Na Denis Chambi, Tanga

HALMASHAURI ya jiji la Tanga imepongezwa na tume ya maadili ya viongozi wa Umma  kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo kwenye taarifa ya mkaguzi na mdhibiyi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG' ikitakiwa kuongeza usimamizi wa matumizi ya fedha pamoja na koboresha utendaji ili kuendelea kufanya vizuri.

Pongezi hizo zimetolewa leo November 2, 2023 na afisa maadili kutoka tume ya maadili nchini  Zanabu Kissoky akimwakilisha mkurugenzi wa tume ya maadili ya viongozi wa Umma  kwenye kikao cha  robo ya kwanza  cha baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji la Tanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kusema licha ya pongezi hizo ni lazima halmashauri iangalie na kujitathmini kupitia hoja zilizotolewa mwaka uliopita na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali 'CAG'

"Nilikuwa najaribu kuangalia ripoti za ukaguzi kwa miaka mitano jiji la Tanga mnapata hati safi na  inayoridhisha niwapongeze kwa hilo lakini tunafahamu hoja  ndogo ndogo hazikosekani katika uwajibikaji tunaambiwa tujitathmini katika utendaji wetu ukiangalia kwa mwaka wa fedha uliopita hatukuweza kukusanya mapato kama ilivyokusudiwa yawezekana labda sababu ni ufuatiliaji umekuwa hafifu kwahiyo katika uwajibikaji sasa inatutaka tujitathmini" alisema Kissoky.

"Tuanze kuhuisha kanzi data zetu za halmashauri kuanzia ngazi ya kata tukishirikiana na viongozi kuhakikisha tuna kanzi data zote za biashara zilizopo kwahiyo katika kujitathmini tuboreshe na kubuni mbinu mbalimbali ambazo zitaweza kuboresha utendaji kazi wetu sote kwa pamoja kwa nafasi zetu" aliongeza

 Aidha amewataka watumishi wote  wa Umma kwa kushirikiana na viongozi kuendelea kutimiza majukumu yao kwa wakizingati sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza na kujiepusha na migogoro mahala pa kazi ambayo inakwenda kinyume na maadili.

"Watumishi wa Umma mnatakiwa kufwata na kuzingatia misingi ya maadili  yanayotakiwa kila mtu kwa nafasi yake uwajibikaji uanzie ndani yake tujiepushe na migongano ya kimaslahi mahala pa kazi lakini vitendo vyote vya uvunjifu wa maadili na sio tu mahala pa kazi bali hata tunapokuwa nje ya majukumu yetu maadili tunapaswa kuyazingati@amnapokuwa nje  ninyi ni serikali mnamwakilisha Rais  hivyo matendo yako shalti yawe yenye heshima na staha" alisema.

Akifunga baraza hilo mstahiki meya wa jiji la Tanga  Abdulrahaman Shillow amesema baraza  limemtaka mkurugenzi kutekeleza mamuzi mbalimbali yaliyotolewa na  baraza lililopita la madiwani yakiwemo yakumtaka kubomoa nyumba iliyopo katika mtaa wa Ikulu ambayo haipo kwenye  raman ya miapango miji.

"Tumeondoka na maadhimio ya kumwachia mkurugenzi wiki mbili ili atekeleze maamuzi ya baraza la madiwani ya kubomoa nyumba ya ikulu na maamuzi mbalimbali yaliyotolewa kwenye mabaraza ya kata  ikiwa ni pamoja na kujenga shule za gorofa,  lakini pia  tumeondoka na maadhimio ya kwenda kuweka taa kayika barabara za Ngamiani Kaskazini pamoja na kuwachia kazi ya kutafuta fedha kwaajili ya  stendi ya daladala ya Ngamiani kati" alisema Shillow.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya jiji la Tanga Abdulrahman  Shillow akiongoza mkutano wa robo ya kwanza wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo leo November 2,2023.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya jiji la Tanga wakiwa kwenye mkutano wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jiji hilo.



Baadhi ya wataalam na wakuu wa idara wa halmashauri ya jiji la Tanga wakifwatilia mkutano wa madiwani  wa  robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika leo.
Share To:

Post A Comment: