Na Elizabeth Joseph, Monduli.

Wakristo wilayani Monduli wametakiwa kuishi kwa Upendo kama mafundisho ya Dini yanavyowataka ili kuepusha vitendo vya Ukatili hasa kwa watoto.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 31 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh,Gloriana Kimath wakati akisalimia waumini waumimi katika Ibada ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Jengo la Kanisa Anglikana (St.Peter's) Dayosisi ya Mount Kilimanjaro ambapo Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro Dkt Stanley Hotay.

Alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la vitendo mbalimbali vya Ukatili hasa kwa watoto jambo alisema kwa kiasi kikubwa linachangiwa na kukosekana kwa upendo katika jamii zinazowazunguka.

"Mafundisho ya Dini yanatufundisha juu ya upendo lakini kwasasa wengi wetu hatuuishi huo upendo tunaoelekezwa kwenye vitabu vya Dini,Mfano Wakina Mama tunaishi kwa kuwanyanyasa hawa Wasaidizi wetu wa kazi majumbani yaani hatuwaoneshi upendo wakati wao ndio wanatupikia,wanalea watoto wetu tukiwa na bize na kazi zetu na kufanya shughuli nyingine majumbani mwetu lakini tunawalipa mabaya badala ya kuwapenda.

"Jambo hili linawafanya na wao kuhamisha hasira  na chuki zao kwa watoto wetu kwa kuwafanyia vitendo vya kikatili,niwaombe sote tubadilike, tupendane ili tuweze kutokomeza vitendo hivi kwenye jamii zetu maana palipo na upendo hakutakuwa na chuki. "alifafanua Mh,Kimath.

Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais na Viongozi wengine Mh,Kimathi aliwaomba waumini hao kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh,Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine ikiwa ni pamoja na kuliombea Taifa la Tanzania katika mchakato huo ili amani iendelee kutawala nchini.

Naye Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro Dkt Stanley Hotay katika mahubiri yake aliwaomba waumini hao kuhakikisha wanadumisha Amani ya Nchi na kwakuwa ndio kipaumbele kikubwa katika maisha ya kila mmoja.

"Usiombe kukosa Amani maana hata uwe na mali kiasi gani hilo Gari,Nyumba na pesa ulizonazo hazitakuwa na faida kwenye maisha yako kwakuwa utaishi maisha ambayo hutajua usalama wa maisha yako kwa saa zijazo utakuwa wapi,utatamani kwenda mjini ama mahali pengine lakini hutakuwa na uhakika wa kurudi salama hivyo ni muhimu kulinda  na kuombea sana Amani yetu "Alisisitiza Dkt Hotay.

Share To:

Post A Comment: