Na Elizabeth Joseph,Monduli.

Wakina mama zaidi ya 400 wilayani Monduli wameandamana huku wakiwa na fimbo mkononi kwa lengo la kupinga mmomonyoko wa maadili hasa katika jamii ya Kimaasai kufuatia kuwepo kwa tetesi za mama mtu mzima kuwa na uhusuano wa kimapenzi na vijana wadogo maarufu kama Nyangulo.

Akiongea na Mwandishi wa habari hii Katibu wa maandamano hayo Bi Judica Elibariki amesema kuwa wameandamana kwa lengo la kupinga vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya wanawake ikiwemo kuvaa mavazi yasiyo ya heshima.

"Kumekuwa na taarifa za mwanamke mmoja mtu mzima kujihusisha kimapenzi na Nyangulo mdogo sana lakini pia ipo taarifa ya mzee kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mkwe wake yaani mke wa kijana wake hadi wamezaa mtoto hii sio sawa ni laana katika Jamii yetu ya Kimaasai hivyo tunapinga vitendo hivi"alieleza Katibu huyo.

Aliongeza kuwa lengo la fimbo alizobeba ni kuwaadhibu wale wote watakaovunja sheria zilizowekwa na kabila hilo hasa kuhusu maadili ikiwa ni kuwachapa viboko.

Naye mmoja wa Wamama aliyeshiriki maandamano alitejitambulisha kwa jina la Mama Namnyaki alipongeza maandamano hayo ma kusema yanaleta heshima na nidhani pamoja na kuonya wale wote wenye tabia hizo.

Mama mwingine alitejitambulisha kwa jina la Mama Given alishauri maandamano hayo na kuchapa viboko viwe sheria kwa Wasichana na wanawake wote wanaovaa nguo fupi zinazoonesha viungo vya mwili wa pamoja suruali za kubana ili kuleta nidhani ya mavazi wilayani humo.



Share To:

Post A Comment: