NA DENIS MLOWE IRINGA 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kufanya mabadiliko ya sheria za kodi mwaka 2025 kwa kupunguza na kuongeza baadhi ya kodi katika sehemu 12 za vipengele kwenye kodi.

Moja ya sehemu ambazo TRA imeweza kuboresha suala la kodi ni kwenye kilimo ambapo Serikali imeongeza miaka 3 ya kutoza VAT kwa kiwango cha sifuri kwa wazalishaji wa ndani wa mbolea hadi June 2028. 
Akizungumza kwenye semina. Afisa Mwandamizi wa kodi kutoka TRA makao makuu, Alex Mwambenja alisema kuwa sheria imeongeza mwaka mmoja wa kutoza VAT kwa kiwango cha sifuri kwa wazalishaji wa nguo wanaotumia pamba zinazozalishwa nchini hadi Juni, 2026. 

 Alisema kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya mapato imeendelea kutoa msamaha wa VAT kwenye mafuta ya kula yanayozalishwa nchini na wazalishaji wa ndani kwa mbegu zinazozalishwa hapa nchini. 

Mwambenja amefafanua kuwa lengo la serikali kuendelea kutoa misamaha hiyo ya kodi ni kupunguza gharama na kuongeza tija katika kilimo, kuzuia mfumuko wa bei za bidhaa na kuongeza soko la uhakika kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Alisema kuwa sheria za Kodi zilizorekebishwa ni sheria ya Malipo ya Huduma ya Uwanja wa Ndege, Sura. 365 , Sheria ya Ushuru wa bidhaa, Sura. 147, Sheria ya Kodi ya Mauzo ya Nje, Sura. 196 na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura. 41 

Aliongeza kuwa sheria nyingine Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332 ,Sheria ya Udhibiti wa Uagizaji, Sura. 276 ,Sheria ya Magari (Kodi ya Usajili na Uhamisho) Sura. 124 Sheria ya Tozo ya Huduma ya Bandari, Sura. 264 

Aidha sheria zilizorekebishwa ni sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, Sura ya 399 Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 
Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, Sura. 220 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura ya. 148 

Akizungumzia sheria ya malipo ya huduma ya uwanja wa ndege imerekebisha malipo ya huduma kama kwa kuongeza malipo kutoka Sh. 10,000 hadi Sh. 11,000 hii ni Ada kwa abiria wanaosafiri ndani ya na abiria wanaosafiri nje imepanda kutoka dola 40 hadi dola 40.4.

Alisema kuwa mapato kutokana na ongezeko hilo yanalenga kufadhili Mfuko wa Udhamini wa Ukimwi (ATF) na Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote

Mabadiliko ya siku ya kuwasilisha ritani na kulipa ada kutoka siku ya mwisho ya kazi hadi siku ya 20. 

Kwa upande wake meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa, Peter Jackson awali alisema kuwa lengo la semina hiyo iliyowakutanisha wafanyabiashara na wanahabari kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu mabadiliko ya Sheria ya Kodi yaliyoanza kutekelezwa Julai 1, mwaka huu.

Jackson alisema utaratibu huo ni sehemu ya mpango wa TRA wa kuwakutanisha walipa kodi ili kuwafahamisha mabadiliko yanayotokea sambamba na kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Aidha, aliwapongeza wafanyabiashara kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kudumisha ushirikiano, akisisitiza kuwa mshikamano huo unachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato ya mkoa na nchi kwa ujumla
Share To:

Post A Comment: