Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer akiongea wakati wa utoaji wa mikopo kwa vikundi 27 vya wananchi wa Halmashauri hiyo
Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi na serikali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanavikundi wakionyesha mfano wa hundi pesa za mikopo ambazo vikundi 27 vimepata
Baadhi ya wanavikundi wakionyesha bango ambalo linampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati wa kupokea mikopo kutoka Halmashauri ya Mji Mafinga.
Baadhi ya wanavikundi wakiwasikiliza viongozi mbalimbali wakati wa zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa Halmashauri ya Mji Mafinga.


Na Fredy Mgunda, Mafinga.

HALMASHAURI ya Mji Mafinga imetoa mikopo kwa Vikundi 27 wenye thamani ya kiasi cha shilingi 276,7000,000 ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuviwezesha kiuchumi Vikundi hivyo kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Halmashauri zote zitoe mikopo hiyo.

Akizungumza wakati wa kutoa mikopo hiyo kwa Vikundi hivyo,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer alisema kuwa vikundi vinavyopewa mikopo ni 27 ambapo  vikundi 13 ni vya wanawake wamekopeshwa shilingi 131,800,000/-,Vijana vikundi 8 wanakopeshwa shilingi 100,800,000/- Watu wenye Ulemavu vikundi 6 wamekopeshwa shilingi 44,100,000/-

Laizer alisema kuwa Vikundi hivyo vinatakiwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kuendelea kupata mikopo hivyo ambayo haina riba yeyote ile.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi (CCM),George Kavenuke alisema kuwa Utoaji wa Mikopo ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 kupitia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Rais Samia Suluhu Hassan inatoa mikopo ili kuinua uchumi wa wananchi.

Kavenuke alivitaka vikundi vilivyopewa mkopo visimuangushe Rais na uongozi wa Halmashauri kwa kurejesha mikopo hiyo ili kutoa nafasi kwa vikundi vingine kupata mkopo huo ambao hauna riba.

Aliwaomba wananchi wote ambao wamepata mikopo hiyo kuendelea kumuunga mkono Rais Samia na kumusemea mema anayowafanyia wananchi katika kuhakikisha wanapata maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

Kavenuke alisema kuwa lazima mikopo hiyo irejeshwe kwa sababu ipo kisheria na msiporejesha hatua kazi za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu wote waliotafuna fedha hizo.

Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Regnant Kivinge alisema kuwa awali wananchi walikuwa wanaona fedha za Halmashauri kama sadaka Ila kwa sasa ni kaa la moto bora ikakope benki kuliko kuchezea fedha hizo.

Kivinge alisema kuwa kuna wananchi wapo mahakamani na wengine polisi kwa ajili ya kuzichezea fedha za mikopo ya Halmashauri hivyo kama hamjajipanga juu ya matumizi ya mikopo hiyo bora muache.

Alimazia kwa kusema kuwa Sasa watakuwa wanafanya ziara ya kushtukiza kwenye vikundi ili kuangalia maendeleo ya fedha za mikopo walizopewa na Halmashauri ya Mji Mafinga zinafanya kazi gani.

Saad Mtambule ni mkuu wa wilaya ya Mufindi aliwataka wananchi walipata mikopo hiyo kwenda kuitumia kwenye shughuli walizokusudia za kuongeza mitaji yao.

Mtambule alisema kuwa atakaye tokomea na fedha hizo sheria itachukua mkondo wake mara moja bila woga wala kumuogopa mtu.

Share To:

Post A Comment: