Na John Walter-Manyara 
Mbunge wa Vijana Taifa kutoka mkoa wa Manyara Asia Halamga ametoa msaada wa Karatasi (REEM PAPERS) kwa ajili ya uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye majimbo yote Matano ya mkoa wa Manyara.

Halamga amekabidhi Karatasi hizo leo Mbele ya Katibu wa NEC, Siasa, Itikadi na uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka Katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi mjini Babati.

Amesema Karatasi hizo zitasaidia katika zoezi la kutoa fomu za kugombea nafasi mbalimbali na kuondoa usumbufu wa kusuasua kwa utoaji wa fomu hizo katika majimbo ya mkoa wa Manyara.Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Babati Daniel Muhina amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo akieleza kuwa ametoa katika muda muafaka ambao Chama kinaendelea na chaguzi zake ndani ya Chama.

Share To:

Post A Comment: