Kila usiku nilipozima taa na kujaribu kulala, nilihisi kama macho fulani yananitazama gizani. Mara nyingi ningejigeuza kitandani, nikafunika kichwa kwa shuka, lakini hisia ile haikuondoka. Nilihisi sauti za minong’ono zikiniita majina yangu, wakati mwingine miguu ikitembea sebuleni ilhali nilikuwa peke yangu nyumbani. Mwanzoni nilidhani ni mawazo yangu tu, lakini mambo yalizidi kuwa mabaya.
Kila saa sita usiku, nilihisi kivuli kizito kikisimama pembeni ya kitanda changu. Mara nyingine niliona kama ni mtu mrefu amevaa mavazi meusi, uso wake haukuwa na maumbile. Ningejaribu kupiga kelele, lakini sauti yangu haikutoka.
Nilijikuta nikipumua kwa shida, nikihisi kama kuna kitu kimenikalia kifuani. Asubuhi, nilipoamka, nilikuwa nimechoka mno kana kwamba sikulala kabisa.
Familia yangu haikunielewa. Wengine walidhani labda ninasumbuliwa na msongo wa mawazo au labda nimezidi kuamini hadithi za usiku. Lakini mimi nilijua hii haikuwa ndoto wala mawazo. Nyumbani nilianza kuhisi baridi kali isiyo ya kawaida, hata wakati wa mchana. Vitu vilianguka bila mtu kugusa, na mara nyingine taa ziliwaka na kuzimika zenyewe. Soma zaidi hapa
Post A Comment: