Kituo cha kuhudumia Wazee cha Meru Elderly Iniativies kilichopo chini ya kanisa la International Evangelism,Shirika la Dorcas Tanzania kwa Kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha (AWM) wameandaa kongamano maalum la kuadhimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wazee katoka maeneo mbali mbali na kusherehekea siku ya Wazee Duniani.
Kongamano hilo limefanyika kituo hicho kilichopo kata ya Kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa wazee mkoa huo.
Katibu wa chama cha wazee wilaya ya Arusha mwalimu Wiliam Ayo amesema kuwa wazee wana changamoto mbali mbali ikiwemo kukosa uwakilishi katika maeneo mbali mbali kwa kuwa Mabaraza Mengi ya kata hayapewi kipaumbele licha ya kuchagua wawakilishi.
"Kwa kweli katika mkoa wetu wa Arusha bado hatushirikishwi katika maeneo mengi serikali iliagiza kuundwa kwa mabaraza ya kata mpaka wilaya tumechagua wawakilishi lakini bado wazee wengi hawashirikishwi na pia tunaomba mafunzo maalum ili wajue wajibu wao ndani ya mabaraza hayo"Alisema Ayo
Pia bw.Ayo ameomba serikali kuhakikisha kuwa inakamilisha mchakato wa utoaji wa vitambulisho wazee ndani ya wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine aliomba kuhakikisha uwakilishi wa wazee na kupewa nafasi zao katika vikao vya maamuzi katika ngazi zote na pia kuwepo kwa mhudumu maalum katika vituo vya afya ambae atahudumia wazee tu.
Nae Askofu Mkuu wa kanisa la International Evangelism lililopp sakila wilyani Arumeru Eliud Isangya amewataka vijana kuhakikisha kuwa wanawapa chakula wazee ili kupata baraka zao.
Askofu Isangya amesema kuwa katika ngazi ya familia ni muhimu kuwaenzi wazee kwa kuhakikisha kuwa kila familia inatimiza wajibu wake na kupunguza changamoto kwa wazee.
"Ikiwa familia zitashindwa kuangalia familia basi mzazi huyo atapata chakula kutoka kwa mpita njia na mpita njia atapata baraka za mzazi huyo hivyo watoto wahakikishe kuwa wanatumiza jukum hilo pindi wazazi wao wakiwa hai na wana uwezo wa kula"Alisisitiza Askofu
Nae Mratibu wa shirika la Meru Elderly Iniativies Bi.Ruth Kaaya amesema kuwa wanahudumia wazee zaidi ya 1500,tangu kuanzishwa kwa shirika hilo wakiwemowalofadhiliwa na wasiofadhiliwa .
Pia amesema kwasasa shirika hilo linahudumia jumla ya wazee waliofadhiliwa 255,ambapo 57 wanaume na 198 wanawake ndani yao 7 wanaishi kituoni hapo ambapo wanaume ni 5 na wanawake wawili.
Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Arumeru mheshimiwa Amir Mkalipa ambaye ni Afisa Tarafa ya Poli bw.Jiliki Japhet Milinga amesema kuwa serikali itakuwa bega kwa bega na wazee kwa kuwa ni Hazina na pia imepokea changamoto hizo na kuahidi kwenda kuzitafutia ufumbuzi.
Bw.Milinga amesema kuwa hauli mbiu ya mwaka huu 2024 isemayo"Tuimarishe huduma kwa wazee,wazeeke kwa heshima ina dhamira ya kuhakikisha kuwa fundi hilo linaendelea kuwa muhimu na kuendelewa kuboreshewa mahitaji mbali mbali ili kulinda heshima yao.
Katika hatua nyingine katibu wa chama cha waandishi wa habari wanawake mkoa wa Arusha (AWM) Bi.Ashura Mohamed ameiomba serikali kuendelea kuboresha huduma za wazee haswa huduma za Afya na kuendelea kuboresha sera ya wazee ili kuwapunguzia changamoto.
Amesema kuwa kundi hilo linapitia wakati mgumu kutokana na mmomonyoko na maadili wa watoto kutelekeza wazazi wao na kuachia mzigo huo serikali pekee.
"Tunaamini wazee hawa walitusaidia kujenga nchi kwa kujitolea kwao ndio tunaona Tanzania yetu nzuri hivyo basi tusaidiane na serikali kuhakikisha kuwa wazee wetu wanaishi kwa heshima na pia ikiwezekana wazee wapate pensheni kidogo kama ilivyo kwa wazee wetu kule Zanzibar.
Pia Bi.Ashura ametumia fursa hiyo kuishukuru Halmashauri ya Meru kwa kubuni kampeni ya "MPISHE MZEE KWAMZA"katika hospitali ya wilaya ya Meru ili wazee wapewe kipaumbele katika huduma ya Afya.
Post A Comment: