NA DENIS CHAMBI, TANGA

Hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo imezindua mpango wa matibabu ya kibingwa ambapo karibu wagonjwa 366 watanufaika na huduma hiyo inayotolewa bila malipo na madaktari bingwa wa taasisi ya Pelecks kutoka nchini Uingereza wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka hospital hiyo.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema kuwa bado Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madaktari bingwa ambapo uhitaji kwa Tanzania nzima ni madaktari 1782 huku wakiwepo wakiwa ni 992 pekee. 

Waziri Ummy ameishukuru taasisi hiyo kwa kujitolea kuja kutoa hduma hiyo bure ambapo wagojwa wenye magonjwa mbalimbali watapata huduma yakiwemo magonjwa ya moyo, upasuaji wa mishipa ya fahamu huku akiwaomba mara baada ya kumalza kwa mkoa wa Tanga kuangalia uwezekano wa kufika katika mikoa mingine ya Tanzania kutoa matibabu hayo

 “Tuna uhaba mkubwa sana wa madktari bingwa nchini tanzanai , tunatakiwa tuwe na madaktari bingwa 1782 lakini waliopo ni 992 tu kwahiyo utaona uhaba wa madaktari bingwa nchini ini asilimia hamsini na watanzania wanahitaji huduma hizi za matibabu ya kibingwa ikiwemo upasuaji wa magojwa ya moyo, mishipa ya fahamu, m na maswala mengine kwahiyo tunapopata wadau wa kuja kutusaisia ka Pelecks tunawashukuru sana na huduma hii isiishie Tanga tu nendeni na mikoa mingine ili tuweze kuwafikia wagonjwa wengi zaidi” aisema 
Ummy. 

Aidha katika hatua nyingine waziri Ummy amewataka watanzania kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya Corona pamoja kuendelea kuchukuwa tahadhari ya ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umekithiri katika nchi jirani ya Uganda.

 “Wizara inakusudia kuzindua booster doze ya ugonjwa wa UVIKO -19 ado Corona ipo niwaombe sana watanzania kujitokeza kupata chanjo ya Corona kama hatujapata chanjo tujitahidi tupate tutafanya kila wilaya kuhamasisha kama mmefwatilia vyombo vya habari Corona imerudi tena”

 “Napenda kutoa tahadhari juu ya ugonjwa wa Ebola upo katika nchi jirani ya Uganda kwahiyo tuchukuwe tahadhari ya kujilinda na kujikinga na ugonjwa huu usiingie katika nchi yetu kama sio lazima kwenda kwenye nchi zenye ugonjwa huu tunaomba msisafiri takwimu zinaonyesha wakipata watu kumi wanne wanafariki kwahiyo tuombe sana Mungu ugonjwa huu usiingie katika nchi yetu” alisema 
Waziri Ummy. 

Akizungumza Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa ameipongeza taasisi ya Pelecks kwa mchango wao kwa watanzanai kupitia wizara ya afya kwa kuhakikisha inazidi kuimarisha huduma za afya hapa nchin huku akiwaomba kuongeza siku za kutoa huduama hiyo ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi wenye matatizo mbalimbalii” 

“Niwashukuru sana taasisis ya Pelecks kwa kuendelea kujali afya ya watanzana na sisi kazi yetu kubwa ni kuendelea kuwaombea afya njema wenzetu hawa kwa kile ambacho wamedhamiria kufanya kwa wanatanga lakini tuwaobe ikiwezekana kuongeza siku za kutoa huduma ili tuwafikie watu wote ambao wanahitaji matibabu lakini hawana pesa za matibabu” alisema mgandilwa. 

Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Jonathan Budenu alisema kuwa ujio wa huduma hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au kuondokana na matatizo ya wagonjwa ambao wamekuwa wakihitaji huduma za kibingwa huku akikiri changamoto ya uhaba wa vitanda vitakavyotumka kwaaajili ya wagonjwa watakaokuwa wakipatiwa huduma hiyo. 

“Uwepo wa zoezi hili utatusaidia kuwa kiasi kikubwa kuwahudumia wagonjwa ambao tungewapasua kwa muda mrefu na wegine walikuwa hawana uwezo, tutakuwa na changaoto ya vitanda kwa wagonjwa ambao watakuwa wakipatiwa matibabu baada ya upasuaji kwa sababu vitanda vilivyopo ni vichache ukilinganisha na wagonjwa waliopo” alisema Budenu. 

Huduma hiyo itaghalimu kiasi cha shilingi Million 876 ikitolewa ndani ya siku 7 ndani ya Hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo. 
Share To:

Post A Comment: