MBEYA ITANUFAIKA NA MATIBABU BURE KIKAMILIFU KWA WASIO NA UWEZO

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kusisitiza ahadi ya kuanzisha mfuko maalumu wa kugharamia matibabu ya maradhi makubwa na ya kibingwa kwa wananchi wasiokuwa na uwezo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mbeya Mjini leo, Septemba 4, 2025, Dkt. Samia amesema mfuko huo utagharamia kikamilifu matibabu ya saratani, magonjwa ya moyo, figo, kisukari, mifupa na mishipa ya fahamu, ambayo kwa sasa yamekuwa yakigharimu fedha nyingi na kuwa kikwazo kwa wananchi wa hali ya chini.

“Tukihakikisha mtu hana uwezo, haya maradhi yatalipiwa kikamilifu na serikali,” amesema Dkt. Samia.

Katika hatua nyingine, Dkt. Samia amesema huduma za afya ya uzazi zitajumuishwa rasmi katika bima ya afya, jambo litakalosaidia wanawake wengi kupata huduma bila vikwazo. Hata hivyo, amesisitiza kuwa utaratibu huo utawahusu zaidi wananchi wasio na uwezo, huku wenye uwezo wakichangia gharama zao wenyewe.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: