Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda,akiwasilisha bungeni Jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026.

WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia itaendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya vyuo 64 vya ufundi stadi (VETA) vya wilaya
na chuo kimoja cha Mkoa wa Songwe.

Hayo yameelezwa leo bungeni Mei 12,2025 na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya  bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026. 

Waziri Mkenda  amesema Wizara itaendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya vyuo 64 vya ufundi stadi (VETA) vya wilaya na chuo kimoja cha Mkoa wa Songwe.

Amesema Serikali itaendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi na vyuo vya maendeleo ya wananchi.

Amesema lengo ni  ili kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu ya amali.

Amesema Wizara itaanza na  ujenzi wa vyuo vitano (5) vya ufundi (Polytechnics college) katika Mkoa
wa Rukwa, Kigoma, Mtwara, Morogoro na Zanzibar.

Share To:

Post A Comment: