Articles by "TASAF"
Showing posts with label TASAF. Show all posts

 


Kufuatia changamoto ya kukaa umbali wa takribani KM 24 wanayokumbana nayo walimu wa shule ya msingi Deo Sanga iliyopo katika kijiji cha Manga halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

Hatimaye Changamoto hiyo inaelekea kupunguzwa kwa kiasi kikubwa mara baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho kukamilisha nyumba pacha yenye thamani ya Tshs 92,410,714.29

Akitoa taarifa ya ujenzi wa Nyumba hiyo mbele ya Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi,Liston Ngimilanga ambaye ni afisa Mtendaji wa kijiji cha Manga amesema ujenzi wa nyumba hiyo umefikia hatua ya umaliziaji ambapo mradi huo mpaka sasa umegharimu Shilingi 91,360,714.29

"Katika kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi wa kijiji cha Manga,kijiji kilipokea fedha hizo kutoka serikali kuu kupitia TASAF kwa ajili ya ujenzi wa nyumba pacha na hii ni baada ya wananchi kuibua na kuthibitisha mradi"amesema Ngimilanga

Awali Mwalimu Naboti Ilongo kutoka shule hiyo amesema mpaka sasa shule hiyo ina nyumba nne lakini mahitaji yao ni nyumba saba hivyo mara baada ya ujenzi wa nyumba hiyo kutakuwa na mahitaji ya nyumba moja kwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya walimu kutoka mjini Makambako wakifanya kazi katika shule hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo amesema serikali imetoa kiasi hicho ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Manga na kupongeza kwa usimimizi wa mradi huo.

"Jengo ni zuri na hata umaliziaji wake umefanyika kwa umahili mkubwa,na kwa kweli niwashukuru CMC kwa kusimamia hii kazi na nina imani mwezi ujao mtakuwa mmemaliza hii kazi"amesema Ilomo

 


Wananchi wa kijiji cha Igagala halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe wameomba Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuwasaidia ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti (Mochwari) kwa kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kukamilisha mradi wao wenye thamani ya Milioni 501 kwa uaminifu bila kutokea vitendo vya wizi.

Ombi hilo limetolewa na wananchi wa kijiji hicho kwa Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo mara baada ya kukagua baadhi ya majengo ya kituo cha afya Igagala ikiwemo kichomea taka,jengo la upasuaji,jengo la mama na mtoto,jengo la Maabara pamoja na nyumba mbili za watumishi kupitia mradi wa uboreshaji wa miundombinu.

Awali mtendaji wa kata ya Ulembwe Sharifa Kunga akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika kijiji hicho amesema utekelezaji wa mpango ulianza mwaka 2015 ambapo jumla ya kaya 78 ziliandikishwa na mpaka sasa kaya mbili pekee zimebaki zikinufaika na mpango huo.

"Kupungua kwa walengwa kumetokana na sababu mbalimbali kama kuhama na kuimarika kiuchumi"amesema Sharifa Kunga

Kwa Upande wake mwenyekiti wa halmashauri  ya wilaya ya Wanging'ombe Agnetha Mpangile amesema kujengwa kwa majengo hayo kumezidi kuimarisha huduma za afya huku akishukuru TASAF kwa kubadilisha kaya maskini na kuwataka wananchi kutumia kituo hicho kikamilifu ikiwemo kuongeza idadi ya watu.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Dkt.Peter Nyanja amesema kijiji hicho kwa sasa ni miongoni mwa vijiji vilivyoimarika kiuchumi hali iliyopelekea wanufaika wa TASAF kubaki wawili pekee.

"Ukiangalia kulia na kushoto, makazi yamebadilika sana na nyumba zao ni kisasa  na hamna tena yale mabati yale ya zamani ndio maana uchumi umeongezeka na wamebakia watu wawili TASAF nao wako mwishoni kuhitimu"amesema Dkt.Peter Nyanja

Nyanja amesema lengo lao ni kufanya kituo hicho kuwa hospitali ndogo ndio maana kwa kushirikiana na wananchi wanahitaji ongezeko la  majengo ya kutolea huduma.

"Kituo hiki kipo kwenye barabara kuu ya kwenda Makete mapaka Mbeya kwa hiyo lengo letu tunataka tukifanye kuwa hospitali ndogo ndio maana tunaomba wodi ya Wanaume,Wanawake na Mochwari na hiyo ndio dira yetu ya wilaya"amesema Nyanja

Naye Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo amesema kupatika kwa huduma nyingi kwenye kituo hicho utakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi na kupongeza kazi kubwa ya ujenzi iliyofanyika huku akiagiza utunzaji wa mali za kituo cha afya ambapo pia amesema kwa kushirikiana na serikali wanakwenda kutafuta njia bora ya kutekeleza maombi hayo.

 


HALMASHAURI ya Arusha wilayani Arumeru imefanikiwa kutekeleza miradi 40 ya Maendeleo ya Jamii chini ya mfuko wa TASAF, yenye thamani ya bilioni2.3 ikiwe miradi ya ujenzi wa shuleni na kituo Cha Afya.


Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Selemani Msumi amesema miradi hiyo imefanyika katika vijiji 16 katika halmashauri hiyo na wamefanikiwa kupata miradi 40 ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu na afya ikiwemo miradi kuendeleza miundombinu katika Kijiji Cha oldonyowas katika sekondari ya oldonyowas na mradi wa ujenzi wa kituo Cha Afya Bwawani," amesema.

Msumi, amesema katika Kijiji cha Oldonyowas chenye Sekondari ya Oldonyowas umetekelezwa jumla ya miradi 11 yenye thamani ya zaidi ya milioni 920.

Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa mawili, ofisi mbili, choo cha matundu manne na samani, ujenzi wa nyumba mbili za walimu, ujenzi wa jengo la utawala, ujenzi wa mabweni SITA ya wavulana na wanaume, ujenzi wa maabara ya jiografia na fizikia na ujenzi wa uzio.

"Kituo Cha Afya Bwawani kimepata jumla ya milioni 611.125 kwaajili ya kutekeleza miradi nane ya miundombinu ya Afya ambayo ni ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa nje kata za Bwawani na majengo, ujenzi wa jengo la mama na mtoto kata ya mwandeti, na kata ya Lamelock, ujenzi wa maabara kigongoni, ujenzi jengo la upasuaji Namagana na Songambele na ujenzi wa nyumba ya watumishi 3 kwa 1," amesema.

Amesema miradi hiyo imeleta manufaa makubwa kwa jamii ikiwemo kuongezeka kwa miundombinu ya elimu na afya, kuongeza ufanisi wa waalimu kufanyakazi kufuatia kuwepo maeneo ya shule.

Msumi amesema pia faida nyingine ni kuchangia kupata matokeo mazuri ya wanafunzi katika mitihani yao, jamii kupata mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa miradi midogo midogo ya kuwaongezea kipato, huduma za Afya kupatikana kwa Karibu na huduma za maji, umeme kusogezwa Karibu.

Hata hivyo amesema miongoni mwa changamoto walizopata ni pamoja na mfumuko wa bei ambao umesababisha gharama za mradi kuongezeka wakati wa utekelezaji pamoja na wananchi kushindwa kuchangia kulingana na asilimia zinazotakiwa kutokana na kipato kidogo kinachotegemea kilimo.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo, Halmashauri imeendelea kuhamasisha jamii kuchangia zaidi ili kukamilisha miradi sambamba na kushirikisha wadau mbalimbali.

 


Zoezi la Uhawilishaji fedha za walengwa Kaya za mpango katika dirisha la Novemba/Disemba 2023 limefanyika leo tarehe 26 Machi, 2024 Wilaya ya Ngorongoro katika kijiji cha Lopolun ambapo jumla ya Kaya 140 zimenufaika.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Kanali Wilson Sakulo pamoja na mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Mratibu wa TASAF Wilaya Bw. Thomas Nade,  wamefika katika Ofisi ya Kijiji cha Lopolun Kata ya Olorien Magaiduru kushuhudia uendeshaji wa zoezi hilo ukifanyika, huku kiasi cha shilingi 6, 750, 000.00 kikitolewa kwa kaya 140.

Ikumbukwe Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha shilingi 442, 540, 000.00 za kitanzania katika Vijiji 68 wilayani Ngorongoro kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF

Mfuko huu wa TASAF ulianzishwa na Serikali mwaka 2000, ikiwa ni moja ya mbinu za kutokomeza umasikini.





 

1000277802
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mkoani Simiyu, ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao.
1000277803
Sehemu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza na wilayani humo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
1000277804
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega mara baada ya kukagua zahanati iliyotekelezewa na mradi wa TASAF


NA.LUSUNGU HELELA-SIMIYU

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Ridhiwani Kikwete (Mb) amewatahadharisha Watumishi wa Umma kujiepusha na mikopo yenye riba kubwa maarufu kwa jina la " Kausha Damu" huku akisisitiza kuwa mikopo ya aina hiyo imekuwa ikidhalilisha na kutweza utu wa Watumishi katika Jamii.

Mhe.Kikwete ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu wakati akihitimisha ziara yake aliyoianza mapema wiki hii Mkoani Mara.

Amesema mikopo hiyo imewafanya baadhi ya watumishi wa umma kuathirika kisaikolojia na kushindwa kufika katika vituo vya kazi na hivyo kuathiri utoaji wa huduma bora kwa wananchi. 

Amefafanua kuwa mikopo hiyo ambayo huchukuliwa kwenye Taasisi za Kifedha zisizotambulika imekuwa na riba kubwa ambayo huwapelekea Watumishi wengi kushindwa kuwasilisha marejesho na hivyo kupelekea kuuzwa kwa nyumba au vitu vya thamani wanavyo vimiliki.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe.Kikwete amewataka Watumishi kuanza kutumia Mfumo mpya wa kieletroniki wa kukopa (e-loans) ulioanza kutumika kuanzia Septemba 1, 2023 ambao unamuwezesha Mtumishi wa Umma kuomba mkopo pasipo kufika kwenye Taasisi ya Kifedha au Tawi la Benki.

Amesema mfumo huo umeanzishwa na Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora ili kumsaidia Mtumishi wa Umma kupata mikopo katika Taasisi za Kifedha zinazotambulika na Mwajiri ili kumuepusha Mtumishi kukopa sehemu ambazo humpeleka Mtumishi kunyang'anywa kadi ya Benki.

Aidha, Mhe.Kikwete amewataka watumishi hao kujenga nidhamu ya matumizi ya pesa wanazopata kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao ya baadaye baada ya kustaafu.

Amewasihi kujiwekea malengo ya kujiandaa kustaafu kuanzia leo ili wasije kuwa wateja wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Kuendeleza Jamii ( TASAF )

"Hakikisheni hata hela mnazozikopa mnafanya uwekezaji wa kimkakati kwa ajili ya kujitegemea kiuchumi katika siku za mbeleni" amesisitiza Mhe.Kikwete

Katika ziara hiyo Mhe.Kikwete mbali ya kuzungumza na watumishi wa umma katika mikoa ya Mara na Simiyu pia amekagua miradi mbalimbali 

inayotekelezwa na TASAF pamoja na kuzungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ameagiza takwimu za utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) ziakisi kila Wilaya na Halmashauri zake ili kupata tathmini sahihi itakayowezesha kuweka mipango itakayowafikia walengwa kwa usahihi.

Aidha ameelekeza TASAF Mkoa kuongea na Halmashauri ziweze kusaidia kubeba ama kuongeza nguvu ya kutenga asilimia fedha kuwezesha wenye uhitaji.

Akizungumza na wakuu wa idara pamoja na watendaji wa TASAF Mkoani Pwani, Ridhiwani alihimiza taarifa zipatikane na kutolewa kwa hali za wilaya ili kufikia malengo ya mradi.

Alielezea malengo ya Serikali na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona milango inafunguliwa kwa walengwa ,kwa kubadilisha maisha yao kuwatoa kwenye hali ya umaskini.

"Ziwepo taarifa zinazoakisi takwimu sahihi za wenye mahitaji kwa wilaya zote,hizi taarifa za kutoa kimkoa na wilaya moja moja ,tunakuwa hatupati tathmini kwa  usahihi,Hatua hii itasaidia walengwa kujua idadi Yao na kufikiwa ili kutimiza Nia ya Serikali inayoelekeza kuwafikia kaya zenye watu wenye uhitaji ili kuondokana na umaskini na kujijenga kiuchumi kuanzisha miradi "alieleza Ridhiwani.

Ridhiwani alielezea Kuna kila sababu pia ya kuendelea kuwafuatilia walengwa ambao wametolewa ili kujua kama wanaendelea vizuri kwa hali zao za kimaisha na kiuchumi.

"Katika taarifa ya TASAF Mkoani Pwani kulikuwa na walengwa zaidi ya 37,000 na idadi imeshuka kufikia 35,000 ni Lazima hao waliotolewa wafuatiliwe kujua wanaishije unaweza kukuta bado hali ya kiuchumi na maisha yao hairidhishi"

Awali Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta alisema , mpango wa kunusuru kaya maskini unatekelezwa katika Halmashauri tisa zenye vijiji 417, hadi kufikia Juni 2023 kaya zinazonufaika na mpango ni 35,427 idadi hiyo imepungua kutoka kaya 37,663 kwa takwimu za mwaka 2020/2021.

Alieleza idadi hiyo imepungua kutokana na kufariki,kuhama,kufutwa katika mfumo na zingine kuhitimu.

Mchatta alifafanua, kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2023 Jumla ya sh Bilioni 14.239.763.7 zimetolewa kwa walengwa.

Nae mratibu wa TASAF Mkoani Pwani,Roselyn Kimaro aliongeza kusema, fedha hizo zimewasaidia walengwa kuongeza kipato cha kaya na kuwezesha upatikanaji wa chakula, huduma za afya na elimu kwa watoto

Alisema, kaya hizo hupokea ruzuku za Msingi na masharti,nyongeza za ujira kwa walengwa wanaoshiriki utekelezaji wa miradi ya ajira za muda (PWP) pamoja na usaidizi wa watu wenye ulemavu

Roselyn alielezea, ipo miradi mbalimbali ambayo wametekeleza kupitia TASAF ikiwemo soko la kisasa Utete,Mochwari Chalinze, Zahanati ya Mwanalugali ambayo ipo hatua ya umaliziaji, Nyumba mbili za watumishi katika Zahanati Vikawe,ufadhili kwa watu wenye ulemavu,sekta ya elimu  na miradi ya muda ambapo wananchi wamenufaika kwa kupata ujira.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.

Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Mohammed Moyo akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa yake, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Mohammed Moyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.


Mtumishi wa Iringa Manispaa, Bi. Jamila Mwindi, akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.


Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Philemon Mmbaga (Wakwanza kulia) akichukua taarifa za mtumishi aliyewasilisha changamoto yake wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi aliyoifanya katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.


Na. Veronica E. Mwafisi-Iringa

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameutaka uongozi wa Manispaa ya Iringa kuzingatia mahitaji na maslahi ya watumishi ili kuwajengea ari na morali ya utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa viongozi wa Manispaa ya Iringa, wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi hao.

Mimi naomba sana viongozi mbadilike katika suala zima la kusimamia rasilimaliwatu, tuzingatie maslahi na mahitaji ya watumishi wetu ili kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii, weledi na morali ya hali ya juu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka wakuu wa idara katika Manispaa ya Iringa kuwa na utaratibu wa vikao vya mara kwa mara na watumishi wanaowasimamia ili kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa wakati.

“Si jukumu la Mkurugenzi au Afisa Utumishi pekee kuzungumza na watumishi, wakuu wa idara mnawajibu wa kuwa na vikao vya kuzisikiliza kero na changamoto zinazowakabili watumishi mnaowaongoza ili kuzitatua,” Mhe. Ndejembi amehimiza.

Kuhusiana na wingi wa malalamiko kutoka kwa watumishi, Mhe. Ndejembi amesema, uongozi wa Manispaa ya Iringa unapaswa kufanya tathmini ya hali ya utendaji kazi kwani idadi kubwa ya watumishi imewasilisha malalamiko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Mohammed Moyo amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kutenga muda wa kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi katika wilaya yake ikiwa ni pamoja na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amehitimisha ziara ya kikazi Mkoani Iringa iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.


Waziri Jenister Mhagama katika moja ya hafla ya kuhamasisha matumizi ya Lishe bora kwa watoto

Lishe ina uhusiano na afya ya akili_ hivyo mtoto anahitaji lishe kamili ili kuwa na afya njema pamoja na akili timamu.

Watoto wadogo wanapata lishe bora kwa kula milo iliyo kwenye makundi yote matano ya vyakula kama inavyoonekana katika picha hii. 

Na Abby Nkungu, Singida 

ASILIMIA 97 ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili mkoani Singida hawapati mlo kamili unaokubalika na waatalamu wa lishe bora, hali inayochangia kupata changamoto mbalimbali za kiafya; ikiwemo udumavu, ukondefu na uzito mdogo.

Taarifa ya Utafiti wa Kitaifa wa Lishe (TNNS) uliofanyika mwaka  2018, inaonesha kuwa ni asilimia tatu tu (3%) ya watoto wenye umri wa chini ya miaka miwili mkoani Singida ndio wanaopata mlo unaokubalika kilishe.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Victorina Ludovick ilieleza kuwa lishe duni ni moja  ya sababu zinazochangia kuendelea kuwepo kwa tatizo la udumavu mkoani humo kwa asilimia 29.8, ukondefu asilimia 4.7 na uzito pungufu asilimia  14 kwa watoto walio chini ya miaka mitano.

Hata hivyo, alisema kuwa pamoja na hali kuwa bado sio ya kuridhisha, matatizo hayo yamepungua ikilinganishwa na miaka minne kabla ya kutafiti huo (yaani 2014) ambapo  udumavu ulikuwa asilimia 34, ukondefu asilimia 5 na  uzito mdogo asilimia 15.

“Maendeleo sio mabaya. Hii Programu Jumuishi ya Taifa ya miaka mitano juu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto itasaidia kuleta matokeo chanya zaidi katika suala la lishe kwani inahusisha masuala mtambuka” alisema na kuongeza kuwa ni suala la muda tu kumaliza changamoto hiyo.

Alieleza kuwa chini ya Programu hiyo, wadau wamekuwa wakiunganisha nguvu kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kuimarisha ulinzi kwa watoto wenye umri chini ya miaka minane, afya, lishe, elimu na masuala mengine mtambuka kwa kundi hilo muhimu katika jamii.

Alisema kuwa, pamoja na wadau wengine kutimiza vyema wajibu wao kupitia Programu Jumuishi ya Taifa, Serikali nayo imeongeza bajeti ya lishe kwa mtoto kwa kila  halmashauri kutoka 1,000/- kwa mwaka wa fedha 2020/21 hadi 1,239/- kwa mwaka 2021/2022.

Wataalamu wa afya ya Mama na Mtoto wanasema kuwa pamoja na udumavu, ukondefu na uzito pungufu, suala la lishe duni ni miongoni mwa sababu za homa za mara kwa mara kwa mtoto.

“Lishe duni ni chanzo mojawapo cha magonjwa na vifo kwa watoto wadogo; hasa walio chini ya miaka mitano. Pia hudumaza ukuaji wa kimwili na kiakili" alisema Dk Suleiman Muttani, Daktari Bingwa Mshauri wa magonjwa ya wanawake na watoto hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida.

"Kama hiyo haitoshi, lishe duni pia hupunguza uwezo wa mtoto kufanya vizuri awapo shuleni na ufanisi wa kazi katika maisha yake ya utu uzima hapo baadae" aliongeza Dk Muttani.

Wazazi, walezi na wataalamu kutoka Mashirika, Asasi na Taasisi zinazoshughulikia ustawi wa mtoto, wanasema njia pekee ni kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa lishe bora kwa mtoto  ndani ya siku 1,000 za awali ili kujenga afya bora.

“Unaweza kushangaa tatizo kubwa la lishe duni kwa watoto lipo vijijini kuliko mjini wakati huko ndiko vyakula vingi vya asili na vyenye virutubisho vinapatikana. Kwa hiyo, shida ni elimu kwa jamii” Mama Amina Ali wa Kibaoni Singida mjini alisema.

Ofisa Maendeleo ya Jamii mstaafu na Mtafiti wa masuala ya mila na desturi za Wanyaturu, Patrick Mdachi alisema imani potofu miongoni mwa jamii; hasa vijijini juu ya ulaji wa baadhi ya vyakula muhimu vinavyoshauriwa na wataalamu wa afya ili kujenga mwili wa mjamzito na mtoto, ni kikwazo kingine.

“Huwezi kuamini ila jaribu kutoka nje kidogo ya mji.  Kuna wajawazito na watoto hawali mayai, maini,  firigisi na vyakula vingine vingi muhimu eti kwa kukatazwa na Wazee wa kiume. Hii inaturudisha nyuma sana” alieleza Mdachi na kutaka wadau kushirikiana na Viongozi wa dini, Wazee wenye uelewa na wataalamu wa afya kukemea mila hizo potofu. 

 


Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma

Tarehe 25 Septemba, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na

Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Kamati ya Taifa ya

Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuwa na utamaduni wa

kuwatembelea walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini,

unaoratibiwa na TASAF ili kubaini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto

zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mpango huo ambao Serikali

inautekeleza kwa lengo la kuboresha maisha ya kaya maskini nchini.

Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma, wakati akizindua

Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF iliyoteuliwa hivi karibuni mara baada

ya kamati iliyopita kumaliza muda wake kiutendaji.

Waziri Jenista amewahimiza wajumbe wa kamati hiyo, kuhakikisha

wanakwenda kuzungumza na viongozi, waratibu na walengwa katika

maeneo yote ambayo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa,

ili kufikia lengo la Serikali la kuzikwamua kaya maskini kutoka katika lindi la

umaskini.

“Mhe. Mwenyekiti na wajumbe wa kamati hii, tembeleeni maeneo ambayo

mpango wa TASAF unatekelezwa ili mjiridhishe namna ambavyo

unawafikia walengwa na kuwanufaisha,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, wajumbe wa kamati wakitembelea maeneo

ambayo mpango wa TASAF unatekelezwa, watapata fursa ya kujionea

namna walengwa walivyonufaika, ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto

ambazo walengwa hao wa TASAF wanakabiliana nazo.

Akizungumzia azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuzikwamua kaya

maskini, Mhe. Jenista amesema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

haitomuacha mtu nyuma katika kufikia malengo ya maendeleo kama

yalivyoainishwa katika dira ya maendeleo (Vision 2025), na ndio maana


imejipanga vema katika kuhakikisha inaboresha maisha ya kaya zote

maskini kwenye vijiji, mitaa na shehia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Peter Ilomo

amemhakikishia, Mhe. Jenista kuwa yeye pamoja na kamati yake

watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo ameyatoa ili kutimiza lengo la

serikali la kuboresha maisha ya kaya maskini.

Naye, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Dkt. Moses Kusiluka amesema,

ataendelea kushirikiana na TASAF ili kuhakikisha inatimiza lengo lake la

kuboresha maisha ya wananchi ambao wanaishi katika familia zenye hali

duni kiuchumi.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake,

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amesema,

TASAF imekuwa na mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya kaya

maskini ikiwa ni pamoja na kujenga rasilimaliwatu ya kutosha kwa

kuwawezesha kielimu wanafunzi wanaotoka kwenye kaya maskini kutoka

hatua moja kwenda nyingine.

“Mwaka jana, TASAF kwa kushirikiana na bodi ya mikopo tumewawezesha

wanafunzi 1200 kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali

nchini, na mwaka huu mchakato bado unaendelea lakini tunatarajia

kuwawezesha wengi zaidi kwani walioomba wako zaidi ya 3000,” Bw.

Mwamanga amefafanua.

Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

kwa sasa inaundwa na Mwenyekiti Bw. Peter Ilomo, pamoja na wajumbe

wengine ambao ni Balozi Zuhura Bundala, Bw. Richard Shilamba, Dkt.

Charles Mwamwaja, Dkt. Ruth Lugwisha, Dkt. Naftali Ng’ondi, Bw. Ali

Salim Matta, Mhandisi Rogatus Mativila na Dkt. Grace Magembe.


Walengwa wa TASAF na wananchi wa Kijiji cha Bukulu wilayani Kondoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani humo.

Na James K. Mwanamyoto-Kondoa

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ametoa siku moja kwa Mtendaji wa Kijiji cha Bukulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha mlengwa wa TASAF kijijini humo, Bw. Laurent Chebu anapewa ruzuku yake na kumpatia taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo.

Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na walengwa wa TASAF na wananchi wa Kijiji cha Bukulu wilayani Kondoa akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo.

Mhe. Jenista amesema akiwa katika ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya TASAF hupenda kusikiliza shuhuda za walengwa pamoja na changamoto zinazowakabili, hivyo baada ya kusikia changamoto ya Bw. Laurent Chibu kutopata ruzuku ameamua kutoa maelekezo kwa Mtendaji wa Kijiji ili mlengwa huyo apate haki yake.

“Mtendaji nimekuuliza hapa na umekiri kwamba Bw. Laurent Kibu hajapata ruzuku yake kwasababu yeye na mwenzeke walikuwa safarini, hivyo nikupa muda wa kushughulikia suala hili mpaka kesho jioni na unipigie simu wewe mwenyewe kunieleza kuwa mlengwa huyu ameshapewa na wengine ambao bado wapewe ruzuku zao”, Mhe. Jenista amesisitiza.

Waziri Jenista amewataka watendaji na waratibu wa TASAF kote nchini kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya walengwa wa TASAF zinawafikia walengwa kwa wakati, kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ilivyokusudia.

Katika kuhakikisha ruzuku inawafikia walengwa kwa wakati, Mhe. Jenista amewataka walengwa wa TASAF kujisajili kwenye mfumo wa kidigitali wa simu ili waweze kuhawilishiwa ruzuku zao kupitia mitandao ya simu, na hatimaye kuondokana na changamoto ya kutopokea ruzuku zao kwa wakati.

“Watendaji na waratibu wa TASAF nisingependa kusikia mlengwa wa TASAF hajapewa ruzuku yake, iwe kwasababu ya kutokuwepo wakati wa dirisha au sababu nyingine yoyote ile kwani lengo la TASAF ni kuwawezesha walengwa kuboresha maisha yao”, Mhe. Jenista amefafanua.

Akieleza namna TASAF ilivyoboresha maisha yake, mlengwa wa TASAF wa Kijiji cha Bukulu, Bi. Rukia Kasi amesema ruzuku aliyoipata imemuwezesha kununua mbuzi na kuku wa kufuga, kusomesha watoto pamoja na kukarabati nyumba anayoishi na mme wake ambaye ni mlemavu wa macho.

Mlengwa mwingine wa TASAF wa Kijiji cha Bukulu, Bi. Mwanaidi Dohu amesema kuwa TASAF imemuwezesha kununua ng’ombe, kujenga nyumba ya kuishi, kuchimba kisima cha maji na kujishughulisha na kilimo cha migomba.

Naye, Bw. Abdilahi Ally ambaye ni mlengwa wa TASAF Kijiji cha Bukulu amesema licha ya ulemavu wake TASAF imemuwezesha kusomesha watoto wanne waliohitimu kidato cha nne na mmoja amemaliza kidato cha sita hivyo anaishukuru Serikali kupitia TASAF kwa kumuwezesha kumudu gharama za kuwasomesha watoto wake.

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika mwaka wa fedha 2021/2022 imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.6 katika Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini wilayani humo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na walengwa wa TASAF na wananchi wa Kijiji cha Bukulu wilayani Kondoa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Hamis Mkanachi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na walengwa wa TASAF na wananchi wa Kijiji cha Bukulu wilayani humo wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani humo.
Mlengwa wa TASAF Kijiji cha Bukulu, Bw. Laurent Chebu akiwasilisha hoja yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na walengwa wa TASAF na wananchi wa Kijiji cha Bukulu wilayani Kondoa wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani humo.

 Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwahakikishia wadau wa maendeleo kutoka Swideni wanaoshughulikia miradi ya TASAF kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha miradi inayotekelezwa inazingatia Thamani halisi ya Pesa inayotumika.
Mhe. Hemed akipata maelezo kutoka Bibi Annie Stomnge kutoka Swiden juu ya azma yao ya kufanya ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya TASAF inayotekelezwa Zanzibar.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa miradi ya Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuwainua wananchi kiuchumi na kujiongezea kipato.

Mhe. Hemed alieleza hayo wakati akizungumza na wadau wa maendeleo wanaoshughulikia masuala ya TASAF kutoka Swiden waliofika Afisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Alisema serikali inangalia uwezekano wa kuengeza nguvu katika sekta mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kupitia miradi ya TASAF.

Alibainisha kwamba ujio wa ugeni huo utapata fursa ya kutosha ya kutembelea miradi mbali mbali iliotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na viongozi wanaosimamia TASAF Zanzibar.

Alisema kitendo cha ugeni huo kwenda kujionea wenyewe katika maeneo yaliotekelezwa miradi hio kutathibitisha jinsi gani Zanzibar ilivyojipanga kuinua hali za maisha za wananchi wake.

Alisema miongoni mwa sekta watakazozitembelea ni pamoja na sekta ya Afya na Elimu ili kuona kwa jinsi gani miradi iliotekelezwa imesaidia jamii sambamba na kushauriana juu ya namba bora ya kuweka vipau mbele kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mengine.

Akizungumzia kuhusiana na Changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo Makamu wa Pili wa Rais alisema tayari Ofisi yake imeshatoa maelekezo kwa watendaji wanaosimamia TASAF na baadhi ya changamoto zimeanza kupatiwa ufumbuzi.

Mhe. Hemed alieleza kuwa serikali ya awamu ya nane itahakikisha inasimamia kwa karibu katika kuhakikisha thamani ya pesa inayotumika inaendana na miradi halisi inayotekelezwa.

Nae, mdau wa maendeleo kutoka Swideni Bibi Annie Stomnge alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa katika ziara yao hiyo watatembelea pia katika maeneo yanayotumiwa kufanyika malipo kwa walengwa wa miradi sambamba na kupata maoni kutoka kwa walengwa wa miradi hiyo.