Articles by "NEEMALUGANGIRA"
Showing posts with label NEEMALUGANGIRA. Show all posts

 


Mbunge mstaafu na mdau wa masuala ya teknolojia na maendeleo ya kidijitali, Neema Lugangira, amepata heshima ya kuteuliwa tena na Katibu Mkuu wa United Nations kuhudumu katika Kamati ya Ushauri kuhusu masuala ya utawala wa mtandao duniani pamoja na maendeleo ya kidijitali.

Kamati hiyo ya kimataifa ina jukumu la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu namna bora ya kuimarisha ushirikiano wa kidijitali, usalama wa mtandao, upatikanaji wa teknolojia, pamoja na kuhakikisha maendeleo ya kidijitali yanawanufaisha watu wote duniani kwa usawa.

Akizungumzia uteuzi huo, wachambuzi wa masuala ya teknolojia wameeleza kuwa nafasi hiyo ni ishara ya kuongezeka kwa ushawishi wa Watanzania katika majukwaa ya kimataifa yanayojadili mustakabali wa dunia ya kidijitali.

Neema Lugangira amekuwa mmoja wa viongozi wanaosukuma ajenda ya matumizi ya teknolojia, ubunifu wa kidijitali pamoja na ujumuishaji wa wananchi katika uchumi wa kidijitali nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Uteuzi huo pia unatajwa kuwa fursa muhimu kwa Tanzania kuendelea kushiriki katika maamuzi na mijadala ya kimataifa kuhusu sera za teknolojia, mtandao na maendeleo ya kidijitali katika dunia inayobadilika kwa kasi.



Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Viongozi Wanawake (WPL) Mhe. Neema Lugangira ameendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia inayolenga kulinda afya na kutunza mazingira miongoni mwa Watanzania.

Lugangira ameyasema hayo wakati akikabidhi mitungi ya gesi katika makundi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa chama cha bodaboda,madereva taxi sambamba na vijana waliojiari katika migahawa (wauzachipsi) katika Manispaa ya Bukoba.

“Moja ya changamoto zinazoleta athari ya afya na kusababisha vifo kwa akina mama ni matumizi ya nishati isiyo safi mfano kuni na mkaa ambavyo vinatoa hewa isiyofaa naakina mama wa Tanzaniawamekuwa wakiathirika kwa kuvuta hewa hiyo lakini pia ukataji miti unaharibu mazingira yetu,” amesema Lugangira

Kwa upande wake Danstan ambaye ni mwakilishi wa kundi la vijana waliojiajiri katika migahawa amempongeza Neema Lugangira kwa kuwakumbuka na kuwapatia nishati safi ya kupikia.

"Tunamshukuru sana Lugangira kwa kutuletea mitungi hii ambayo ni rafiki kwa mazingira, sasa tutapika kwa wakati mfupi,tunakushukuru kwa kuwajali wananchi wa Bukoba kwa sasa tunakwenda kutumia mitungi ya kisasa" Amesema Danstan

Hata hivyo wananchi wa Bukoba wamempongeza Neema Lugangira kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa WPL kwani alifanya kazi nzuri sana wakati akiwa Mbunge aliyewakilisha Kundi la NGO’s kwa kuwa kinara katika kuchangia maendeleo katika jamii.















Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Viongozi Wanawake Duniani (WPL) na Mbunge mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Neema Lugangira, amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo wa Kumi na Nne, katika makazi yake binafsi jijini Vatican, Italia, leo Jumamosi, Agosti 23, 2025.

Hii ni mara ya kwanza kwa Neema Lugangira kukutana na Papa Leo wa Kumi na Nne, ikiwa ni siku chache tu tangu ateuliwe rasmi kuwa Katibu Mkuu wa WPL, nafasi ya juu inayomweka kuwa Mtanzania wa kwanza kuiongoza jumuiya hiyo yenye makao yake makuu Brussels, Ubelgiji.

Neema Lugangira pia aliwahi kupata heshima ya kukutana na Marehemu Papa Francis mwaka 2023, hatua inayodhihirisha nafasi yake ya kimataifa na ushawishi wake katika masuala ya uongozi, jinsia na maendeleo.



Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Viongozi Wanawake duniani (WPL), Neema Lugangira ameshauri wahariri kuhakikisha wanatumia kwa usahihi teknolojia ya Akili Unde (AI) wakati wa Uchaguzi Mkuu kuepusha madhara katika vyombo vya habari.

Akitoa mada ya 'Uchaguzi Mkuu na Matumizi ya AI'  kwenye mkutano wa kawaida wa TEF, jijini Dar es Salaam ameeleza katika uchaguzi kuwa kuna taarifa nyingi potofu hivyo AI inaweza kutumika vizuri kuhakiki usahihi wa taarifa.

"Kuna faida nyingi za kutumia AI ikiwemo kusaidia kuhakiki taarifa kwa haraka, kufuatilia kauli za uchochezi hata uchambuzi wa data," amesema.

Lugangira ameendelea kueleza kuwa licha ya AI kuwa na matumizi makubwa kwenye dunia ya sasa, pia hutumika kupotosha jamii sambamba na kuharibu heshima ya mtu ama mgombea katika jamii.

Hata hivyo amesisitiza kwamba, vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kulinda maadili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Sambamba na hayo Lugangira alikabidhi nakala 40 kwa Jukwaa la Wahariri na 20 kwa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) za mwongozo wa Jumuiya ya Tume za Uchaguzi Afrika (AAEA) kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na Teknolojia kwenye chaguzi barani Afrika ambapo miongozo hiyo alishiriki kuiandaa wakati akiwa mjumbe wa timu ya wataalamu mwaka wa 2022/2023.






 

Aliyekuwa Mbunge Viti Maalum, Neema Lugangira amenza kazi jijini Brussels kama Katibu Mkuu wa Women Political Leaders (WPL) — Jumuiya ya Kimataifa ya Viongozi Wanawake: Marais, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Mawaziri, Wabunge na Mameya/Wenyeviti wa Halmashauri; ambapo wanalenga kuongeza uwakilishi wa wanawake katika siasa na kuimarisha sauti, ushawishi na aina ya uongozi wao katika nyanja na sekta mbalimbali. #UongoziUnaopimika

 


Neema Lugangira aliyekuwa Mbunge Viti Maalum CCM - Kundi la NGOs amechukua Fomu ya Kugombea Ubunge wa Viti Maalum NGOs katika Uchaguzi ujao 2025. 

Lugangira anatetea nafasi aliyoitumikia katika Bunge la 12, 2020-25 kwa mafanikio makubwa yaliyopelekea CCM kuongeza nafasi ya Uwakilishi kwa Kundi hili kutoka kuwa moja Tanzania Bara na moja Zanzibar hadi sasa ni nafasi mbili kwa upande wa Tanzania Bara na nafasi moja kwa upande wa Zanzibar.

Fomu hizo amekabidhiwa leo tarehe 28 Juni na Mkuu wa Idara ya UWT Taifa ya Oganaizesheni, Itikadi na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Mary Mwenisongole katika Ofisi za Makao Makuu ya UWT, Dodoma.




 MBUNGE wa Viti Maalum,Neema Lugangira ameshauri Serikali ipunguze gharama ambazo zisizo za lazima katika bajeti yake.


Ushauri huo ameutoa leo Juni 17,2025,bungeni wakati alichangia mjadala wa bajeti Kuu ya Serikali.

"Nashauri serikali ione namna ya kufanya tathmini ya gharama zake zote ili iweze kuondoa gharama ambazo sio za lazima,”amesema na kuongeza

“Spika alishawahi kunisemea bungeni utakuta magari ya serikali yanaweza yakakaa yana nguruma hata saa nne hadi tano serikali inaingia gharama ya mafuta pasipo ulazima kwa hiyo niombe sana serikali ikafanya tathmini ya gharama zake za uendeshaji na iweze kuondoa,”amesema Mbunge huyo

Kuhusu mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali, Mbunge huyo alisema bado yanapata changamoto katika sheria ya kodi ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshindwa kutofautisha kati ya biashara na Ngo’s.

“TRA inatambua Ngo’s kama ni biashara jambo ambalo linaleta changamoto kubwa na mkanganyiko mkubwa kwa hiyo niombe sana serikali kwa kutambua kwamba tayari Tanzania imepata mtikisiko ambao serikali inajitahidi kuhimili kufuatia mabadiliko ya fedha za wahisani, ni muhimu sasa sheria ya kodi ibadilishwe ili itofautishe kati ya Ngo’s na biashara,”amesema Mbunge huyo

 


Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamenufaika na elimu ya akili mnemba yatakayowawezesha kutumia teknolojia mpya  katika kuharakisha upatikanaji wa maendeleo. 

Akizungumza katika Semina iliyofanyika Jijini Dodoma Mwakilishi wa Afrika, wa Women Political Leaders (WPL) Mb. Neema Lugangira amesema fursa hiyo ya mafunzo juu ya matumizi ya akili mnemba (AI) ambayo ni sehemu ya mradi Barani Afrika unaojulikana kama Female AI Leaders (FemAI) unalenga kuchagiza na kuimarisha uwezo na uelewa wa viongozi wanawake katika siasa na maendeleo yao kwa ujumla kwa kutumia teknolojia kama akili mnemba.

Aidha, ameongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kufahamu vyema mifumo ya nchi kisera na kisheria kwa kutumia teknolojia mpya  kama akili mnemba. 

"Ni muhimu sana kwetu viongozi na wabunge tujue namna ya kutumia teknolojia mpya ya akili mnemba maana hatua hii itatusaidia kurahisisha kazi zetu na kutekeleza majukumu yetu" amesema Mbunge Lugangira. 

Vilevile amebainisha kuwepo kwa fursa mbalimbali zinazotokana na matumizi ya akili mnemba katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, na nyinginezo sambamba na changamoto za matumizi ya AI pale yasipotumika kwa umakini kama kusababisha ukatili wa kijinsia, kurubuni watoto na kufifisha uwezo wa kufikiri na kuwa tegemezi. 

"Katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu Oktoba  25, sisi kama wabunge itatusaidia kuandaa mikakati ya kampeni katika maeneo yetu na uzuri tulifanya jaribio na  tukajiinea AI inavyofanya kazi" ameeleza Mb.Lugangira.

Hata hivyo ameshukuru kufanikisha semina hiyo kupitia Shirika lake la OMUKA Hub kwa ushirikiano mkubwa wa Bunge la Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kaamti ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Fatma Toufiq akimwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Tulia Ackson  Mwansansu, amesema matumizi ya Akili mnemba (AI) ni ya muhimu kwenye kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kilimo, mazingira na Bunge inayachukulia kwa uzito na wanajipanga kuandaa   sera na sheria za usimamizi. 

"Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefurahi kuwa sehemu ya kunufaika na mafunzo haya ya teknolojia ya Akili mnemba" amesema Mb. Fatma. 

Katika namna hiyo hiyo Mbunge wa Iringa mjini Jesca Msambatavangu aliyeshiriki semina hiyo amesema ni muhimu kukubaliana na mabadiliko ya teknolojia ili kwenda Dunia inavyotaka. 

"Tulikuwa tukitumia akili bandia bila kujua, mfano matumizi ya (Google) na kutupatia taarifa, unaweza kuona kwamba si kitu kigeni kwani tumeelezwa kuwa matumizi ya akili bandia yameanza zamani sana mnamo mwaka 1950, kwetu hii ni fulsa kubwa na mimi kama Mbunge nitaweza kuwafundisha wanawake wenzangu faida na namna ya kukabiliana na changamoto za Matumizi ya akili bandia" amefafanua Mbunge Msambatavangu













Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, amekutana na kufanya mazungumzo na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) katika Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma.

Katika kikao hicho, Ndg. Rabia alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali pamoja na kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Asasi za Kiraia walioratibiwa na Mhe Neema Lugangira, Mbunge wa Viti Maalum CCM Kundi la NGOs. 

Miongoni mwa waliokutana naye ni pamoja na Baraza la Taifa la NGOs (NACONGO), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, wawakilishi wa Machinga, na Chama cha Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA).

Akizungumza katika kikao hicho, Ndg. Rabia aliwataka wadau wa asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuendeleza mshikamano na kushirikiana kwa karibu katika kuunga mkono juhudi za maendeleo. Alisisitiza umuhimu wa kuelekeza nguvu kwa pamoja katika kupambana na changamoto za umasikini, maradhi na ujinga, ili kujenga taifa lenye ustawi na haki kwa wote.