Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof Joyce Ndalichako amesema kuwa takwimu zilizofanywa mwaka 2021 zinaonesha jumla ya watu milioni 2.9 hupoteza misha duniani wakiwa katika mazingira ya kazini na jumla ya watu milioni 402 duniani hupata ajali wakiwa katika mazingira ya kazini.


Waziri huyo ameeleza hayo leo Aprili 26 ,2023 jijini Dodoma na alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kilele cha maadhimisho ya Usalama wa Afya mahala pa kazi(Osha) yatakayofanyika kitaifa mkoani Morogoro.

Mbali na hilo amesema kuwa kwa takwimu za Nchini Tanzania zinazoishia Julai mwaka 2019 hadi 2022 jumla ya magonjwa katika maeneo ya kazi ni 4993 ambapo ajali ni 247 na vifo ni 217.

Prof. Ndalichako amesema kuwa maadhimisho hayo nchini Tanzania ni ya 19 na kitaifa yatafanyika mjini Morogoro na kilele kitakuwa tarehe 28 Aprili na wakati huo sikukuu ya wafanyakazi nchini kitaifa itakuwa Morogoro.

Amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa usalama mahali pa kazi na mazingira ya kazi serikali imekuwa ikishirikiana na OSHA kuhakikisha mazingira ya kazi kwa watumishiwa sekta zote wanafanya kazi kwa mazingira ambayo ni salama kwa afya zao.

Waziri huyo amesema kuwa serikali inatambua sheria na 5 ya usalama wa afya na usalama katika maeneo ya kazi kwa kuhakikisha kila mmoja anayefanya kazi anafanya kazi katika mazingira salama ambayo hayatakuwa hatarishi kwa mtumishi.




pia amewataka watumishi kuhakikisha wanapokuwa wakisafiri kikazi kuhakikisha wanatoa taarifa ili inapotokea ajali au kifo iwe raisi kuwatambua na kuwa tayari wapo katika mfuko wa fidia jambo ambalo ni muhimu kulizingatia.

Hata hivyo Prof. Ndalichako ameeleza kuwa sehemu kubwa ya uzalishaji kwa maana ya viwanda kunaongoza kunachangia kwa kiasi kikubwa katika kusababisha ajali kutokana na kuwa vijana wengi wasiokuwa na uzoefu kufanya kazi katika viwanda hivyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi,Hadija Mwenda amesema kuwa kutokana na utafiti mdogo walioufanya wamebaini ajali nyingi kazini zimekuwa zikitokea katika Sekta ya uzalishaji kwa maana ya Viwanda huku akieleza hatua ambazo wameanza kuchukua


Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA)Tumaini Nyamhokya ameiomba Serikali kuweka Sheria kali ambazo zitawabana Waajiri kuzingatia masuala ya usalama mahala pa kazi.


Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani( ILO) Getrude Sima amesema wataendelea kushirkiana na serikali ya Tanzaniana kuitaka kuendelea kutumia sheria namba tano ya usalama mahala pa kazi.




Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: