Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Thomas Labi akitoa huduma kwa mwanachama wakati wa maonyesho ya 9 ya Technologia ya  madini mkoani Geita.


Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Nathan Makuchilo (kushoto), akikabidhi zawadi kwa kaimu Katibu tawala Mkoa wa Geita  Bw. Charles Chacha siku ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Nathan Makuchilo, akitoa huduma ya elimu na  huduma za PSSSF alipotembelea banda la Benk Kuu ya Tanzania alipofanya ziara ya banda kwa banda

Maafisa wa PSSSF wakitoa huduma na elimu kuhusu bidhaa za Mfuko wa PSSSF  walipofanya ziara ya banda kwa banda walipotembelea banda la Benk  kuu ya Tanzania

Afisa wa PSSSF akitoa huduma na elimu kuhusu bidhaa za Mfuko wa PSSSF  wakati wa ziara ya banda kwa banda walipotembelea banda la Bima ya Afya.

Maafisa wa PSSSF wakitoa huduma na elimu kuhusu bidhaa za Mfuko wa PSSSF  walipofanya ziara ya banda kwa banda walipotembelea banda la mahakama kuu ya Tanzania


Geita, Oktoba 3, 2026

Meneja wa PSSSF kanda ya Ziwa Magharibu, Bw.Thomas Labi, amewasihi wastaafu tarajiwa kuhakiki taarifa zao mapema kabla ya siku ya kustaafu, ili kuhakikisha wanalipwa jana kwa wakati na usahihi.  

Bw. Labi amesema hayo katika Maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita, ambayo yamehitimishwa Oktoba 3 2026, baada ya kudumu kwa siku 11, ambapo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekamilisha utoaji wa elimu na huduma kwa wananchi, watumishi wa umma, na wastaafu watarajiwa kupitia banda lake.

“Mfuko unadhamiria kuhakikisha makundi yote yanapata huduma na elimu kwa uelewa sahihi, tunashukuru watumishi wapya waliotembelea banda la PSSSF na kupata elimu juu ya PSSSF, Hifadhi ya Jamiii na elimu ya matumizi ya huduma za kidigitali”alifafanua Bw. Labi. 

Katika maonesho hayo, PSSSF ilitoa elimu ndani ya banda, timu ya PSSSF ikiongozwa na Kaimu Meneja Bw. Nathan Makuchilo, pia imetembelea wanachama moja kwa moja kwenye mabanda yao (banda kwa banda) ili kuendelea kuwafahamisha na kuwahudumia kwa njia ya kidigitali. Wanachama waliotembelea banda la PSSSF wameonyesha kuridhishwa na huduma walizopata, hasa matumizi ya mfumo wa PSSSF Member Portal unaowawezesha kuangalia taarifa zao kupitia simu za mkononi.

Pamoja na kufungwa kwa maonyesho hayo, Bw. Thomas Labi ametoa wito kwa wanachama na wananchi wote kuendelea kutembelea Ofisi za PSSSF zilizopo kote nchini ili kupata ufumbuzi wa changamoto, kuwasilisha kero au malalamiko, na kupata majibu kuhusu huduma za Mfuko

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: