"Kuna mambo mengine sikutaka kuyasema kwasababu nina uwezo mkubwa sana wa kupuuza lakini nimechokonolewa sana na baadhi ya watu kiasi ambacho inawezekana kuna baadhi ya watu mkachanganywa. Kwahiyo kwasababu nimelazimishwa, mengi nitapuuza, nitasema walau moja, naomba mnikubalie.
Kuna mtu mmoja ambaye amekuwa akijinadi siku nyingi anasema wakati anaenda kwenye SendOff alitumia Koti langu mimi mtoto wa muuza uji. Lakini leo hii anadiriki kufikia kusimama mahali anasema eti Gambo ameumiza watu wengi, leo nataka niwaulize hivi mimi na yeye nani ameumiza watu wengi katika nchi hii? hivi mnapajua Dar Es salaam ninyi? nendeni mkatafute habari zake kule hata kumsalimia mtaogopa.
Nataka popote alipo mumuambie mikono yangu ni safi!sima changamoto yoyote na sijamuumiza yeyote badala yake nimesaidia watu wengi sana kote nilipopita. Nimesaidia watu wenye ulemavu, tumewapatia viti mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia, tumewasaidia watu kupata miguu bandia ambao hawakutarajia kupata ulemavu, tumesaidia vituo vya yatima, tumesaidia kila mahali. Mwambieni hayo ni matendo mema hakuna hata moja la kumuumiza mtu."
Na nimeamua nisema kwasababu amesema eti nenda kwa wananchi wa Arusha, nenda kawaombe radhi, wananchi wa Arusha nimewahi kuwakosea?"- Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini.
Post A Comment: