Articles by "ARUSHA"
Showing posts with label ARUSHA. Show all posts

 


Na WAF, Arusha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, ametoa wito kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ushauri na maelekezo ya wataalam wa afya na malezi ili kuwalea watoto, kwa kuweka mkazo maalum wa lishe bora, malezi yenye upendo na mazingira salama kwa ajili ya ustawi wao, kwakuwa watoto ni hazina ya taifa la kesho.

Dkt. Shekalaghe ametoa wito huo Julai 23, 2025, mkoani Arusha, wakati  akifungua Kongamano la pili la Kitaifa la Afya na Ustawi wa Watoto, ambapo amesisitiza kuwa taifa haliwezi kuwa na viongozi bora wa baadaye ikiwa jamii haitawalea watoto kwenye misingi imara ya afya, elimu na maadili.

“Watoto wasipo pata malezi vizuri, wakakosa lishe bora, mazingira salama na malezi yanayojali maendeleo yao ya kimwili na kiakili, hatuwezi kuwa na viongozi bora wa kesho, rai yangu ni muhimu jamii kutambua na malezi bora hujengwa kwa kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya na wataalam wa malezi,” amesema Dkt. Shekalaghe.

Ameongeza kuwa familia zinapaswa kuzingatia kila nyanja ya afya ya mtoto kuanzia mlo anaopata, mazungumzo ya kila siku, michezo anayoshiriki, hadi mazingira anayoishi. 

“Afya siyo tu kukosekana kwa ugonjwa, bali ni hali njema kimwili, kiakili, kijamii na kiutamaduni. Kwa hiyo, tuwalee watoto wetu kwa njia sahihi ili wajenge taifa lenye msingi thabiti,” amesisitiza.

Dkt. Shekalaghe pia amewahimiza wataalam na watoa huduma za afya nchini, hususan wale wanaohudumia watoto, kulenga zaidi kuzuia vifo na kujikita pia kwenye kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora na malezi chanya kwa watoto.

Kwa upande wake, Rais Mteule wa Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania, Dkt. Theopista Jacob, amesema kuwa, licha ya uwekezaji mkubwa na juhudi za Serikali za kuhakikisha watoto wanapata huduma za chanjo, bado ipo haja ya Idara ya Huduma za Chanjo (IVD) kushirikiana kwa karibu na watumishi wa afya ili kila mtoa huduma awe na uelewa sahihi na anasaidia kupata taarifa kwa wakati kuhusu watoto wanaopata magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kufanikisha juhudi za kudhibiti na kuzuia magonjwa yanayoweza kutokomezwa kwa njia ya chanjo.











Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stagomena Tax amewataka wanawake kuzitendea haki nafasi mbalimbali wanazozipata, akizitaka asasi za kiraia kutoa fursa sawa katika utendaji.

Dkt. Stagomena ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa kongamano la wanawake Kanda ya Kaskazini linaloendelea Jijini Arusha kuelekea siku ya wanawake duniani ambapo kitaifa yatafanyika Machi 08, 2025 ambapo mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya michezo vya sheikh Amri Abeid.

Waziri Tax pia ametoa wito kwa sekta binafsi kutoa fursa za hadhi na mazingira salama kazini kwa wanawake kwenye sekta ya utalii nchini, akihimiza pia jamii kupambana na ukatili wa kijinsia ambao mara nyingi umekuwa ukirudisha na kuwaacha nyuma wanawake kwenye maendeleo.

Waziri Stagomena kadhalika amehimiza wanawake kujiongeza na kutumia fursa mbalimbali zinazotengenezwa na serikali, akihimiza ushirikiano kati ya wanaume na wanawake katika nyanja zote, kwa kiwango sawa na malengo bora katika kufikia maendeleo ya wote.

Kwa upande wake Naibu waziri wa wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia na makundi maalum, Mwanaidi Ally Khamisi amesema kupitia kampeni ya Royal Tour, kumekuwepo na ongezeko la watalii, ukuaji wa pato la taifa na pato la mmoja mmoja.

"Wizara imeratibu kongamano hili ili kuhakikisha kila mshiriki anapata fursa sawa, na kwamba wanawake sasa wanatambua nguvu zao – ndiyo maana wanaongoza katika nyanja mbalimbali." Aliongezea

Hata hivyo Katibu Mkuu wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na makundi maalum Dkt John Jingu amesema maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu 2025 yamepambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo makongamano ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Sambamba na hayo Jackline Mafuru ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wenye Makampuni ya Utalii Tanzania, ameonesha furaha yake kwa ukuaji wa sekta ya utalii ambayo imewajumuisha wanawake madereva, wapokezi, na hata waongozaji watalii, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa. Wajasiriamali walioshiriki kongamano hili wamesisitiza kuwa fursa hizo zinawafikia moja kwa moja, zikiwapa hamasa zaidi ya kupiga hatua mbele.



 Wananchi Jijini Arusha wamevutiwa na bidhaa mbalimbali za Nishati Safi ya Kupikia na wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kufikisha bidhaa hizo katika Maonesho yanayoendelea mkoani humo kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti Machi 6, 2025 mara baada ya kutembelea Banda la REA na kushuhudia teknolojia mbalimbali za majiko ya Nishati Safi ya Kupikia; wananchi hao wamepongeza uwepo wa teknolojia hiyo ambayo wamesema licha ya kulinda mazingira lakini pia inarahisisha suala zima la kupika na hivyo kurahisisha maisha.

"Tumefurahi kuona majiko yaliyoboreshwa, teknolojia iliyotumika ni nzuri, majiko haya tumeyapenda," amesema Ester Mwasigo mkazi wa Dodoma ambaye yupo Jijini humo kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kimataifa 2025.

Mwasigo alitoa wito kwa wananchi kutembea banda la REA ili kujifunza na kuchangamkia bidhaa hizo za Nishati Safi ikiwa ni hatua moja wapo ya kuunga mkono jitihada na dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Tunatumia gharama kubwa kununua mkaa huu wa kawaida; mimi ni balozi wa teknolojia hii; Serikali imefanya jambo kubwa muhimu ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kama hivi," amesema.

Akizungumzia kwa ujumla mwenendo wa kuhama kutoka kwenye utamaduni wa zamani kwenda kwenye utamaduni mpya wa Nishati Safi ya Kupikia, Mwajuma Tarek Mkazi wa Muriet Jijini Arusha alisema kwa kampeni inayoendelea kutolewa dhamira ya Serikali itafikiwa kikamilifu hasa ikizingatiwa kila mwanamke amehamasika.




 Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wametakiwa kusimamia kikamilifu suala la lishe katika maeneo yao ili kuwa na Taifa lenye watu wenye afya bora pamoja na utimamu wa akili.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Dadi Kolimba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda katika kikao cha tathmini ya lishe Mkoa wa Arusha.

Kolimba amesema kuwa agenda ya Mheshiwa Rais ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na afya njema ili kuweza kusaidia kuwa na Taifa lenye watu waliosalama kiafya .

"Mheshiwa Rais ameingia mkataba na wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na wakurugenzi ambapo imeenda mpaka kwa watendaji wa kata kwasababu ya usalama wa nchi yetu kuanzia usalama wa mama na mtoto kabla na baada ya kuzaliwa"Alisema

Aidha amewaeleza wadau hao wa lishe kuangalia afua za lishe kila wilaya kuona kama zinatekelezwa ili kuwa na tija.

Kwa upande wake Afisa lishe Mkoa Dotto Mirembe anasema kuwa taarifa ya utekelezaji ya viashiria vinavyosimamiwa na mkataba kwa kipindi cha July hadi Desemba 2024 hadi 2025 ambapo mkoa umeweza kutenga bajeti ya afua za lishe ambapo Mkoa umetenga kiasi cha shilingi Milioni 947 ambapo ni sawa na shilingi 2490.4 kwa kila mtoto.

Dotto amesema tathmini ya lishe kwenye ngazi ya kata Mkoa wa Arusha wanafanya vizuri kwa kuwa mpaka sasa wameweza kuvuka lengo la Taifa katika suala la lishe.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Charles Mkombachepa kwa niaba ya Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Mussa Misaile amepongeza Afua za lishe kwa kuendelea kufanya vizuri na kuwataka kutobweteka na kuendelea kushika nafasi nzuri katika masuala ya lishe kimkoa.





 


Na, Egidia Vedasto Arusha. 

Wanawake Jijini Arusha wamenufaika na mafunzo ya uongozi wa mabadiliko kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wanawake (UN Women) kwa ushirikiano na Serikali ya Finland ili waweze kuleta mabadiliko chanya katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii. 

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN Women) Hodan Addou amezungumzia masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wananwake katika masuala mbalimbali ikiwemo uchumi na siasa. 

Amesema kuwa (UN Women) imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa wananwake wanapata nafasi sawa katika sekta zote za maendeleo na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana katika mipango ya maendeleo jumuishi inayozingatia mahitaji ya wanawake vijijini na wale walioko mazingira magumu. 

"Uwezeshaji wa wananwake si tu suala la haki za binadamu bali ni msingi wa maendeleo endelevu, na tunafurahi kuona Mkoa wa Arusha ukichukua hatua madhubuti katika kusimamia usawa wa kijinsia" ameeleza Addou. 

Kwa upande wake Muwezeshaji wa mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam  Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Prof. Bernadetha Killian amesema mafunzo hayo  yanawalenga wanawake viongozi ngazi za serikali za mitaa, (TAMISEMI) Madiwani waliochaguliwa na wale viti maalum, wenyeviti serikali za mitaa, wenyeviti serikali vijiji na wenyeviti majukwaa mbalimbali. 

Vilevile amewasisitiza wanawake waliopata mafunzo  kuhudhuria mafunzo hayo kwa siku zote zilizopangwa, kujiamini na kutunza vitabu vya kumbukumbu. 

"Mradi huu ni wa mwaka mmoja, umeanza Oktoba 2024 na utakamilika Septemba 2025 kwa ufadhili wa (Un Women) kwa ushirikiano wa Serikali za mitaa na mkoa kupitia kwa Maafisa maendeleo ya jamii lwa ajili ya kutafuta  walengwa stahiki, nno furaha yetu kwamba tumefanikisha hilo" amebainisha Prof. Bernadetha. 

Hata hivyo mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo na mwenyekiti wa jukwaa la wanawake kata ya Muriet Miriam Mbise amewataka wanawake kuacha woga katika masuala ya siasa na uchumi bali wathubutu kupaza sauti  ili kupigania haki na kutimiza ndoto zao. 

"Wananwake wa Kaskazini tuache woga, tujione tunafaa maana sisi ni viongozi kuanzia katika ngazi za familia zetu, tena tuwaze kugombea nafasi za juu" amesema Miriam. 

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Lake Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 406.7 wa kusambaza majiko ya gesi 19,530 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% katika maeneo ya vijijini ndani ya Wilaya ya Arusha, Karatu, Longido, Meru, Monduli na Ngorongoro Mkoani Arusha.


Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya amebainisha hayo Desemba 6, 2024 Mkoani Arusha wakati wa kumtambulisha mtoa huduma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

"Tumeanza utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao unasisitiza miaka 10 kutoka sasa 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, na hili linaweza kufikiwa kupitia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo hii ya usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku," alisema Mhandisi Yesaya.

Alifafanua kuwa REA imeandaa programu mbalimbali ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali ambayo imeasisiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya za wananchi wake sambamba na kuhifadhi mazingira kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za Nishati Safi ya kupikia ili kupunguza ukataji miti ambapo alibainisha kuwa takribani hekta 400,000 hukatwa kila mwaka.

"Mradi huu unakwenda kusaidia kuondokana na athari za kiafya, pia utasaidia kuepuka vitendo vya kikatili, kulinda vyanzo vya maji na kutunza Mazingira na pia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi," alifafanua Mhandisi Yesaya.

Aidha, alisema kuwa mradi huo vilevile ni nyenzo muhimu ya kupunguza umaskini miongoni mwa jamii za maeneo ya vijijini kwani utatoa fursa kwa akina mama kujikita katika shughuli za uzalishaji mali pindi wanapotumia mitungi ya gesi kama njia mbadala ya kupikia sababu inaokoa muda ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Musa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango huo ambao amesema unakwenda kusaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kumudu gharama ya manunuzi ya majiko hayo ya gesi.

"Tunashukuru kwa mawazo haya ya Mhe. Rais na kwa kazi inayofanywa na REA. Ninaamini kwa ruzuku hii iliyowekwa na Serikali, Watanzania walio wengi wataweza kumudu gharama na hii itafanikisha lengo la 80% ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034," alisema.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya Lake Gas, Kanda ya Kaskazini, Ismail Juma alithibitisha kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha wanufaika wa majiko hayo wanafikiwa kikamilifu na alitoa wito kwa wananchi mkoani humo kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Serikali kupitia REA.

Alitoa rai kwa wananchi kutumiza masharti ya kupata majiko hayo ya ruzuku ikiwa ni pamoja na kuwa na kitambulisho cha Taifa cha NIDA ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa kila mwananchi.

Wakala wa Nishati Vijijini unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.





 


Na Magesa Magesa,Arusha

WATAALAMU wa ununuzi na hapa nchini wametakiwa kuwa wazalendo na kuzingatia maadili,weledi,kanuni na taratibu katika kutekeleza majukumu yao .

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Missaile Musa ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua mafunzo kwa wataalamu wa manunuzi yanayoendelea mjini hapa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi(PSPTB)na kushirikisha wataalamu wa sekta hiyo toka halmashauri zote na sekretarieti ya mkoa wa Arusha.

Musa amewataka kujiepusha na vitendo vya rushwa na kujikita zaidi katika kusimamia kikamilifu fedha zote za umma   zinazotengwa kwa ajili ya  miradi mbalimbali.

“hakikisheni mnajifunza   kwa umakini mkubwa kuandaa na kutunza mikataba,na mzingatie yaleyote mnayofunzishwa hapa ili mkitoka muende mkayatekeleze kwa vitedo”alisisitiza katibu Tawala huyo wa Mkoa.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi hapa nchini(PSPTB)Godfred Mbanyi alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu hao juu ya sheria mpya ya ununuzi na namna ya kusimamia mikataba.

Alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika maeneo mengi hapa nchini ni wataalamu wa ununuzi kufanya kazi pasipo kusajiliwa na bodi hyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria na kuwataka wale wote ambao hawajasajiliwa wajisajili mara moja.

“Natoa wito kuzingatia sheria kanuni na taratibu za manunuzi katika kutekeleza majukumu yenu,na nawataka wale wote ambao hawajasajiliwa na bodi kujisajili haraka iwezekanavyo kwani iko kwa mujibu wa sheria na anayefanya kazi bila kusajiliwa anavunja sheria za nchi”alisema Mbanyi

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo,Catherine Mwamasage ambaye ni Mkuu wa kitengo cha manunuzi kutoka TANAPA,aliipongeza PSPTB kwa kuwapatia mafunzo hayo na kusema kuwa yatawasaidia kupata maarifa zaidi na wataenda kuyafanyia kazi kwa vitendo.

 


Na Elinipa Lupembe 


Jumla ya wanafunzi 29,508 mkoa wa Arusha, wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2024, unaoanza Novemba 11 - 29, 2024 nchini,  kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania. 

Akitoa taarifa ya kufanyika mtihani huo, Afisa Elimu Mkoa wa Arusha, Mwl. Sara Mlaki, amesema kuwa, kati ya watahiniwa hao 29,508, wasichana ni  16,222 na wavulana ni 13, 286.

Aidha, wanafunzi 28,209, wavulana ni 12,769 na wasichana 15,440, ni watahiniwa wa shule 'school candidates' watakaofanya mtihani kwenye shule 255 za Serikali na binafsi kukiwa na mikondo 760 huku Wanafunzi 1,299 wavulana 517 na wasichana  782, ni watahiniwa wakujitegemea 'Private candidates'  watakaofanya mtihani kwenye vituo 61 vilivyoanishwa vikiwa  na mikondo 54.

Afisa Elimu Mlaki amebainisha kuwa,  maandalizi yote yamekamilika ikiwemo uwepo wa vifaa vyote muhimu pamoja na wasimamizi wote kupatiwa semina elekezi, na kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kwa kuhakikisha mahitaji yote muhimu ikiwemo rasilimali fedha kutolewa kwa wakati.

Hata hivyo Afisa Elimu huyo, amewasisitiza wasimamizi wote wa mtihani kuwa waadilifu kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na taratibu za mtihani wa Taifa na kuwaasa kutojihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na maadili ya utumishi wa Umaa, kwa kutambua kuwa kazi wanayoifanya ni kwa maslahi mapana ya watoto wakitanzania ambao wanategemewa kuwa ndio wajenzi wa Taifa lao

Sambamba na hilo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe Paul Christian Makonda Makonda  wanawatakia kila la kheri wahitimu wote waweze kufanya mtihani wao vyema na kufaulu vizuri pamoja na kuwakumbusha watahiniwa wote kuzingatia maelekezo na kujiepusha na aina yoyote ya vitendo vya udanganyifu.

 


Kituo cha kuhudumia Wazee cha  Meru Elderly Iniativies kilichopo chini ya kanisa la International Evangelism,Shirika la  Dorcas Tanzania kwa Kushirikiana na  Chama cha waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha (AWM) wameandaa  kongamano maalum la kuadhimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wazee katoka maeneo mbali mbali na kusherehekea siku ya Wazee Duniani.

Kongamano hilo limefanyika kituo hicho kilichopo kata ya Kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa wazee mkoa huo.

Katibu wa chama cha wazee wilaya ya Arusha mwalimu Wiliam Ayo amesema kuwa wazee wana changamoto mbali mbali ikiwemo kukosa uwakilishi katika maeneo  mbali mbali  kwa kuwa Mabaraza Mengi ya kata hayapewi kipaumbele licha ya kuchagua wawakilishi.

"Kwa kweli katika mkoa wetu wa Arusha bado hatushirikishwi katika maeneo mengi serikali iliagiza kuundwa kwa mabaraza ya kata mpaka wilaya tumechagua wawakilishi lakini bado wazee wengi hawashirikishwi na pia tunaomba mafunzo maalum ili wajue wajibu wao ndani ya mabaraza hayo"Alisema Ayo

Pia bw.Ayo ameomba serikali kuhakikisha kuwa inakamilisha mchakato wa utoaji wa vitambulisho wazee ndani ya wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine aliomba kuhakikisha uwakilishi wa wazee na kupewa nafasi zao  katika vikao vya maamuzi katika ngazi zote na pia kuwepo kwa mhudumu maalum katika vituo vya afya ambae atahudumia wazee tu.

Nae Askofu  Mkuu wa kanisa la International Evangelism lililopp sakila wilyani Arumeru  Eliud Isangya amewataka vijana kuhakikisha kuwa wanawapa chakula wazee ili kupata baraka zao.

Askofu Isangya amesema kuwa katika ngazi ya familia ni muhimu kuwaenzi wazee kwa kuhakikisha kuwa kila familia inatimiza wajibu wake na kupunguza changamoto kwa wazee.

"Ikiwa familia zitashindwa kuangalia familia basi mzazi huyo atapata chakula kutoka kwa mpita njia na mpita njia atapata baraka za mzazi huyo hivyo watoto wahakikishe kuwa wanatumiza jukum hilo pindi wazazi wao wakiwa hai na wana uwezo wa kula"Alisisitiza Askofu

Nae Mratibu wa shirika la Meru Elderly Iniativies  Bi.Ruth Kaaya amesema kuwa wanahudumia wazee zaidi ya 1500,tangu kuanzishwa kwa shirika hilo wakiwemowalofadhiliwa na wasiofadhiliwa .

Pia amesema kwasasa shirika hilo linahudumia jumla ya wazee waliofadhiliwa 255,ambapo 57 wanaume na 198 wanawake ndani yao 7 wanaishi kituoni hapo ambapo wanaume ni 5 na wanawake wawili.

Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Arumeru mheshimiwa Amir Mkalipa ambaye ni Afisa Tarafa ya Poli  bw.Jiliki Japhet Milinga amesema kuwa serikali itakuwa bega kwa bega na wazee kwa kuwa ni Hazina na pia imepokea changamoto hizo na kuahidi kwenda kuzitafutia ufumbuzi.

Bw.Milinga amesema kuwa hauli mbiu ya mwaka huu 2024 isemayo"Tuimarishe huduma kwa wazee,wazeeke kwa heshima ina dhamira ya kuhakikisha kuwa fundi hilo linaendelea kuwa muhimu na kuendelewa kuboreshewa mahitaji mbali mbali ili kulinda heshima yao.

Katika hatua nyingine  katibu wa chama cha waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha (AWM) Bi.Ashura Mohamed ameiomba serikali kuendelea kuboresha huduma za wazee haswa huduma za Afya na kuendelea kuboresha sera ya wazee ili kuwapunguzia changamoto. 

Amesema kuwa kundi hilo linapitia wakati mgumu kutokana na mmomonyoko na maadili wa watoto kutelekeza wazazi wao na kuachia mzigo huo serikali pekee. 

"Tunaamini wazee hawa walitusaidia kujenga nchi kwa kujitolea kwao ndio tunaona Tanzania yetu nzuri hivyo basi tusaidiane na serikali kuhakikisha kuwa wazee wetu wanaishi kwa heshima na pia ikiwezekana wazee wapate pensheni kidogo kama ilivyo kwa wazee wetu kule Zanzibar. 

Pia Bi.Ashura ametumia fursa hiyo kuishukuru Halmashauri ya Meru kwa kubuni kampeni ya "MPISHE MZEE KWAMZA"katika hospitali ya wilaya ya Meru ili wazee wapewe kipaumbele katika huduma ya Afya.

 


Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Arusha DC, iliyoko Wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, Selemani Msumi ametangaza mapema watu watakaoruhusiwa kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024.

Amesema kuwa wenye sifa ya kugombea na nafasi za serikali za mitaa, lazima awe Raia wa Tanzania na mkazi wa eneo husika analogombea tena awe na umri kuanzia miaka 21 na kuendelea.

Sifa zingine, Msumi amesema Mgombea lazima awe na akili na timamu na awe alimepewa dhamana au mwanachama wa Chama wa siasa na zaidi awe na shughuli za kujipatia kipato lakini pia aweze kuandika na kusoma lugha ya Kiswahili au Kingereza.

Msumi ambae pia ni Mkurugenzi wa halmashauri wa Arusha Meru, ameyasema hayo wakati akitoa maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa Leo Septemba 26,2024 ikiwa ni siku 62 kabla ya siku ya uchaguzi huo Novemba 27 mwaka huu.

Mbali na hilo amesema wapiga kura watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale Watanzania waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na wakazi wa eneo husika lakini waliofikia umri wa miaka 18 na kuendelea na zaidi wawe na akili timamu.

"Fomu za kugombea zitatolewa na kutakiwa kurudishwa kuanzia Novemba Mosi hadi saba mwaka huu kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi ambapo uteuzi utafanyika Novemba nane na siku hiyo tutaanza kupokea mapingamizi kuhusu uteuzi kwa siku mbili hadi Novemba 10" amesema Msumi.

Amesema kuwa baada ya hapo wataanza kupokea rufaa na kutolewa maamuzi yake kuanzia Novemba 10 hadi 13.

"Baada ya mchakato huo wa uteuzi, kampeni rasmi za uchaguzi zitaanza Novemba 20 hadi 26 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12 hivyo niwaombe wananchi wenye sifa hizo hapo juu wahakikishe wanashiriki mchakato mzima hadi kupatikana viongozi wenye sifa" amesema Msumi.

Amesema nafasi zinazogombewa ni Mwenyeviti wa Mtaa, na vitongoji,  wajumbe watano ambao kati yao wajumbe wawili ni wanawake hivyo kuwataka watu wote washiriki Ili kukuza demokrasia na kuhakikisha upatikanaji wa viongozi Bora kwa maendeleo ya Taifa" amesema Msumi.

 

Uploading: 371712 of 670245 bytes uploaded.

KAMPUNI ya Orxy Gas Tanzania Limited inayozalisha na kusambaza nishati ya gesi za majumbani imemuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo kwa kutoa msaada wa mitungi midogo 600 kwa familia zenye Watoto wenye ulemavu.


Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na Mbunge huyo kwaajili ya kugawa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu Jijini Arusha jana, Meneja Masoko wa Orxy Gas  Peter Ndomba amesema msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiitoa kwa familia duni nchini lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuokoa mazingira yetu.

"Oryx tumekuwa tukishiriki kikamilifu katika kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za Rais DK.Samia Suluhu Hassan katika kufanikisha matumizi ya nishati safi.Tumekuwa tukishirikiana na Wabunge mbalimbali katika kuwezesha wananchi kupata mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake bure."

Akitoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati ya gesi, Ndomba kabla ya kugawiwa kwa mitungi ya Oryx ,Ndomba  amewatahadharisha watumiaji wa nishati hiyo kuwa makini na bidhaa hiyo kwa kutofunga milango wakati wa matumizi ili kuepuka athari kubwa endapo itatokea ikalipuka.

" Ukiwa nyumbani wakati unatumia gesi hakikisha milango Iko wazi ili hewa iweze kuingia na kutoka, lakini pia gesi yetu imetengenezwa kwa kuwekwa harufu kama yai viza, lengo ni kama ikatokea gesi ikavuja ni rahisi kusikia harufu tofauti na mtumiaji kuchukua tahadhari," Amesema.

Kwa upande wake Mbunge Mrisho Gambo amewashukuru wadau mbalimbali kujitokeza kugawa vifaa pamoja na mitungi ya Oryx kwa familia zenye watoto wenye mahitaji Maalumu.

Akizungumzia msaada wa Orxy Gambo amesema kampuni hiyo imekuwa ikiendeshwa na watu waungwana kwa kuwa alipopeleka ombi lake walilifanyia kazi bila kuuliza maswali mengi tofauti na kampuni zingine.

" Nawashukuru Orxy kwa msaada huu wa mitungi ya gesi, nilivyoleta maombi kwenu mliyapokea kwa haraka lakini kampuni zingine zilianza kunihoji kwamba endapo tu kununua hawawezi, je gesi ikiisha wataweza kuijaza?, ...jamani ndugu zangu kwani hapa mlipofikia mmekuwa mkiishi kwa misaada hii tu?," Gambo aliwahoji wanufaika wa misaada hiyo.

Amesema  mitungi hiyo itawarahisishia katika huduma ya nishati kwa kuwa wakati mwingine imekuwa ikiwawia ugumu sana kupata nishati ya kupikia kwa haraka hususani mtoto anapokuwa anasumbuliwa na maradhi na anatakiwa kupelekwa kupata huduma za Afya.

" Zoezi hili sio mara ya kwanza kulifanya hapa Arusha, tangu nimekuwa Mbunge mwaka 2000 tumekuwa tukigawa vifaa mbalimbali kwa walemavu lakini pia tumekuwa na utaratibu wa kusaidia kulipia bima ya Afya, namshukuru Rais Samia kwa kurejesha Bima kwa watoto, hii imesaidia sana," amesema.

Amesema katika zoezi hilo la ugawaji wa vifaa tiba, Watoto 600 watapatiwa bima ya Afya ambapo kati yake yeye binafsi amelipia Watoto 210, mfanyabiashara Atul Mittal amelipia Watoto 100, Satbir HansPaul pamoja na marafiki zake Watoto 100 na Jiji la Arusha kupitia kwa mkurugenzi wake Juma Hamsini wamelipia Watoto 200.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Hamisi Hamduni  amesema ofisi yake imeamua kumuunga mkono Mbunge huyo kwa kuwa kazi anayoifanya ni sadaka kwa Mungu lakini pia anatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

"Kwa kuwa kazi hii inayofanywa na Mbunge ni kazi ya Mungu sisi kama Jiji tunamuunga mkono na tunaahidi kulipia bima ya Afya Watoto 200 pamoja na baiskeli mwendo (wheel chair), tatu, hivyo Jumatatu nitakabidhi hundi ya milioni 11," amesema.