Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha nne  katika shule ya sekondari Ketumbeine, wilayani Longido Mkoani Arusha wanadaiwa kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao kutokana na adhabu kali ya viboko walipoewa na walimu wa shule hiyo kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Wakisimulia mkasi hao baadhi ya Wazazi hao wamesema Watoto wao walilazwa sakafuni kwa muda wa siku mbili katika ofisi ya walimu, wakilazimishwa kukiri kuwa wanatumia madawaya kulevya aina ya bangi Pamoja na kula mandazi nje ya shule.

Licha ya adhabu hiyo iliyowasabishia majeraha na maumivu katika maeneo ya mgongoni na mbavuni,  baadhi ya wanafunzi hao wamesimamishwa shule wakisubiria maamuzi ya bodi ya shule.


Hata hivyo mmoja wa wazazi hao amesema ameshindwa kumpeleka mwanae hospitali licha ya majeraha aliyoyapata, kutokana na hali ya umasikini inayomkabili huku akiiomba serikali kuangalia upya adhabu walimu wanazozitoa kwa wanafunzi.

Uongozi wa shule ya sekondari Ketumbeine licha ya kukiri kuwasimamisha baadhi ya wanafunzi kutokana na utovu wa nidhamu, lakini hawajaweka wazi kama wanafunzi hao walipewa adhabu kali.


Mkuu wa wilaya ya Longido Marko Henry Ng'umbi, Pamoja na mkurugenzi wa Halmshauri ya Longido Steven Ulaya wamesema wanafuatilia kiundani taarifa za tukio hilo la wanafunzi kufanyiwa ukatili, kabla ya kutoa taarifa rasmi juu ya hatua zipi zitachukuliwa.

Share To:

Post A Comment: