Na Denis Chambi, Tanga.

MASHIRIKA na Taasisi zisizo za Kiserikali  zinazofanya shughuli mbalimbali katika mkoa wa Tanga  yametakiwa kubuni Miradi endelevu na vyanzo vitakavyowasaidia kujipatia fedha za kuweza kujiendesha na hatimaye kutoka kutegemea  fedha za wafadhili huku wakitakiwa kushirikiana kwa pamoja kwa mustakabali wa kuwaletea wananchi maendeleo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani wakati akifungua  Jukwaa la mwaka la mashirika yasiyo ya Kiserikali na kilele cha maadhimisho ya mwezi wa maafisa maendeleo ya jamii ambapo amewasisitiza kuwa  uwepo wao katika jamii  una nafasi kubwa ya kuweza kuijenga Tanga kimaendeleo ikizingatiwa na fursa mbalimbali zilizopo ikiwa ni pamoja na Miradi wanayoitekeleza sambamba na  Ile ya Serikali.

" Mnafanya shughuli zenu katika mkoa ambao una fursa na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya mazingira Serikali peke yake haiwezi, kazi yenu nyinyi kama mashirika yasiyo ya Kiserikali ni nguzo muhimu sana kwani nyingi ndio mnafika vijijini mnaungana na maafisa maendeleo wa jamii na wananchi kupitia shughuli mbalimbali mnapaswa kujitathmini mefanya nini na mnatakiwa kufanya nini mnatakiwa muunganishe nguvu ili muweze kufanya pakubwa" amesema Dkt. Buriani.

"Tunawakumbusha na kuwahamasiaha kubuni Miradi endelevu itakayoweseaha kujitegemea  na kujiendesha , Serikali tunatambua kuwa nyinyi sio wapinzani wa Serikali bali ni wasaidizi wa Serikali na maendeleo ya wananchi ndio lengo letu sote" amesisitiza.

Aidha Dkt.Buriani ameongeza kuwataka wadau hao wa maendeleo mkoani humo  kutekeleza dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 ikiwa ni pamoja na kutoa elimu mbalimbali kwa jamii, pamoja na kutekeleza miradi ya kiuchumi ambayo itawasaidia wananchi kujiletea maendeleo.

Awali akizungumza Msajili msaidizi wa mashirika na taasisi zisizo za Kiserikali mkoani Tanga Gloria Malela  ameeleza kuwa jumla ya Mashirika 346 yanaendelea  kutoa huduma katika nyanja tofauti ikiwemo sekta ya elimu, afya msaada wa kisheria pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi sambamba na kuwasaidia wenye ulemavu katika jamii.

"Mpaka sasa mkoa wa Tanga tuna Mashirika 346 ambayo yapo hai na yanafanya kazi na wamejikita zaidi kutoa huduma katika sekta ya afya , elimu, msaada wa kisheria, ukatili wa kijinsia uwezeshaji wananchi kiuchumi na kutoa huduma stahiki kwa makundi maalum kama watu wenye ulemavu" amesema Malela.


Amebainisha kuwa  uwepo wa mashirika hayo ndani ya mkoa wa Tanga ikiwemo yanayotoa huduma kwa waraibu wa dawa za kulevya wilaya za Muheza , Pangani na Mkinga kumekuwa na idadi kubwa ya wananchi walioathirika na dawa za kulevya  wengi wakiwa ni vijana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika  yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Mkoa wa Tanga,  Mganga Khalifa ameipongeza na kuishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kuyalea Mashirika  na taasisi zisizo za Kiserikali huku akiahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zote zinazofanyika hapa nchini kwa maslahi mapana ya Taifa pamoja na kuwataka wadau hao wa maendeleo kuzingatia uwajibikaji pamoja na sheria zinazowaongoza.

"Tunaishukuru na kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri na kuwezesha Mashirika na Taasisi kufanya kazi zake kwa ufanisi sekta ya Mashirika mkoa wa Tanga inaendelea kutoa mchango mkubwa kwa Serikali kupitia afya, elimu, tunaendelea kusisyiz Mashirika na Taasisi zote kuendelea kuzingatia uwajibikaji na kuzingatia Sheria zinazotuongoza" amesema Khalifa.


Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika  yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Mkoa wa Tanga,  Mganga Khalifa akizungumza kwenye kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.




Baadhi ya viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizokuwa za Kiserikali wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: