NA DENİS CHAMBİ.
JESHİ
la Polisi mkoa wa Tanga limefanikiwa kumkamata Swalehe Miraji Ally
mwenye umri wa miaka 38 kwa kosa la kuwaua mke wake pamoja na shemeji
yake kwa kuwakata na mapanga mara mbili kichwani wakati wakiwa shambani
kisha kukimbilia mkoani Tabora.
Akitoa
taarifa hiyo leo Augost 17 kwa waandishi wa habari kamanda wa jeshi la
Polisi mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi amesema kuwa mtuhumiwa
huyo ambaye ni fundi ujenzi mkazi wa Mkanyageni wilayani Muheza
alimuua mkewe Mwanahawa Hassan (24) na Sauda Sufian (20) kisha
kukimbilia Tabora lakini jitihada za Polisi zilifanikiwa na kumkamata
mtuhumiwa kwaajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha
jeshi hilo wilayani Handeni limefanikiwa kumkamata Rajab Athuman
mwenye miaka 32 kwa kosa la kumuua kwa kumkata kichwa Helena Sila
ambapo bado upelelezi unaendelea kufwatia tukio hilo.
Katika
taarifa nyingine kamanda Mchunguzi amesema kuwa jeshi hilo limefanikiwa
kuwatia hatiani watu watano kwa makosa mbalimbali ambapo Ally Kilulu
amehukumiwa miaka 15 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya
aina ya Heroin gram 1, Amos Hamis akihukumiwa miaka 14 jela kwa kosa
la kubaka huku Halid Yusufu akihukumiwa miaka mitano jela kwa
kosa la wizi wa mifugo.
Wengine
ni Bakari Mohammed ambaye amehukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la
kuvunja duka usiku na kuiba huku Ernest Petro akihukumiwa kifungo cha
miaka 20 jela kwa makosa ya kuzini na Maharimu (ndugu yake) .
Hata
hivyo kamanda Mchunguzi amewataka wananchi mkoani wa Tanga kuendelea
kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapoona
viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao ili sheria kali dhidi
ya wahalifu na uhalifu ziweze kuchukuliwa.
"Jeshi
la Polis linatoa wito kwa wananchi wote mkoani Tanga kuendelea kutoa
ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi la Polis
ili kuzifanyia kazi na kuimarisha hali ya utulivu na amani"
"Wananchi
wa mkoa wa Tanga muendelee kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi
katika maendeo yenu na kutumia wakaguzi kata wa jeshi la Polisi waliopo
katika kata zote mkoani hapa katika kuzuia viashiria vya uhalifu na
wahalifu kabla haujatendeka katika maeneo yenu" alisema kamanda ACP
Mchunguzi.
Post A Comment: