Na DENIS CHAMBI, TANGA.

SERIKALI imewaagiza wakandarasi na wawekezaji wa kimataifa wanaoutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati hapa nchini kuhakikisha kuwa wanazingatia usawa wa kijinsia katika utoaji wa ajira kwenye shughuli mbalimbali  wanazozisimamia ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele cha wazawa wakiwemo wanawake na makundi maalum.

Rai hiyo imetolewa mkoani Tanga na waziri wa jinsia wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akimwakilisha waziri mkuu Kassim Majaliwa katika kufungua kongamano la wanawake na manunuzi lililoandaliwa na Mbunge wa  viti maalum mkoa wa Tanga Mhandishi Mwanaisha Ulenge ambapoa amesisitiza kuwa ni lazima ushiriki wa jamii katika utekelezaji wa miradi hiyo upewe kipaumbele. 
 
Aidha taasisi zote zinazotekeleza na kusimamia miradi ya kimkakati zihakikishe kuwa zinawasilisha taarifa za utekelezaji wa ushiriki wa watanzania katika ofisi ya waziri mkuu kupitia Baraza la  Taifa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ili kuiwezesha nchi kupata  na kupima thamani inayobaki kwenye uchumi wa nchi.

"Waziri mkuu anasisitiza kuwa wawekezaji  na wakandarasi wa maswala ya kimataifa wa maswala ya kiuchumi wahakikishe kuwa maswala ya kujengea ujuzi kwa watanzania uhaulishaji wa teknolojia na ushiriki wa jamii kwenye eneo la uwekezaji yanapewa kipaumbele na taasisi zote zinazotekeleza mradi wa kimkakati ziwasilishe taarifa katika ofisi ya waziri mkuu kupitia baraza la  Taifa la uwezeshaji ili kutuwezesha nchi kupima thamani ya  kutokana na ushiriki wa watanzania alisema  Gwajima

"Watanzania hususan wanawake wapewe kipaumbele katika ajira  na manunuzi ya umma katika miradi yote ya kimkakati inayotekelezwa nchini na  kwenye fursa za biashara kupitia ujuzi walio nao na bidhaa ili kukidhi viwango"

"Lakini pia waziri mkuu anasisitiza ufwatiliaji na tathmini kuhusu  ushirikishwaji wa watanzania katika miradi ya kimkakati uendeleee kufanyika ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki kuhusu changamoto zinazojiyltokeza mara kwa mara ili ushiriki wa watanzania uweze kuwa wenye tija na manufaa kwa ujumla na mimi nasema taarifa zote tutazifwatilia na miradi itekeleze uwiano wa kijinsia ili kutimiza adhima ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya uwezeshaji wanawake kiuchumi" alisisitiza Dkt. Gwajima.

Dkt Gwajima amabaye pia alizindua taasisi ya Ng'arisha Maisha  iliyoanzishwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mwanaisha Ulenge amewataka wanawake  kujiunga na kutumia vyema mabaraza ya uwezeshaji wanawake kiuchumi yaliyopo ili kuweza kuwasaidia katika maswala mbalimbali yanayowahusu ikiwemo ya kiuchumi huku akizitaka taasisi za kifedha kuendelea kuwewezesha mikopo wananchi ili kuweze kujikwamua kiuchumi .

Awali akizungumza mkurugenzi wa taasisi ya  Ngarisha maisha  Foundation Mhandisi  Mwanaisha Ulenge amesema kupitia taasisi hiyo isiyokuwa ya kiserikali wamedhamiria kuwainua wananchi hususan wanawake  katika kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta za kilimo uvuvi na biashara sambamba na kuunga mkono juhudi zote za serikali zinazolenga kuwaletea maendeleo wananchi.

"Taasisi ya Ng'arisha  Maisha foundation ni  ya kitaifa isiyokuwa ya kiserikali  inayolenga kuwainua wananchi kiuchumi hususan wanawake ,  taasisia imeleta mafunzo hayo kwa lengo la kuunga mkono jiyihada za serikali katika  kuwaleta watanzania maendeleo,  taasisi ya NMF imedhamiria  kuunga mkono jitihada za serikali katika kutatua changamoto za makundi maalum wakiwemo wanawake,  na kuhakikisha mipango ya serikali ya kimaendeleo inawafikia walengwa wakiwemo wanawake"

"Taasisi ya  Ng'arisha Maisha foundation 'NMF' itasisimamia ugawaji wa mbegu bora za Alizeti kwa wakulima hususan wanawake na kuwapelekea wananachi kuachana na kilimo cha asili badala yake kujiingiza kwenye kilimo cha kisasa,  na taasisi itaendelea kugawa mbegu bora kwa wananachi hususan wanawake, ni matumain yetu barabara ya Handeni kwenda Kibirashi wakulima wa zao la Alizeti wataweza kunufaika nayo".

"Pamoja na kuwezesha mbegu kwa wananch nimewezesha vijana kupata elimu katika vyuo vya kati pamoja na kuwezesha vifaa tiba kwa  watoto njiti. nipo kwenye mchakayo wa kuwezeaha miguu bandia 100 kwa  wahitaji, kuhusu uvuvi bado wanawake  walionufaika ni wachache sana,  taasisis yeyu itaweka mipango zaidi kuhakikisha wanawake wengi zaidi wananufaika tunaomba serikali iwezeshe vifaa ili wanawake waweze kunufaika na uchumi wa bluu".

Kwa upande wake waziri wa afya na mbunge wa  Jimbo la  Tanga Ummy Mwalimu amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mhandishi Mwanaisha Ulenge kwa kuja wazo la kuanzisha taasisi ya Ng'arisha Maisha foundation ambayo inakwenda kugusa Maisha ya wananchi moja kwa moja hususan wanawake katika nyanja mbalimbali.

"Tunashukuru sana mheshimiwa Ulenge kwa kuthubutu na tutaendelea kufanya kazi pamoja kwaajili ya manufaa ya wanawake wa mkoa wa Tanga hususan kupitia taasisi hii uliyoianzisha lakin Jambo la kusistiza ni kwamba  uchumi unaendana na afya bora kwahiyo pia tutazungumza  na maswala ya saratani hususan saratan ya kizazi, matiti tuweze kupata matibabu" alisema Ummy.
 
 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga na mkurugenzi wa taasisi ya Ng'arisha Maisha Foundation Mhandisi Mwanaisha Ulenge akizungumza katika kongamano la wanawake na manunuzi ya Umma(Daraja Comference )lililowakutanisha wanawake zaidi ya 1000 wa mkoa wa Tanga kujadii fursa mbalimbali ikiwemo za uchumi.
 

Share To:

Post A Comment: