Mgombea ubunge wa Jimbo la Same Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mathayo David maarufu kama Mwana wa Kaya, ameweka wazi kuwa uchaguzi wa Oktoba si wa majaribio, bali ni wa kuchagua kasi, utekelezaji na maendeleo.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni uliojaa shamrashamra, zilizofanyika katika katika kata ya Hedaru,Dkt. Mathayo alitoa wito mzito kwa wananchi wa Same Magharibi kuhakikisha wanawachagua viongozi wa CCM – kuanzia kwa Rais Samia Suluhu Hassan, yeye mwenyewe kama mbunge, hadi kwa madiwani – akisema viongozi hao “wanatekeleza wanachoahidi.”

“Miaka mitano iliyopita tumefanya kazi. Sasa tunakuja kuhitaji nafasi ya kuendelea – kazi ya maendeleo ya kweli,” alisema kwa msisitizo.

Wananchi Wapaza Sauti: “Tunaiona kazi ya Mama Samia!”

Katika hali iliyojaza hamasa, wananchi wa Same Magharibi walitumia jukwaa hilo kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa kiwango cha juu asilimia 100, wakisema kazi imeonekana katika kila kijiji, kata na kata ndogo.

“Mama Samia ametupa maji, afya, shule, barabara, umeme… hatuna cha kulalamika. Sasa tunaomba aendelee pamoja na Dkt. Mathayo ambaye kazi yake tunaijua,” alisema mama mmoja kutoka Kata ya Bwambo huku akishangiliwa na umati.

Aidha, wananchi walishukuru Kamati Kuu ya CCM kwa uamuzi wake wa kurejesha jina la Dkt. Mathayo David kuwa mgombea wa CCM katika jimbo hilo, wakieleza kuwa ni kiongozi mchapakazi, mnyenyekevu na mwenye kuelewa vipaumbele vya wananchi wake.

“Tunawashukuru sana Kamati Kuu. Mmetusikiliza. Tumempata mtu wetu – Mwana wa Kaya. Tunaamini atatufikisha mbali zaidi,” alisema kijana mmoja aliyeshiriki mkutano huo kwa hisia kali.

Ahadi Kubwa: Afya Bila Malipo, Mochwari Bila Deni

Katika kile kinachoonekana kama ahadi yenye uzito wa kihistoria, Dkt. Mathayo alitangaza mpango wa huduma za afya kwa wote, akisema:

“Tunaposema afya bora kwa wote, tunamaanisha kweli. Hata motuary itakuwa bure – hakuna mzazi atakayeambiwa hawezi kumzika mpendwa wake kwa sababu ya deni.”

Kupitia mpango huu mpya, unaotarajiwa kuzinduliwa ndani ya siku 100 za kwanza za uongozi wa Rais Samia iwapo atachaguliwa tena, serikali inalenga:

Huduma za bima ya afya kwa wote

Matibabu bure kwa wazee, wajawazito, watoto na watu wenye ulemavu

Mochwari bure, kwa heshima ya wafu na familia zao

Kazi Iliyoonekana: Maji, Miundombinu, Elimu na Umeme

Katika tathmini ya mafanikio ya miaka mitano, Dkt. Mathayo alieleza hatua zilizopigwa:

✅ Zahanati na vituo vya afya vyenye vifaa na watumishi

✅ Visima na mtandao wa maji vijijini

✅ Madarasa, mabweni na nyumba za walimu

✅ Barabara na miundombinu bora ya kijamii

✅ Usambazaji wa umeme vijijini unaoendelea

Mpango wa awamu ijayo unalenga kukamilisha kilichobaki – kuhakikisha kila kijiji kinapata huduma zote za msingi.

“Kila kijiji, kila kata – tunaleta maendeleo,” alisema Dkt. Mathayo, huku akipigiwa makofi na umati wa wananchi waliokuwa wakiimba: “Kazi iendelee!”

Ilani 2020 Yatekelezwa – Sasa Ni Wakati wa Hatua Zaidi

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Same Abdilah Suleiman alieleza kuwa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 imetekelezwa kwa mafanikio, na sasa chama kiko tayari kusukuma mbele ajenda ya maendeleo.

“Leo tunamkabidhi Dkt. Mathayo zana za utekelezaji – kwa sababu kazi imeonekana,” alisisitiza.

Wito wa Mwisho: “Samia, Mathayo, Madiwani – CCM Tena!”

Akihitimisha mkutano huo, Dkt. Mathayo aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu na kufanya uamuzi wa maendeleo:

“Tunaomba tena mtuchague – Mama Samia, Mathayo na madiwani wa CCM – kwa sababu mnatujua. Tukiahidi, tunatekeleza.





Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: