katika kongamano la Daraja Comference lililoandaliwa na mbunge wa mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge ,ambalo limewakutanisha wanawake zaidi ya 1000 wa mkoa wa Tanga kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi.
 Na DENIS CHAMBI, TANGA.

SERIKALI imewaagiza wakandarasi na wawekezaji wa kimataifa wanaoutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati hapa nchini kuhakikisha kuwa wanazingatia usawa wa kijinsia katika utoaji wa ajira kwenye shughuli mbalimbali  wanazozisimamia ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele cha wazawa wakiwemo wanawake na makundi maalum.

Rai hiyo imetolewa mkoani Tanga na waziri wa jinsia wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akimwakilisha waziri mkuu Kassim Majaliwa katika kufungua kongamano la wanawake na manunuzi lililoandaliwa na Mbunge wa  viti maalum mkoa wa Tanga Mhandishi Mwanaisha Ulenge ambapoa amesisitiza kuwa ni lazima ushiriki wa jamii katika utekelezaji wa miradi hiyo upewe kipaumbele. 
 
Aidha taasisi zote zinazotekeleza na kusimamia miradi ya kimkakati zihakikishe kuwa zinawasilisha taarifa za utekelezaji wa ushiriki wa watanzania katika ofisi ya waziri mkuu kupitia Baraza la  Taifa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ili kuiwezesha nchi kupata  na kupima thamani inayobaki kwenye uchumi wa nchi.

"Waziri mkuu anasisitiza kuwa wawekezaji  na wakandarasi wa maswala ya kimataifa wa maswala ya kiuchumi wahakikishe kuwa maswala ya kujengea ujuzi kwa watanzania uhaulishaji wa teknolojia na ushiriki wa jamii kwenye eneo la uwekezaji yanapewa kipaumbele na taasisi zote zinazotekeleza mradi wa kimkakati ziwasilishe taarifa katika ofisi ya waziri mkuu kupitia baraza la  Taifa la uwezeshaji ili kutuwezesha nchi kupima thamani ya  kutokana na ushiriki wa watanzania alisema  Gwajima

"Watanzania hususan wanawake wapewe kipaumbele katika ajira  na manunuzi ya umma katika miradi yote ya kimkakati inayotekelezwa nchini na  kwenye fursa za biashara kupitia ujuzi walio nao na bidhaa ili kukidhi viwango"

"Lakini pia waziri mkuu anasisitiza ufwatiliaji na tathmini kuhusu  ushirikishwaji wa watanzania katika miradi ya kimkakati uendeleee kufanyika ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki kuhusu changamoto zinazojiyltokeza mara kwa mara ili ushiriki wa watanzania uweze kuwa wenye tija na manufaa kwa ujumla na mimi nasema taarifa zote tutazifwatilia na miradi itekeleze uwiano wa kijinsia ili kutimiza adhima ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya uwezeshaji wanawake kiuchumi" alisisitiza Dkt. Gwajima.

Dkt Gwajima amabaye pia alizindua taasisi ya Ng'arisha Maisha  iliyoanzishwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mwanaisha Ulenge amewataka wanawake  kujiunga na kutumia vyema mabaraza ya uwezeshaji wanawake kiuchumi yaliyopo ili kuweza kuwasaidia katika maswala mbalimbali yanayowahusu ikiwemo ya kiuchumi huku akizitaka taasisi za kifedha kuendelea kuwewezesha mikopo wananchi ili kuweze kujikwamua kiuchumi .

Awali akizungumza mkurugenzi wa taasisi ya  Ngarisha maisha  Foundation Mhandisi  Mwanaisha Ulenge amesema kupitia taasisi hiyo isiyokuwa ya kiserikali wamedhamiria kuwainua wananchi hususan wanawake  katika kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta za kilimo uvuvi na biashara sambamba na kuunga mkono juhudi zote za serikali zinazolenga kuwaletea maendeleo wananchi.

"Taasisi ya Ng'arisha  Maisha foundation ni  ya kitaifa isiyokuwa ya kiserikali  inayolenga kuwainua wananchi kiuchumi hususan wanawake ,  taasisia imeleta mafunzo hayo kwa lengo la kuunga mkono jiyihada za serikali katika  kuwaleta watanzania maendeleo,  taasisi ya NMF imedhamiria  kuunga mkono jitihada za serikali katika kutatua changamoto za makundi maalum wakiwemo wanawake,  na kuhakikisha mipango ya serikali ya kimaendeleo inawafikia walengwa wakiwemo wanawake"

"Taasisi ya  Ng'arisha Maisha foundation 'NMF' itasisimamia ugawaji wa mbegu bora za Alizeti kwa wakulima hususan wanawake na kuwapelekea wananachi kuachana na kilimo cha asili badala yake kujiingiza kwenye kilimo cha kisasa,  na taasisi itaendelea kugawa mbegu bora kwa wananachi hususan wanawake, ni matumain yetu barabara ya Handeni kwenda Kibirashi wakulima wa zao la Alizeti wataweza kunufaika nayo".

"Pamoja na kuwezesha mbegu kwa wananch nimewezesha vijana kupata elimu katika vyuo vya kati pamoja na kuwezesha vifaa tiba kwa  watoto njiti. nipo kwenye mchakayo wa kuwezeaha miguu bandia 100 kwa  wahitaji, kuhusu uvuvi bado wanawake  walionufaika ni wachache sana,  taasisis yeyu itaweka mipango zaidi kuhakikisha wanawake wengi zaidi wananufaika tunaomba serikali iwezeshe vifaa ili wanawake waweze kunufaika na uchumi wa bluu".

Kwa upande wake waziri wa afya na mbunge wa  Jimbo la  Tanga Ummy Mwalimu amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mhandishi Mwanaisha Ulenge kwa kuja wazo la kuanzisha taasisi ya Ng'arisha Maisha foundation ambayo inakwenda kugusa Maisha ya wananchi moja kwa moja hususan wanawake katika nyanja mbalimbali.

"Tunashukuru sana mheshimiwa Ulenge kwa kuthubutu na tutaendelea kufanya kazi pamoja kwaajili ya manufaa ya wanawake wa mkoa wa Tanga hususan kupitia taasisi hii uliyoianzisha lakin Jambo la kusistiza ni kwamba  uchumi unaendana na afya bora kwahiyo pia tutazungumza  na maswala ya saratani hususan saratan ya kizazi, matiti tuweze kupata matibabu" alisema Ummy.
 
 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga na mkurugenzi wa taasisi ya Ng'arisha Maisha Foundation Mhandisi Mwanaisha Ulenge akizungumza katika kongamano la wanawake na manunuzi ya Umma(Daraja Comference )lililowakutanisha wanawake zaidi ya 1000 wa mkoa wa Tanga kujadii fursa mbalimbali ikiwemo za uchumi.




 

 


Na Elizabeth Joseph,Monduli.

Wakina mama zaidi ya 400 wilayani Monduli wameandamana huku wakiwa na fimbo mkononi kwa lengo la kupinga mmomonyoko wa maadili hasa katika jamii ya Kimaasai kufuatia kuwepo kwa tetesi za mama mtu mzima kuwa na uhusuano wa kimapenzi na vijana wadogo maarufu kama Nyangulo.

Akiongea na Mwandishi wa habari hii Katibu wa maandamano hayo Bi Judica Elibariki amesema kuwa wameandamana kwa lengo la kupinga vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya wanawake ikiwemo kuvaa mavazi yasiyo ya heshima.

"Kumekuwa na taarifa za mwanamke mmoja mtu mzima kujihusisha kimapenzi na Nyangulo mdogo sana lakini pia ipo taarifa ya mzee kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mkwe wake yaani mke wa kijana wake hadi wamezaa mtoto hii sio sawa ni laana katika Jamii yetu ya Kimaasai hivyo tunapinga vitendo hivi"alieleza Katibu huyo.

Aliongeza kuwa lengo la fimbo alizobeba ni kuwaadhibu wale wote watakaovunja sheria zilizowekwa na kabila hilo hasa kuhusu maadili ikiwa ni kuwachapa viboko.

Naye mmoja wa Wamama aliyeshiriki maandamano alitejitambulisha kwa jina la Mama Namnyaki alipongeza maandamano hayo ma kusema yanaleta heshima na nidhani pamoja na kuonya wale wote wenye tabia hizo.

Mama mwingine alitejitambulisha kwa jina la Mama Given alishauri maandamano hayo na kuchapa viboko viwe sheria kwa Wasichana na wanawake wote wanaovaa nguo fupi zinazoonesha viungo vya mwili wa pamoja suruali za kubana ili kuleta nidhani ya mavazi wilayani humo.



NA DENIS CHAMBI.

MKUU wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kuendelea kutoa anuani za makazi katika maeneo ambayo bado pamoja na kuweka vibao vinavyoelekeza  maeneo mabalimbali ikiwa ni maelekezo ya serikali katika kuhakisha huduma za kijamii zinaendelea kutolewa kwa urahisi kama ilivyokusudiwa.

Kindamba ametoa maagizo hayo leo wakati akifungua mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi ,  watendaji,  wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi maalum  wa mkoa na halmashauri ya jiji la Tanga ambapo amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya wananchi wakieleza kuwa bado hawajapata anuani za makazi na vibao vilivyokuwa vimewekwa viking'olewa.

"Kumekuwa na changamoto katika utekelezaji wa anuani za makazi na wapo ambao  wamesema bado hawajapatiwa  anuani zao,  wengine wakisema kuwa vibao vimeng'olewa hivyo niagize kuendelea kuweka vibao kwa maana ya alama ambazo zinatambulisha mitaa yao kama mnavyofahamh hili ni zoezi endelevu kwahiyo uongozi wa  halmashauri na majiji yetu ni lazima kyhakikisha zoezi hili linaendelea kwa kasi ili kutambulika na kufikika kirahisi"

"Tuachane  na mazoea ya kizamani maendeleo ya teknolojia  yameongezeka  na yamekuwa yakibadilika badilika sana kwahiyo ni lazima tukubaliane hatuweze kwenda kwa namna hiyo." alisema Kindamba.

Alisema kwa mujibu wa matokeo  ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi ya watu mkoani Tanga imeongezeka  kutoka 2, 45,  205 kwa mwaka 2012 na sasa imefikia 2, 615, 557 kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la watu 570 ,392.

"Kwa kujibu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022  idadi ya watu mkoani Tanga  imeongezeka kutoka  milion mbili elfu atobaini na tano  mia mbili na tano kwa mwaka 2012 hafi kufikia milion mbili laki sita elfu kumi na tano mia tano hamsini na saba sawa na ongezeko la watu laki tano elfu sabini mia tatu tisini na mbili kwa mwaka 2022" alisema Kindamba

Awali akizungumza  meneja takwimu wa mkoa wa Tanga  Tonny Manjota amesema kuwa hadi sasa  ripoti kumi zimekamilishwa  kulingana na makundi mbalimbali  kwa kuonyesha matokeo ya sensa  ya mwaka 2022 ambayo yatasaidia wataalam katika mpango wa  maendeleo ya Taifa.

Alisema sensa ya watu na makazi iliyofanyika kitaifa mwaka 2022 ambayo ni ya 6 hapa nchini imekuwa  ya tofauti na zilizopita ikiwa imeanza na uhamasishaji pamoja na uyoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu ambapo kumekuwa na mayokeo chanya mpaka mwisho wa zoezi hilo.

Kulingana na sensa ya mwaka  ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 matokeo yameonyesha kuwa watoto  tegemezi chini ya miaka 15 kitaifa imekuwa ikipungua kutoka 42.3 hadi 40.8 na mkoa wenye watoto wachache ni Dar es salam.
 
  Meneja takwimu wa mkoa wa Tanga  Tonny Manjota akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Legal Naivera Augost 16,2023.

Baadhi ya viongozi ,  watendaji,  wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi maalum  wa mkoa na halmashauri ya jiji la Tanga wakiwa katika mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yaliyofanyika Augost 16,2023 kwenye ukumbi wa Legal Naivera.


 


NA DENIS CHAMBI, TANGA.

ASILIMIA 60 ya ukatili wa kijinsia  kwa watoto hapa nchini umebainishwa kutekelezwa ndani ya familia na ndugu wa karibu wakiwemo wazazi huku asilimia 40  ukifanywa nje hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na  serikali kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto UNICEF.


Hayo yameelezwa na naibu katibu mkuu kutoka wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Amon Mpanju wakati akifungua semina kwa viongozi wa dini kanda ya kaskazini mkoani Tanga  kuhusu muongozo wa malezi kwa wazazi na malezi ya watoto kwa mwaka 2023 ambapo amesema kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuwaelekeza wazazi,  kukemea na kupunguza  migogoro mbalimbali inayotokana na ndoa ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia ukatili ndani ya familiya kwa watoto. 

"Ongezeko la mmomonyoko wa maadili imeathiri sana watoto na kwa mujibu wa  utafiti uliyofanywa  na serikali pamoja na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto la UNICEF ulionyesha kuwa ongezeko kubwa  la vitendo vya ukatili majumbani  60% hufanywa na watu wa karibu wakiwemo wazazi , 40% ni nje ya nyumba  zetu na utafiti huu ulionyesha  wanaofanya vitendo vya ukatili  ni ndugu na jamaa ndani ya familiya"

"Serikali baada ya kuona tunayo changamoto hiyo ya mmomonyoko wa maadili,  malezi kwa watoto migogoro ya ndoa mapenzi ya jinsia moja  na sio sehemu ya  sheria zetu za nchi wala mila na desturi zetu hazitambui ndio tukasema kwa kushirikiana na wadau tutengeneze muongozo wa kitaifa  wa malezi kwa wajibu wa wazazi na walezi kwa malezi ya watoto na  familiya  kwa mwaka huu wa 2023  tukasema viongozi wetu wa dini muweze kutusaidia tuungane kuweza  kupeleka elimu sahihi  na kukumbushana wajibu  wa wazazi na walezi kwa watoto na familiya" alisema Mpanju.

Alisema kuwa muongozo huo umesimamia katika kuwaelekeza wazazi na walezi kuwajali watoto kuhakikisha wanapata mahitaji yote ya msingi  yanayolenga kumkuza na kumwendeleza mtoto  katika nyanja zote za kielimu kimalezi mpaka atakapofikia utimilifu wake wa kiakili pamoja na kumlinda dhidi ya ukatili wa kijinsia kuanzia majumbani ,  mashuleni na katika mazingira yoyote yanayomzunguka.

Mkurugenzi anayesimamia maswala  ya watoto kutoka  wizara ya maendeleo ya jamii  jinsia wanawake na makundi maalum ,  Sebastian Kitiku alielsza kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazochangia mmomomyoko wa maadili kwa watoto hapa nchini ikiwemo mogogoro ya ndoa  baina ya wazazi,  muingiliano wa  mila tamaduni na desturi za kigeni  pamoja na maendeleo ya teknolojia.

"Bado kuna changamoto mbalimbali katika malezi ya watoto hasa ambazo wizara imezibaini ikichangiwa na migogoro ya ndoa baina ya wazazi ,  muingiliano wa mila na desturi za kigeni maendeleo ya teknolojia  kuwapa uhuru sana  watoto ,  wazazi wengi kuwakabidhi watoto kwa watu wengine wawalelee hizi ni miongoni mwa sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa  kukosekana kwa malezi bora kwa mtoto" alisema Kitiku.

Viongozi wa dini wamefurahishwa na ujio wa mwongozo huo wa kitaifa juu ya malezi ya watoto ambapo licha ya jitihada mbalimbali zinazoendelea kutumika ikiwemo majukwaa ya kidini inaonekana kuleta mabadiliko ya kizazi cha baadaye kama tu mwongozo huo utatekelezwa kikamilifu.

Juma Ruhuchu ambaye ni Sheikh mkuu wa mkoa wa Tanga alisema " Wito wangu kwa wazazi na walezi ni kwamba wajitahidi katika maswala mazima ya malezi kwa watoto kwa sababu malezi mazuri kwa mtoto yatakuja kutufanya tupate taifa zuri la watu wazima wa baadaye hivyo tuwalee katika maadili ya kidini na ya kitanzania"

Padre Moris Mwambashi wa kanisa katoliki jimbo la Tanga alisema " katika semina hii ambayo inatoa muamko kwa wazazi na walezi katika sehemu zote zile wawe macho kuhakikisha watoto hawaingii katika wimbi la kurubuniwa na maswala ya utandawazi"

Mkurugenzi anayesimamia maswala  ya watoto kutoka  wizara ya maendeleo ya jamii  jinsia wanawake na makundi maalum ,  Sebastian Kitiku akizungumza katika semina ya viongozi wa dini kanda ya kaskazini kuhusu muongozo wa malezi kwa wazazi na malezi ya watoto kwa mwaka 2023 uliofanyika jijini Tanga july 32,2023,

Baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali wakifwatilia semina inayohusu muongozo wa malezi kwa wazazi na malezi ya watoto kwa mwaka 2023 inayofanyika mkoani Tanga kwa siki 4

Sheikh mkuu wa mkoa wa Tanga Juma Ruuchu akizungumzia kuhusu muongozo wa kitaifa wa malezi ya mazi na mlezi kwa watoto wa mwaka 2023.
Padre Moris Mwambashi wa kanisa katoliki jimbo la Tanga akizungumzia kuhusu muongozo wa kitaifa wa malezi ya mazi na mlezi kwa watoto wa mwaka 2023.






  

NA DENIS CHAMBI, TANGA. 
JUMLA ya Kaya 229 kutoka Vijiji mbalimbali wilayani Mkinga Mkoani Tanga zimepatiwa Msaada wa Chakula kupitia Shirika la World Vision ikiwa ni sehemu ya Kukabiliana na Uhaba wa Chakula kwenye baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na ukame kwa miaka miwili mfululizo. 


Baadhi ya wananchi wilayani humo wamekuwa wakikabiliwa  na  tatizo la Uhaba wa Chakula kwa kipindi cha Miaka miwili mfululizo hali inayopelekea kupata Lishe ndogo kutokana na watoto wao kula Mlo mmoja Kwa siku badala ya milo mitatu

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada huo wa Chakula Wananchi wa Vijiji zaidi ya 8 wikayani humo wamesema wamekuwa wakikabiliwa  na Uhaba wa Chakula kwa kipindi cha Miaka miwili sasa jambo linalopelekea afya zao kudumaa na hatimaye watoto kushindwa kufanya vizuri pindi wawapo mashuleni. 

"Watoto wetu wanatakiwa wale kutwa mara tatu lakini wakwetu kutwa wanakula mara moja tuu hii ni changamoto kubwa sana inayotukabili sisi wazazi tunanyongeka sanaa, "alisema mmoja wa wananchi hao. 

Baadhi ya wananchi wengine wamesema wanasumbuliwa na Upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo katika Vijiji vyao ambapo wameliomba Shirika la World Vision kuwawezesha Vikundi vya Ulemavu ili waweze pia kupatiwa Msaada wa Pembejeo

"Tuishukuru World Vision kwa hiki walichotuletea leo tunaomba watutembelee pindi wanapokwenda kwenye miradi yao sisi walemavu tuna vikundi vyetu vya walemavu waje wavione waone nini kinatukwamisha hususani kwenye pembejeo za kilimo maana walemavu sisi hatuoni wengine wamekatwa miguu lakini watoto tulionao ndio wanatusaidia, "alisema Mmoja wa walemavu hao. 

Kwa Upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Maforoni wilayani Mkinga Albertina Makungu amesema Katika mwaka wa 2021 na mwaka 2022 walipatwa na Changamoto ya Ukame katika maeneo ya wilaya ya Mkinga, ambapo amelishukuru Shirika hilo kwa kutoa Msaada kwa watu wenye Uhitataji wa Chakula

"Kweli tuna janga la njaa tunakula kwa shida tunashukuru zaidi kwa msaada huu tumekuwa na janga la njaa kwa muda mrefu sasa kaya hizi na familia hizi zimepata shida ya chakula kwa miaka miwili mfululizo, "alisema Makungu. 

Meneja wa Mradi wa World Vision katika Wilaya ya Mkinga Evodia Chija amesema Shirika hilo kupitia Viongozi wao limeamua kuwagusa waathirika wa Janga la Njaa kutokana na ukame katika baadhi ya maeneo, ambapo wameweza kuwachangia Maharage na mahindi kilo 2000

Amesema lengo la kutoa msaada kwa makundi ya wenye Ulemavu na watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu ni ili na wao waishi kwa furaha kwa kupata tumaini kwenye maeneo yao kama watu wengine.

"Wafanyakazi wa World vision kwa ushirikiano wao na upendo wao tuliweza kukusanya kiasi cha shilingi milioni 7.5 ambazo kwa furaha kubwa viongozi wetu wakazielekeza zile fedha zilizopatikana zije kusaidia watoto wenye uhitaji katika eneo la mradi wa Mkinga, "alisisitiza Chija. 

"Tumetoa msaada wa Maharage,  unga kilo 2000 wenye virutubishi kwenye kaya hizi lakini kati ya kaya hizo Kaya 30 ni za watu wenye ulemavu,  watoto ambao ni wasajiliwa kwenye miradi ya World Vision wako kaya 136,"alibainisha Chija. 
Meneja wa Mradi wa World Vision katika Wilaya ya Mkinga Evodia Chija akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa msaada huo.
Badhi ya kaya zilizonufaika na msaada wa chakula kutoka World Vision