Na: OWM–TAMISEMI, Dar es Salaam

Timu ya Wataalam iliyoundwa kwa ajili ya kuchambua hoja za wananchi kuhusu mgogoro wa muda mrefu wa mipaka ya kiutawala na mpaka wa Msitu wa Kazimzumbwi, imewasilisha taarifa ya uchambuzi wa hoja zaidi ya 60 zilizowasilishwa na wananchi 22 kwa Mawaziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Timu hiyo inaundwa na Mkurugenzi anayeshughulikia Mipango Miji na Vijiji wa OWM–TAMISEMI, Kamishna wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara hiyo pamoja na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Taarifa hiyo imewasilishwa Oktoba 2, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa Septemba 23, 2026 na Waziri wa Nchi, OWM–TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, wakati wa mkutano wa Mawaziri hao watatu na wananchi uliofanyika katika Viwanja vya Chanika Zingiziwa kwa lengo la kusikiliza na kuchambua hoja zao.

Mkutano huo ulikuwa sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, aliyoyatoa Septemba 18, 2026 akiwa Dampo la Pugu, akiwataka Mawaziri hao watatu kukutana na wananchi ndani ya siku saba kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo wa mipaka ya kiutawala.












Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: