NA DENIS CHAMBI.

MKUU wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kuendelea kutoa anuani za makazi katika maeneo ambayo bado pamoja na kuweka vibao vinavyoelekeza  maeneo mabalimbali ikiwa ni maelekezo ya serikali katika kuhakisha huduma za kijamii zinaendelea kutolewa kwa urahisi kama ilivyokusudiwa.

Kindamba ametoa maagizo hayo leo wakati akifungua mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi ,  watendaji,  wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi maalum  wa mkoa na halmashauri ya jiji la Tanga ambapo amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya wananchi wakieleza kuwa bado hawajapata anuani za makazi na vibao vilivyokuwa vimewekwa viking'olewa.

"Kumekuwa na changamoto katika utekelezaji wa anuani za makazi na wapo ambao  wamesema bado hawajapatiwa  anuani zao,  wengine wakisema kuwa vibao vimeng'olewa hivyo niagize kuendelea kuweka vibao kwa maana ya alama ambazo zinatambulisha mitaa yao kama mnavyofahamh hili ni zoezi endelevu kwahiyo uongozi wa  halmashauri na majiji yetu ni lazima kyhakikisha zoezi hili linaendelea kwa kasi ili kutambulika na kufikika kirahisi"

"Tuachane  na mazoea ya kizamani maendeleo ya teknolojia  yameongezeka  na yamekuwa yakibadilika badilika sana kwahiyo ni lazima tukubaliane hatuweze kwenda kwa namna hiyo." alisema Kindamba.

Alisema kwa mujibu wa matokeo  ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi ya watu mkoani Tanga imeongezeka  kutoka 2, 45,  205 kwa mwaka 2012 na sasa imefikia 2, 615, 557 kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la watu 570 ,392.

"Kwa kujibu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022  idadi ya watu mkoani Tanga  imeongezeka kutoka  milion mbili elfu atobaini na tano  mia mbili na tano kwa mwaka 2012 hafi kufikia milion mbili laki sita elfu kumi na tano mia tano hamsini na saba sawa na ongezeko la watu laki tano elfu sabini mia tatu tisini na mbili kwa mwaka 2022" alisema Kindamba

Awali akizungumza  meneja takwimu wa mkoa wa Tanga  Tonny Manjota amesema kuwa hadi sasa  ripoti kumi zimekamilishwa  kulingana na makundi mbalimbali  kwa kuonyesha matokeo ya sensa  ya mwaka 2022 ambayo yatasaidia wataalam katika mpango wa  maendeleo ya Taifa.

Alisema sensa ya watu na makazi iliyofanyika kitaifa mwaka 2022 ambayo ni ya 6 hapa nchini imekuwa  ya tofauti na zilizopita ikiwa imeanza na uhamasishaji pamoja na uyoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu ambapo kumekuwa na mayokeo chanya mpaka mwisho wa zoezi hilo.

Kulingana na sensa ya mwaka  ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 matokeo yameonyesha kuwa watoto  tegemezi chini ya miaka 15 kitaifa imekuwa ikipungua kutoka 42.3 hadi 40.8 na mkoa wenye watoto wachache ni Dar es salam.
 
  Meneja takwimu wa mkoa wa Tanga  Tonny Manjota akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Legal Naivera Augost 16,2023.

Baadhi ya viongozi ,  watendaji,  wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi maalum  wa mkoa na halmashauri ya jiji la Tanga wakiwa katika mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yaliyofanyika Augost 16,2023 kwenye ukumbi wa Legal Naivera.


Share To:

Post A Comment: