Na John Walter-Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amesema umri waliotawala wakoloni unazidi umri wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofikisha miaka 59 sasa.

"Wakoloni walizitawala Tanganyika na Zanzibar zaidi ya Miaka 70" alisema Nyerere

Wakati wanatutawala walikuwa wachache kuliko sisi lakini walitutawala, na walikuwa wakitufanyia kila aina ya Ukatili, walikuwa wanatumia kanuni ya GAWA,TUGAWANE, kuchonganisha" alisema Nyerere

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amezungumza hayo wakati alipowaongoza Wananchi wa wilaya ya Babati na Viunga vyake Kwenye Sherehe za  kumbukizi ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  zilizofanyika katika Kijiji cha Galapo leo April 26,2023.

Nyerere amewaambia Wananchi waendelee kudumisha Muungano ulioasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mwenzake wa Zanzibar Amani Abeid Karume kwa kufanya kazi.

Amesema wakoloni wa kijerumani,uingereza na waarabu walizitawala Zanzibar,Tanganyika kwa muda mrefu wakiwatumikisha kwa mabavu na kuwanyima huduma Muhimu za kijamii.

Katibu tawala Mkoa wa Manyara Karolina Mthapula amesema wiki ya Muungano wamepanda miti maeneo mbalimbali ikiwemo ya Matunda na Vivuli katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Vijijini.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema wataendelea kudumisha Muungano huo kwa kuyaenzi yote yaliyoanzishwa na waasisi.

 

Kadhalika maadhimisho hayo yaliyoanza April 17,2023 yaliambatana na Mashindano ya Michezo mbalimbali kwa Wanaume na Wanawake, Usafi wa Mazingira,upandaji miti pamoja uandishi wa Insha kwa shule za Msingi na Sekondari ambapo washindi wamekabidhiwa zawadi na mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere.

 

 

 

Share To:

Post A Comment: