Na John Walter-Babati

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amewataka wananchi kulinda miundombinu ya maji iliyojengwa wilayani humo kwa sababu serikali inaingia gharama kubwa kuitekeleza ili kufikisha huduma ya majisafi maeneo mbalimbali.

Twange amesema hayo akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa kata za Gidas na Boay ambapo kunatajwa kuwa na kero ya baadhi ya watu wasio waaminifu kukata mabomba na kusababisha watu wengine kukosa huduma ya maji.

Amesema serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maji hivyo ni  wajibu wa kila mmoja kuilinda  na kuwakemea waharibifu.

Aidha amewataka wananchi wa Gidas  kulipa bili za maji kwa wakati na viongozi wa vijiji wasimamie hilo ili kamati ya watumiaji maji iweze kujiendesha na huduma hiyo iendelee kupatikana katika maeneo yao.

Katika kikao hicho mkuu wa wilaya ya Babati aliambatana na meneja wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilaya ya Babati mhandisi Felix Mollel.


Share To:

Post A Comment: