Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Japan kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika maendeleo ya rasilimali watu hususan kwenye sekta ya ujenzi.


Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zimejadili fursa za kuboresha ujuzi wa wataalam wa sekta ya ujenzi kupitia mafunzo, kubadilishana uzoefu na programu maalumu za kukuza uwezo. 

Aidha, Ujumbe wa Japan umeonesha utayari wa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha nguvu kazi ya Kitanzania inakuwa na weledi unaokidhi mahitaji ya soko la kimataifa.


Mazungumzo hayo yamefanyika leo Novemba 24, 2025 Jijini Dar es salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mohmoud Thabit na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Bi. Zuhura Yunus wamehudhuria mazungumzo hayo.





Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: