Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Viongozi Wanawake Duniani (WPL) na Mbunge mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Neema Lugangira, amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo wa Kumi na Nne, katika makazi yake binafsi jijini Vatican, Italia, leo Jumamosi, Agosti 23, 2025.
Hii ni mara ya kwanza kwa Neema Lugangira kukutana na Papa Leo wa Kumi na Nne, ikiwa ni siku chache tu tangu ateuliwe rasmi kuwa Katibu Mkuu wa WPL, nafasi ya juu inayomweka kuwa Mtanzania wa kwanza kuiongoza jumuiya hiyo yenye makao yake makuu Brussels, Ubelgiji.
Neema Lugangira pia aliwahi kupata heshima ya kukutana na Marehemu Papa Francis mwaka 2023, hatua inayodhihirisha nafasi yake ya kimataifa na ushawishi wake katika masuala ya uongozi, jinsia na maendeleo.
Post A Comment: