Kufuatia changamoto ya kukaa umbali wa takribani KM 24 wanayokumbana nayo walimu wa shule ya msingi Deo Sanga iliyopo katika kijiji cha Manga halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

Hatimaye Changamoto hiyo inaelekea kupunguzwa kwa kiasi kikubwa mara baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho kukamilisha nyumba pacha yenye thamani ya Tshs 92,410,714.29

Akitoa taarifa ya ujenzi wa Nyumba hiyo mbele ya Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi,Liston Ngimilanga ambaye ni afisa Mtendaji wa kijiji cha Manga amesema ujenzi wa nyumba hiyo umefikia hatua ya umaliziaji ambapo mradi huo mpaka sasa umegharimu Shilingi 91,360,714.29

"Katika kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi wa kijiji cha Manga,kijiji kilipokea fedha hizo kutoka serikali kuu kupitia TASAF kwa ajili ya ujenzi wa nyumba pacha na hii ni baada ya wananchi kuibua na kuthibitisha mradi"amesema Ngimilanga

Awali Mwalimu Naboti Ilongo kutoka shule hiyo amesema mpaka sasa shule hiyo ina nyumba nne lakini mahitaji yao ni nyumba saba hivyo mara baada ya ujenzi wa nyumba hiyo kutakuwa na mahitaji ya nyumba moja kwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya walimu kutoka mjini Makambako wakifanya kazi katika shule hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo amesema serikali imetoa kiasi hicho ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Manga na kupongeza kwa usimimizi wa mradi huo.

"Jengo ni zuri na hata umaliziaji wake umefanyika kwa umahili mkubwa,na kwa kweli niwashukuru CMC kwa kusimamia hii kazi na nina imani mwezi ujao mtakuwa mmemaliza hii kazi"amesema Ilomo

Share To:

Post A Comment: