Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameshiriki mbio fupi za kilomita 5 katika mashindano ya Tulia Marathon yaliyofanyika katika Jiji la Mbeya ambapo mbioz hizo ziliongozwa na Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na maelfu ya wananchi kutoka ndani na nje ya nchi.
Katika tukio hilo, Mhe. Mtaka ameonyesha mshikamano wa kitaifa na kupongeza juhudi zinazofanywa kupitia michezo katika kuimarisha afya, kukuza utalii na kuendeleza maendeleo ya jamii. Alisisitiza kuwa ushiriki wa viongozi katika shughuli za kijamii una mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya taifa.
“Nimefarijika kuona namna ambavyo mbio hizi zimewaleta pamoja Watanzania kutoka kila kona ya nchi yetu. Hii ni dalili kwamba michezo si tu burudani bali ni nyenzo ya kuunganisha watu na kuchochea maendeleo ya kweli,” alisema Mhe. Mtaka.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, kwa maandalizi bora ya Tulia Marathon, ambayo imeendelea kuwa jukwaa kubwa la kuwakutanisha wananchi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi.
Post A Comment: