Na Denis Chambi Tanga,

WANANCHI wametakiwa kutoa taarifa za matukio ya ukatili pale  yanapotokea na kuyashuhudia katika mazingira yao  na hatimaye kuyaripoti katika Mamlaka husika ili hatua ziweze kuchukuliwa ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Jeshi la Polisi pamoja na wadau mbalimbali katika kukomesha vitendo hivyo kwa maslahi ya Taifa la kesho.

Wito huo umetolewa na  Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi  Mkoa wa Mbeya  wakati akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga katika Parokia ya Mtakatifu Anthony wa Padua  kwenye Ibada ya misa Takatifu iliyofanyika Jumapili 27 September 2026  ambayo amesema kuwa matukio mengi ya ukatili yamekuwa yakianzia ndani ya familiya yakihusisha ndugu wa karibu.

Aidha amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakifanya ukatili bila kujua  hali ambayo imekuwa ikiwaathiri wanaowatendewa kiakili ,kiuchumi kijinsia na kifamiliya na watu wengi wamekuwa wakikaa kimya baadala ya kutoa taarifa sehemu husika ili wahusika waweze kuchukuliwa sheria hali ambayo imekuwa ukichangia kuongezeka kwa vitendo vya hivyo.

"Uhalifu na wahalifu unaendelea kushamili kwenye jamii kwa sababu ya watu wema kuamua kukaa kimya bila kutoa taarifa sehemu sahihi ,sasa hivi kuna ukatili unafanyika mara kwa mara yawezekana watu wanaweza kufanya ukatili bila kujua, ukatili unaweza kumuathiri mtu kiakili, kiuchumi kijinsia na kifamiliya tusikubali kukaa kimya tutoeni taarifa ili sheria ziweze kuchukua mkondo wake" amesema 

Ameongeza kuwa baadhi ya wana ndoa wamekuwa wakipigana ndani ya nyumba  hususani wa kina mama wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa bila ya wahusika kutoa taarifa kwa Mamlaka husika na baadaye kuja kuleta athari mbalimbali ikiwemo ndoa kuvunjika, vifo pamoja na kuathiri watoto wao kisaikolojia.

Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuwa na desturi ya kuwakagua watoto wao pale wanapotoka mashuleni au nyakati ambazo hawapo katibu nao pamoja na kujenga ukaribu  ili kuweza kubaini kama kuna viashiria vyovyote vya ukatili vinavyoweza kumharibu mtoto.

"Tumekuwa tukiwalaza watoto wa jinsia mbili pamoja, kinachofanyika yawezekana hatukijui ikiwemo ngono bila wazazi na walezi kujua wengine ni mabinti wengine ni wakiume hivyo kuna changamoto ya kimalezi matokeo yake tunakuja kuwa na jamii ya watu mashoga na wasagaji, mtaani nako sio salama usiache tu mtoto aende shule anaporudi kaa naye mkague na uongee naye, ulimwengu wa sasa hivi sio salama
,kuna wanaofanya uhalifu kwa sababu ya kulipa visasi, kuna ambao walifanya na kufanyiwa ukatili wameshindwa kupata huduma stahiki hivyo wanaendeleza hii tabia" ameongeza. 


Kwa upande wake Mtendaji wa Dawati la Jinsia kutoka Mkoa wa Kilimanjaro  Koplo Bahati amesema kuwa kila mmoja kwa nafasi yake anao wajibu wa kukemea ukatili katika jamii kupitia shughuli mbalimbali anazofanya Kila siku na sii kiziachia Mamlaka pekee ambazo bila ushirikiano wa jamii na wadau wengine haziwezi kukomesha vitendo vya ukatili.

"Kwa sababu unaishi na upo hai basi tambua kwamba kuna kazi ya Mungu unatakiwa uifanye Je unaifanya?  kila mtu ndani yake ana sauti ya Mungu inamuongoza sisi tuwe wavuvi wa wengine, sasa wewe mwenzangu julize umetumwa wapi?, sasa hivi wimbi kubwa la ukatili linaendelea basi naomba tuende tukaifanye kazi tuliyotumwa, tuongozwe katika kutenda yaliyo mema" amesema Koplo Bahati.


Akizungumza kwa  kwa niaba ya Paroko wa Kanisa hilo , Paroko Msaidizi Godfrey Joseph amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada na hatua mbalimbali linazoendelea kuzichukua katika kukomesha vitendo vya ukatili huku akiitaka jamii kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati.


Maafisa hao wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wapo Mkoani Tanga ambapo pamoja na shughuli nyingine wanasisitiza utoaji wa elimu kwa jamii juu ya kukinga kidhibiti na kupinga vitendo vya ukatili kwenye jamii hususani kwa watoto ambao ni Taifa la kesho.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: