Na Gift Mongi-Moshi 

 Vijana nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali katika kuleta maendeleo yanayoonekana kugusa makundi yote katika jamii. 

Katika kufanya hivyo itawawezesha kuweza kunufaika na miradi mbali mbali ambayo serikali imekuwa ikiianzisha ambapo ipo ile ya moja kwa moja inayowalenga vijana ambapo ndani yake zipo ajira za muda na zile za kudumu. 

 Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenali Shirima akizungumza katika maandalizi ya mbio zitakazofanyika jijini Dodoma novemba 18 2020 zinazojulikana kama 'Vijana Green Marathon' amesema tayari serikali imefungua milango kwa vijana. 

Amesema miongoni mwa milango iliyofunguliwa kwa vijana ni pamoja na mikopo isiyokuwa na riba kutoka katika halmashauri ambayo ni asilimia 4 kutoka katika makusanyo ya ndani lakini kuendelea kuongezwa kwa fedha kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini. 

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ni kuwa hata miradi mingi ikiwemo ya ujenzi wa barabara,reli ya kisasa(SGR)madaraja na hata hospitali mbali mbali wanufaika wakubwa katika soko la ajira ni vijana hivyo ni muda sasa wa kutambua jinsi serikali inavyowafungulia fursa. 

Kuhusu mbio hizo za 'Vijana Green Marathon' amesema kusudio lake ni kufikisha ujumbe kwa jamii lakini pia kumshukuru rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa taifa wa CCM kwa mambo makubwa anayoendelea kuyafanya sio tu kwa taifa bali hata kwa kundi la vijana wenyewe. 

Richard Kessy ni miongoni mwa vijana wa umoja huo ambapo amesema ipo haja ya kushukuru serikali kwa kile walichofanyiwa kundi hilo ambalo kuna kipindi lilionekana kutelekezwa. 

Amesema kundi la vijana ni kubwa na linahitaji kuwezeshwa kwa ajili ya ustawi wa taifa kwa siku za mbeleni na kuwa kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuna jitihada za maksudi ambazo zimefanyika katika kulinususru kundi hilo Doreen Mmasy amesema ili taifa liweze kuwa na nguvu kazi ya kutosha ni lazima kuwekeza mtaji kwa kundi la vijana ambao ndio walio wengi kama inavyofanywa hivi sasa na serikali ya awamu ya sita. Mwisho
Share To:

Post A Comment: