Magesa Magesa ,Arusha .

WIZARA  ya maji imesema kwamba itahakikisha idadi kubwa ya watanzania walioko mjini na vijijini wanapata maji safi salama na ya uhakika .

Waziri wa maji Jumaa Aweso ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua kongamano la maji la mwaka 2025 lililoandaliwa na Taasisi ya huduma za maji (ATAWAS )  linaloendelea mjini hapa .

Aweso amesema kuwa, amewataka watwndaji na watumishi wote wa sekta ya maji nchini kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuondoa  changamoto ya upatikanaji wa maji kwa watanzania hususani maeneo ya vijijini.

"Katika kongamano hili nataka mhakikishe mnaweka mikakati kwa kushirikisha sekta binafsi na za umma ili kupunguza mbalimbali zinazoikabili sekta ya maji hapa nchini "amesema Aweso.

Amesema kuwa, katika utendaji kazi wao hawawezi kufanya kazi wenyewe bali ni lazima washirikiane na sekta binafsi katika kuweka mikakati madhubuti  namna ya utendaji kazi wao na hatimaye kwa pamoja kuweza kufikia malengo yaliyowekwa .

 Akimkaribisha Waziri wa maji ,Katibu mkuu wa wizara hiyo Mwajuma Waziri amewataka watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu mikakati na mipango iliyowekwa na wizara hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya maji safi na salama .

"Dira ya Taifa ya mwaka 2025 inasema kwamba ifikapo mwaka 2050 nchi yetu iwe na uhakika wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa asilimia mia moja ,hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anawajibika kikamilifu katika eneo lake."amesema .

Kadhalika amewataka wataalamu kuhakikisha wanaweka mipango mikakati ikiwemo kutoa elimu ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kutengeneza miundombinu ya kuhifadhia maji hayo hali itakayosaidia kutatua changamoto ya upungufu wa maji hususani katika taasisi mbalimbali za kiserikali ikiwemo mashule,mahospitali nk.

Mwenyekiti wa bodi ya ATAWAS, Geofrey Hilly amesema kuwa mkutano huu ni  mwendelezo wa mikutano yote ambayo wamekuwa wakifanya kila mwaka ambapo Atawas  inashirikisha watu wa sekta ya maji kwa ujumla wake.

Hilly amesema kuwa ,lengo la kukutana leo ni kuangalia namna gani sekta binafsi itashiriki katika kuhakikisha huduma za maji zinasambaa kwa kasi .

Ameongeza  kuwa ,Atawas ni taasisi ambazo karibu kila nchi inakuwa na taasisi kama hii ikiwemo Malawi,Kenya na dunia nzima  na kwamba mkutano huu umeshirikisha taasisi za serikali na binafsi zinazojishughulisha ja shughuli za utafutaji na usambazaji wa maji pamoja na vifaa vyake
Share To:

Post A Comment: