Mbunge mstaafu na mdau wa masuala ya teknolojia na maendeleo ya kidijitali, Neema Lugangira, amepata heshima ya kuteuliwa tena na Katibu Mkuu wa United Nations kuhudumu katika Kamati ya Ushauri kuhusu masuala ya utawala wa mtandao duniani pamoja na maendeleo ya kidijitali.
Kamati hiyo ya kimataifa ina jukumu la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu namna bora ya kuimarisha ushirikiano wa kidijitali, usalama wa mtandao, upatikanaji wa teknolojia, pamoja na kuhakikisha maendeleo ya kidijitali yanawanufaisha watu wote duniani kwa usawa.
Akizungumzia uteuzi huo, wachambuzi wa masuala ya teknolojia wameeleza kuwa nafasi hiyo ni ishara ya kuongezeka kwa ushawishi wa Watanzania katika majukwaa ya kimataifa yanayojadili mustakabali wa dunia ya kidijitali.
Neema Lugangira amekuwa mmoja wa viongozi wanaosukuma ajenda ya matumizi ya teknolojia, ubunifu wa kidijitali pamoja na ujumuishaji wa wananchi katika uchumi wa kidijitali nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Uteuzi huo pia unatajwa kuwa fursa muhimu kwa Tanzania kuendelea kushiriki katika maamuzi na mijadala ya kimataifa kuhusu sera za teknolojia, mtandao na maendeleo ya kidijitali katika dunia inayobadilika kwa kasi.

Post A Comment: