Na Gift Mongi,Moshi 

 Zikiwa zimebaki takribani siku 12 ili kufika novemba 18 ambapo kutafanyika mbio za "Vijana Green Marathon' jijini Dodoma vijana wametakiwa kujitokeza kwa wingi ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali.

 Hadi sasa vijana mbalimbali kutoka umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)katika wilaya ya Moshi wameonesha nia ya kushiriki mbio hizo ambazo zina lengo la kuudhihirishia umma kwa kazi nyingi zinazofanywa na serikali ya CCM. 

 Yuvenal Shirima ni mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini ambapo amesema kwa sasa vijana wengi wanatambua jinsi serikali imekuwa bega kwa bega katika kuleta maendeleo. 

 Amesema vijana ni jeshi kubwa hivyo wao wanao wajibu mkubwa katika kuuambia umma wa watanzania yale mema ambayo yanafanyika au yamefanyika kwa maslahi ya taifa Shirima anasema katika kudhihirisha hayo vijana nao wanaoekana kuguswa moja kwa moja na miradi ambayo inatekelezwa au imetekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa. 

 Mjumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Moshi Vijijini Emanuel Mlaki amesema kwa sasa ni wajibu wa vijana kusemea yale mazuri yanayofanyika ili kuondoa upotoshwaji ambao umekuwa ukifanywa na kikundi cha watu wachache. 

 Amesema kipo kikundi cha watu wachache wasiokubali kwa maksudi miradi mingi inayoendelea kufanyika na kuwa ni lazima ukweli uwekwe wazi maana hakuna mtu asiyeona au kusikia kuhusu kishindo cha awamu ya sita. 

 Agnes Mallya ambaye naye ni miongoni mwa watakaoshiriki katika mbio hizo amesema ni vyema vijana wakawa na uzalendo kwa kuisemea serikali kwa ambavyo imekuwa ikipambana kuleta maendeleo kwa wananchi wake. 

 Amesema kitendo cha vijana kukaa kimya kana kwamba hakuna kilichofanyika sii cha kizalendo kwani katuka miradi mingi inayotekelezwa kwa sasa wanufaika wakubwa ni vijana.
Share To:

Post A Comment: