MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, leo ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Leyla Mtumwa aliyeuawa mumewe, Kema Kasambula, kwa kuchomwa visu mwezi uliopita jijini London nchini Uingereza
Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha.

Mwili wa Leyla ulikuwa ukishikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya kujiridhisha ndipo wakaukabidhi kwa familia na hatimaye kutua nchini jana Jumatatu.
Leyla anadaiwa kuuawa na mumewe huyo, usiku wa kuamkia Machi 30, mwaka huu jijini humo ambapo sasa jamaa huyo anakabiliwa na kesi ya mauaji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: