Na John Walter-Hanang'

Wadau wa Maendeleo mkoani Manyara Kampuni ya Dutch Corner ya mjini Babati kwa kushirikiana na Madereva Boda boda wilaya ya Hanang'  wametoa misaada mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Katesh A iliyopo wilayani humo.

Zawadi ambazo zimekabdishiwa kituoni hapo na Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara George Katabazi  ni sukari, mchele, mafuta ya kupaka, sabuni za kufulia, vinywaji na mafuta ya kupikia.

Zoezi hilo limefanyika katika Tamasha la Nyama Choma lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mkoani manyara kwa kushirikiana na Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) likiwa na lengo la kutoa elimu kwa kundi hilo,  umuhimu wa kushirikiana katika kudhibiti uhalifu.

Mkuu wa shule ya Msingi Katesh A Matilda Shio amelipongeza jeshi la polisi, madereva boda boda na wadau wengine waliogushwa na kupeleka misaada hiyo shuleni hapo.

Kauli Mbiu katika Tamasha hilo ni Manyara Bila Uhalifu inawezekana, tii sheria bila Shuruti.


Share To:

Post A Comment: