Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Viongozi Wanawake (WPL) Mhe. Neema Lugangira ameendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia inayolenga kulinda afya na kutunza mazingira miongoni mwa Watanzania.

Lugangira ameyasema hayo wakati akikabidhi mitungi ya gesi katika makundi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa chama cha bodaboda,madereva taxi sambamba na vijana waliojiari katika migahawa (wauzachipsi) katika Manispaa ya Bukoba.

“Moja ya changamoto zinazoleta athari ya afya na kusababisha vifo kwa akina mama ni matumizi ya nishati isiyo safi mfano kuni na mkaa ambavyo vinatoa hewa isiyofaa naakina mama wa Tanzaniawamekuwa wakiathirika kwa kuvuta hewa hiyo lakini pia ukataji miti unaharibu mazingira yetu,” amesema Lugangira

Kwa upande wake Danstan ambaye ni mwakilishi wa kundi la vijana waliojiajiri katika migahawa amempongeza Neema Lugangira kwa kuwakumbuka na kuwapatia nishati safi ya kupikia.

"Tunamshukuru sana Lugangira kwa kutuletea mitungi hii ambayo ni rafiki kwa mazingira, sasa tutapika kwa wakati mfupi,tunakushukuru kwa kuwajali wananchi wa Bukoba kwa sasa tunakwenda kutumia mitungi ya kisasa" Amesema Danstan

Hata hivyo wananchi wa Bukoba wamempongeza Neema Lugangira kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa WPL kwani alifanya kazi nzuri sana wakati akiwa Mbunge aliyewakilisha Kundi la NGO’s kwa kuwa kinara katika kuchangia maendeleo katika jamii.















Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: