Wanachama zaidi ya mia moja wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kutoka kata za Engutoto na Lemara Jijini Arusha, wamepokelewa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwenye Mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo unaofanyika leo kwenye Viwanja vya soko kuu Jijini Arusha.

Akizungumza kwaniaba ya wawakilishi hao waliopanda jukwaani kuwakilisha wengine waliokihama Chama Cha Chadema, Aliyekuwa Katibu wa Baraza la Wazee kata ya Lemara, amewaambia wananchi wa Arusha Mjini kuwa aliyewaondoa Chadema ni Mhe. Mrisho Gambo, kutokana na kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoshuhudiwa ndani ya miaka mitano ya Uwakilishi wa Mbunge huyo kwenye Bunge la Tanzania pamoja na usimamizi wake wa karibu wa miradi mbalimbali ya maendeleo Jijini Arusha.
















Share To:

Post A Comment: