Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid, akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Mafunzo ya Usimamizi wa Kimkakati wa Elimu Mwalimu Dennis John Otieno, ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) na pia Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilboru mkoani Arusha.

Mafunzo hayo ya Uongozi kwa Viongozi wa Elimu na Wakuu wa Shule yamefanyika katika chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo Bagamoyo.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Dkt. Maulid aliwapongeza washiriki kwa kujituma na kuonesha uzingatiaji mkubwa katika vipindi vya mafunzo. Aliwataka kuyazingatia na kuyatekeleza kwa vitendo maudhui waliyojifunza ili kuleta tija katika usimamizi wa taaluma, malezi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika taasisi zao.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: